Tatizo la maji Dar kuwa historia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la maji Dar kuwa historia

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Paddy, Mar 16, 2011.

 1. Paddy

  Paddy JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Mwandosya: Tatizo la maji Dar kuwa historia
  TUESDAY, 15 MARCH 2011 19:45 NEWSROOM
  NA MWANDISHI WETU

  TATIZO la maji Dar es Salaam litakuwa historia ndani ya kipindi cha miaka minne baada ya serikali kuidhinisha kuanza kwa mradi mkubwa wa kitaifa utakaogharimu sh. bilioni 654, imeelezwa. Mradi huo ulioidhinishwa rasmi na serikali juzi kuwa Mradi wa Kitaifa wa Maji Dar es Salaam, utahusisha ukarabati wa mitambo, utafutaji vyanzo vingine vya maji, utandazaji mabomba mapya, ujenzi wa mitambo ya kusafisha majitaka na ulipaji wa fidia kwa watakoathirika. Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya, alisema hayo jana ofisini kwake wakatialipozungumza na waandishi wa habari, kuhusu Wiki ya Maji inayoanza leo nchini kote.

  Profesa Mwandosya alisema katika jitihada za kutatua kero ya maji kwa wakazi wa Dar es Salaam na katika kutekeleza ahadi za Rais Jakaya Kikwete kufanya tatizo la maji kuwa historia kabla hajaondoka madarakani, utelekezaji wa mradi huo umeanza na umeidhinishwa rasmi.

  “Jambo la kufurahisha kwa wakazi wa Dar es Salaam ni kuwa serikali jana (juzi) imeidhinisha rasmi Mradi wa Kitaifa wa Maji Dar es Salaam, ambao utaondoa tatizo kubwa linalowakabili wananchi kwa sasa,” alisema Profesa Mwandosya.

  Alifafanua kuwa katika mradi huo mkubwa, utahusisha kuongeza vyanzo vya maji ambavyo havijawahi kuongezwa kwa zaidi ya miaka 35 na kuwa asilimia 80 ya fedha za mradi huo zitatolewa na serikali na zilizobaki zitachangiwa na washirika wa maendeleo.

  Kutokana na hali hiyo, serikali itatoa sh. bilioni 526 na washirika wa maendeleo watatoa sh. bilioni 128.

  Kuhusu kuongeza vyanzo vya maji, Profesa Mwandosya alisema vitachimbwa visima virefu vya hadi mita 500 huko Kimbiji na Mpera, ambavyo vitakuwa na uwezo wa kutoa lita milioni 10 kwa siku.

  Jingine ni ujenzi wa bwawa la Kidunda kwa ajili ya kuhifadhi maji ya Mto Ruvu ili yaweze kutumika wakati wa ukame ambapo usanifu wake utakamilika Juni, mwaka huu.

  Profesa Mwandosya alitaja hatua nyingine kuwa ni upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu ambao kwa sasa mhandisi anatafutwa kwa lengo la kuongeza uzalishaji kutoka lita milioni 82 hadi milioni 142 kwa siku na kujenga bomba kubwa kutoka Ruvu hadi Kimara Jaribu na Ubungo.

  Aliongeza bomba hilo litasaidia kusambaza maji kwa watu wanaoishi maeneo ya milimani kama vile Segerea, Kinyerezi, Kisukuru na kwingineko.

  Kuhusu upanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini, Mwandosya alisema mradi huo unatekelezwa kwa msaada wa serikali ya Marekani, lengo likiwa kuupanua kutoka utoaji wa maji lita milioni 182 hadi lita milioni 272 na kuwa tayari kampuni kutoka Ufaransa imepewa kazi hiyo.

  Mradi huo utahusisha kupitishwa kwa bomba jipya kubwa kutoka Ruvu Chini hadi kwenye matanki yaliyopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hivyo kusambaza katika maeneo mengine.

  Lingine litakalofanyika katika mradi huo mbali ya kulipa fidia ni ujenzi wa vituo vipya vya kusafisha majitaka vitakavyojengwa katika maeneo ya Msimbazi, Mbezi Beach na Kurasani na kuwa vituo hivyo vitatumia teknolojia ya kisasa ambayo haihitaji maeneo makubwa.

  Profesa Mwandosya alisema mradi huo unaanza sasa na unatarajiwa kukamilika Desemba 2013.

  Mei, mwaka jana, Rais Kikwete alifanya ziara ya mkoa wa Dar es Salaam ambapo alieleza nia yake ya kutaka kuona tatizo la maji linamalizwa Dar es Salaam ifikapo mwishoni mwa uongozi wake.

  Rais Kikwete alirudia ahadi yake hiyo wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu Oktoba 28, 2010 alipotembelea mkoa wa Dar es Salaam ambapo alisema anataka kuona baada ya kipindi kifupi, ‘tatizo la maji Dar linakuwa historia’.
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,780
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  The same Old Sh**ts!
   
 3. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 1,810
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Most of Places in Dar have been dry with no running tape water for the last four days..It irritates to read these kinds of planning stories.
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 56,810
  Likes Received: 19,317
  Trophy Points: 280
  Semeni, wenye vijiba vya roho. Huyo ndio JMK.
   
 5. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Tuliambiwa hadithi hii miaka 5 iliyopita hadi sasa hakuna dalili za mabadiliko. Hivi huyu waziri anamdanganya nani?
   
 6. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yetu macho. Maana mashairi haya sio mageni kwenye masikio ya wengi.

  Mabomba yametandazwa na wachina sehemu za Kimara, Makongo na nyingine zaidi ya miaka miwili lakini maji hayajawahi kutoka hata siku moja. Hii miradi haina sera endelevu. Sasa serikali inaweka vipi mabomba sehemu ambao hakuna maji. Tafuteni chanzo cha maji kwanza halafu ndiyo tuanze issue ya mabomba.
   
 7. F

  FUSO JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 10,455
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Tulishawahi kuambiwa Umeme utakuwa historia, Foleni Mabarabarani itakuwa historia - Mimi mpaka nione yanatoka hayo maji yenyewe.

  Wewe ukitaka kufanikisha jambo lako - njoo na hoja ya ahadi, watu wanaamini ahadi kuliko ukweli - hii ndiyo Tanganyika ya wadanganyika ipo tofauti na nchi nyingine duniani.
   
 8. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2011
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,484
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Why can't you ever be serious even once in your life? When are you going to grow up?
  These are the same same old songs year in year out ... na hakuna kinachofanyika.
   
 9. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,447
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kuongea tu wanaweza lakini kutekeleza ishu!tusubiri 2013 sio mbali maana tayari ameshajitia kitanzi. Na asipotekeleza ahadi yake ajitayarishe kujihudhuru maana wamezoea kuropoka halafu hakuna la maana wanalofanya
   
 10. M

  Matarese JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 514
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  upuuzi mtupu!
   
 11. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,546
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Bora wasiseme, watende
   
 12. g

  geophysics JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 904
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ni porojo tu au tuseme ni kampeni za 2015 zimeanza...... Can you make smart people believe on day dreams???? Kwani tatizo lilikuwa pesa au?
   
 13. J

  Jahom JF-Expert Member

  #13
  Jan 21, 2014
  Joined: Aug 26, 2008
  Messages: 336
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Naomba taarifa ya utekelezaji wa mradi huu haraka. Ni matarajio kuwa unatakiwa kuwa umefikia asilimia 75.
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Jan 21, 2014
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 12,944
  Likes Received: 881
  Trophy Points: 280
  Huu ni mwaka gani vile? I wish we cold proudly say "Actions speak louder than words"!
   
 15. komeka

  komeka JF-Expert Member

  #15
  Jan 21, 2014
  Joined: May 1, 2013
  Messages: 1,043
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hela zishaliwa ....chezea ccm ww
   
 16. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #16
  Jan 21, 2014
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,056
  Likes Received: 3,416
  Trophy Points: 280
  Sawa tumwona na kumsikia JK wa Msonga ha ha ha


   
 17. KIDOLEGUMBA

  KIDOLEGUMBA JF-Expert Member

  #17
  Jan 22, 2014
  Joined: Apr 17, 2013
  Messages: 504
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  siasa bana!
   
 18. J

  Jahom JF-Expert Member

  #18
  Jan 22, 2014
  Joined: Aug 26, 2008
  Messages: 336
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Naomba hiyo historia ya Maji Dar
   
 19. J

  Jahom JF-Expert Member

  #19
  Feb 5, 2014
  Joined: Aug 26, 2008
  Messages: 336
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hii historia itafundishwa hadi chuo kikuu?
  JanaTabata wamepata maji baada ya wiki moja kupita. Je wastani wa matumizi ya maji Tabata na kwingineko kwenye mgao kama wetu ni mara moja kwa wiki? Hizi siku nyngine mnategemea tunatumia nini? Hata kama mnadhani tuna vyombo vya kutosha kuhifadhia maji, ina maana kwa sisi wapangaji inabidi niongeze chumba kingine cha kuweka ndoo za maji. Maji ni lazima na haki ya msingi. Tunataka maji kila siku walau kwa saa moja, walau tunauwezo wa kutunza maji kwa masaa 23. Vinginevyo tunatumia maji ya visima vifupi na yake yenye kemikali tusizozifahamu. TUOKOENI NA JANGA LA MAJI DAR. WANAOFANYA BIASHARA ZA MAJI WATAFUTE KAZI NYINGINE.
   
 20. J

  Jahom JF-Expert Member

  #20
  Mar 21, 2014
  Joined: Aug 26, 2008
  Messages: 336
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  tunaendelea kuijenga hiyo historia na jana tumeona watu kwenye television wanasherehekea wiki ya maji. Naomba sana hizo sherhe ziletwe tabata na maeneo mengine yanayofanana kama mtatoka bila ngeu!!!!!!!!!!!
   
Loading...