Tatizo la mafuta!

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,772
8,958
Nachukua nafasi hii kueneza habari hii. Jamani nakuombeni tuipigie debe sana hasa mshikaji nakuomba Freeman Mbowe yapeleke mapendekezo haya Bungeni.

Nina imani kubwa kwamba tatizo la mafuta hasa nchi zetu za kiafrika ni tatizo la kujitakia! Kwa nini nasema hivi?

Kwanza kabisa ikiwa leo hao wataalamu wanaamini kwamba pombe inayotokana na mazao yetu (ethanol) inaweza kabisa kuendesha magari na mashine zote zinazotegemea petrol na diesel. Tunapozungumzioa swala la pombe nadhani sisi waafrika tuko mbele sana kwani hii ni jadi yetu toka Nabii Nuhu, sasa tunashindwa kutumia ujuzi na elimu tuliyojaaliwa bila kwenda darasani isipokuwa tunasubiri mzungu avumbue ndipo nasi tuanze kuiga! Huu ni upotofu wa viongozi wetu wasiokuwa wabunifu na wasiotakia kheri nchi yetu zaidi ya maslahi yao na utumwa wa mawazo. Brazil ambao walikuwa wakitegemea mafuta toka nje kwa asilimia 70, leo hii wamekaribia kabisa kujitegemea kwa matumizi ya ethanol... Sii jambo gumu ama laa ajabu!.. Who knows, labda Gongo linaweza kutuondoa ktk umaskini kuliko hiyo dhahabu.
Tazama tovuti hii ifuatayo na utaona hakuna kitu tunachoshindwa sisi kukifanya tena tukiweka na wasomi wetu ndio kabisaaa!

http://www.ethanolstill.com/
 
Mkandara,
Hiyo ni kweli kabisa. Kwa vile malighafi muhimu ni carbohydrate, wakulima wetu watanufaika sana na labda tunaweza kukwamuka toka kwenye lindi la umaskini. Kuna kampuni ambayo inajaribu kupromoti kilimo cha Jatropha for biodiesel production, sijui wamefikia wapi. I think its high time we seize these opportunities. War against poverty should be fought on all fronts
 
Habari zenu waheshimiwa!

Swali:

Hivi ukichukua hii ethanol na ukiiweka kwenye mashine inayotumia dizeli itafanya kazi ?
Kama itafanya kazi basi kweli sisi tumelala. Lakini sasa labda kuna solution.
 
Ogmulik,

Kwa hilo sina uhakika sana, inabidi kufanya kautafiti kidogo. Ila nilichosikia kwa wenzetu wa Brazil wamemodify engine za magari yao kuweza kucope na both conventional fuel pamoja na ethanol. Kwa maneno mengine unaweza kuweka any of the fuels hata kama zikichanganyika hakuna madhara yoyote kwa engine.
 
petroli lazima iwepo, ila tu biodiesel lazima u-blend na kiasi fulani cha petrol, siyo pure ethanol, no. Yaani inapunguza gharama za mafuta.
Ile gas ya Songo songo, vile vile ingeweza kutengezwa mafuta from gas to liquid technology ambapo hadi leo labda ni Sasol tu wenye hiyo technology.
 
..good idea lakini inabidi ufanye homework yako vizuri kabla ya kuja na idea kama hii....anyway Ethanol hatuwezi maana inatumia mahindi/carb na ukweli hata mahindi tuliyonayo hayatoshi kwa ugali wetu sasa unataka tufe njaa na kumbuka still bado tuna import unga,sasa hapo itakuwaje na unavyoongelea Ethanol ujue sio gunia mbili au moja ni mahindi karibu yote na tunayoagiza ndio may be tutaweza na hapo hatujala...utaua watu!
 
Koba,
I like your idea- you are a realist! Watu wetu hawana chakula- hatuwezi kujitosheleza -WFP bado wana prog. kusaidia milo watoto wa shule hawawezi kusoma kwa ajili ya njaa! Brazil hawana taabu ya chakula! Juhudi kwanza ktk kilimo!
Gas Songo2 wazo zuri! Taabu we can not prioritise, tuanze na lipi kwanza as a country- tunatamani kila kitu- at the end tunakuwa hatujafanya kitu! Sasa miaka 40 imeisha wa have done so little!

A: Priorities 1st 10 Years
1. Chakula cha kutosha (Green/Food Revolution)
2. Massive Investment in Education haswa ufundi vijijini
3. Investment in health
4. Ujenzi wa barabara
5. Investment in reliable energy

B: Priorities 2nd 10 years
1: Creation of fund to promote industrialization
2. Promotion of tourism
4. Cut off of external AID unless for humanitarian reasons
3. E.t.c
 
Mzalendo umetoa priorities nzuri sana especially EDUCATION,ENERGY & BARABARA...lakini usisahau RUSHWA ndio sumu ya kila kitu na inabidi wajifunze kukusanya kodi maana nasikia almost 40% inakuwa wasted kwa kutokusanywa kutokana na incompetency ya serikali.
 
..good idea lakini inabidi ufanye homework yako vizuri kabla ya kuja na idea kama hii....anyway Ethanol hatuwezi maana inatumia mahindi/carb na ukweli hata mahindi tuliyonayo hayatoshi kwa ugali wetu sasa unataka tufe njaa na kumbuka still bado tuna import unga,sasa hapo itakuwaje na unavyoongelea Ethanol ujue sio gunia mbili au moja ni mahindi karibu yote na tunayoagiza ndio may be tutaweza na hapo hatujala...utaua watu!
Mkuu watu huja na nadharia nzuri sana kuliko tafiti na uhalisia.
Biashara ya Sungura na mayai ya kwale iliishia wapi?
Kwanini hawaji na teknolojia ya magari yanayotumia maji angali ipo?
Si wazo baya la mtoa mada ila nataraji kajifunza kitu pia
 
Back
Top Bottom