Tatizo la maadili ya Gavana Ndulu na kisa cha Lazaro

Boramaisha

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
820
18
Kisa cha Gavana Ndullu na Lazaro maskini

ban.kijiji.jpg


M. M. Mwanakijiji

KATIKA vichwa vyetu kuna matatizo. Matatizo makubwa kiasi kwamba hatuoni ubaya na makosa ya kukubali ujenzi wa nyumba mbili kwa zaidi ya shilingi bilioni 2.5!

Tuna matatizo kwa sababu ukiwa na wabunge ambao wanatumia muda kuuliza juu ya masuala ya pingu za Muro na wengine kuonyesha kukasirishwa na jinsi polisi walivyoshughulikia suala kiasi cha kukaribia kuwawamba polisi wetu, hakuna mbunge ambaye amejitokeza kukasirishwa na kitendo cha nchi maskini kama ya kwetu kukubali ufujaji wa fedha za umma kama huu wa Benki Kuu (BoT).

Si hivyo tu hata viongozi mbalimbali wa serikali hawaoni ubaya wa kukubali hoja zilizotolewa na Gavana Ndullu mbele ya Kamati ya Bunge kuhalalisha matumizi hayo, viongozi wetu wa dini hawaoni tatizo la kimaadili la jambo hili, wapinzani hawaoni tatizo lake kwani wameridhishwa na maelezo ya “kufuata sheria na mikataba inasema”!

Mniruhusu nifyatuke kidogo; kuna tatizo pale ambapo taifa linalojaribu kujijenga kutumia zaidi ya sh bilioni mbili na nusu kuwajengea watu paradiso yao hapa hapa! Naomba nilionyeshe tatizo hili kwa kutumia mfano mashuhuri wa tajiri na Lazaro katika sehemu fulani ya Biblia.

Tunasimuliwa na Yesu kuhusu mtu mmoja tajiri ambaye tunaambiwa kuwa alikuwa akivaa “nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, ambaye aliishi kwa anasa, kila siku”. Mtu huyo hatutajiwi jina lake, tunamjua kwa hadhi yake na maisha yake ya anasa na vile ambavyo aliweza kuvimudu kutokana na utajiri wake.
Halafu tunaambiwa pia kulikuwa na maskini ambaye “alitamani kujishibisha kwa makombo yaliyoanguka kutoka mezani kwa yule tajiri. Hata mbwa walikuwa wakija na kulamba vidonda vyake.”

Katika simulizi hilo tunaambiwa baada ya kufa hao wawili wakapelekwa kule walikostahili. Tunaambiwa tajiri alipelekwa kwenye moto na Lazaro maskini akapelekwa aliko Baba Ibrahim. Jitihada zote za tajiri kujinasua kule zilishindikana.

Kwa muda mrefu kisa cha tajiri na Lazaro kimetafsiriwa na watu wengi kama simulizi la kutufundisha kuwasaidia maskini. Wanateolojia, wachungaji, mapadre, na wahubiri mbalimbali wametumia simulizi hili kuiasa jamii kujali watu walio maskini na kutumia utajiri wao vizuri.

Japo tafsiri hiyo ina msingi katika simuli kisiasa ninaona tafsiri nyingine mpya ambayo ningependa niihusishe na kashfa ya nyumba za Benki Kuu (za gavana na manaibu wake).

Ninaamini tunaweza kupata mafunzo mawili ambayo naomba niyanyambulishe kidogo. Kwanza, tunafundishwa suala zima la maadili ya mali/utajiri (wealth morality) na pili tunafundishwa suala zima la maadili ya jirani.

Suala la maadili ya mali ni kwamba utajiri unaweza kumfanya mtu amudu vitu vitu anavyovitaka na vile anavyovihitaji (affordability of wants and needs). Ndipo tunasoma kuwa yule tajiri alikuwa “akivaa mavazi ya zambarau, kitani safi na aliishi kwa maisha ya anasa”.


Benki Kuu ni tajiri yule. Ina utajiri wa kutosha kuweza kumudu mahitaji ya gavana wake na manaibu na kuwapa maisha ya anasa. Kwa mujibu wa maelezo ya Benki Kuu juu ya nyumba hizo tunaambiwa kuwa:

“Nyumba zote mbili zilipangwa ziwe za ghorofa moja, vyumba vitano vya kulala, wenyeji na wageni, sebule ya wageni, sebule ya familia, mahali pa kulia na vyoo na mabafu yanayoendana na idadi ya vyumba.

Majengo ya nje ni pamoja na nyumba ya kuishi watumishi, gereji ya magari, bwawa dogo la kuogelea, ukuta na vyombo vya usalama na kibanda cha walinzi. Huduma zilizogharimiwa katika ujenzi wa nyumba hizi ni pamoja na mashine ya umeme (generator), mashine ya kupoza hewa na matenki ya kuhifadhi maji. Wakati huohuo, shughuli zingine zilizofanyika ilikuwa ni kutengeneza mahali pa kuegesha magari pamoja na bustani.” Huo ndugu zangu ni utajiri.

Suala la maadili ya jirani linatueleza juu ya Lazaro. Simulizi linalinganisha kwa namna ya kutisha na kuogopesha hali ya tajiri na mastahili yake na hali ya maskini wetu Lazaro. Kwanza kabisa tunaambiwa Lazaro alikuwa na vidonda mwili mzima. Lakini zaidi cha kusikitisha ni kuwa alikuwa akitamani kula makombo yaliyoanguka toka meza ya tajiri. Huyo maskini alikuwa na maskini, hatuambiwi hata kama alikuwa anavaa nguo maana kama mtu ana njaa kiasi hicho cha kutamani kula makombo unafikiri maisha yake yakoje mtu huyo, utu wake umedhalilishwa, nafsi yake imefanywa duni na yeye anajiona ni mgeni katika nchi yake! Lakini wengi tunakosa kuelewa mgogoro wa kimaadili (moral conflict) ambao unaonyeshwa na kisa hiki. Nifafanue.

Mojawapo ya maneno ambayo wengi wanasoma simulizi hii na kuyaruka yanaanza kwa kusema hivi: “Hapo penye mlango wake (huyo tajiri) aliishi maskini mmoja”. Ndugu zangu kupinga kwangu na kukataa kwangu kabisa hoja za Ndulu na makuwadi wengine wa ufisadi wa benki zenye kuhalalisha matumizi haya ya fedha ni maneno haya.

Kwamba kwenye mlango wa matajiri wetu hawa wanaishi maskini; kwenye miji na vijiji vya taifa letu wanaishi maskini, ukipita yale majengo makubwa na ghorofa kubwa kubwa ndugu zangu wanaishi maskini!!

Tatizo ni nini basi?
Ndugu zangu tatizo lililopo kwenye kisa hiki ni kuwa tajiri hakuona ubaya wowote wa maskini anayeishi kwenye mlango wake (jirani yake) ambaye katika hali yake mbaya yuko tayari kula makombo yanayoanguka mezani kwake.

Tajiri hakuona ubaya wa umaskini wa jirani yake lakini kutokana na utajiri wake aliona anastahili “mavazi ya zambarau, na kitani safi!” Je, hilo si tatizo la ujenzi wa majengo haya ya kifahari ambayo watawala wetu wanasema wanastahili? Je, hili silo ambalo limetokea kwenye manunuzi ya rada, ndege ya rais, ujenzi wa minara miwili ya Benki Kuu n.k?

Hebu angalia
Huko Ukerewe wilaya nzima inahitaji madawati yapatayo 23,000 hivi, kuondoa tatizo la ukosefu wa madawati wilayani humo. Gharama ya kuondoa tatizo hilo ni kama shilingi milioni 713! Yaani karibu nusu ya gharama ya nyumba moja ya gavana! - Watawala tatizo hawalioni!

Huko Monduli wakazi wa Kijiji cha Eng'arooji wametumia shilingi milioni 45 kujenga nyumba mbili za walimu. Kiasi kilichotumika kujenga nyumba za BoT kingeweza kujenga karibu nyumba nyingine 100 za walimu! Tatizo hawalioni!

Hapo Mabibo, Dar es Salaam wametumia shilingi milioni 41 kujenga zahanati ya kata; kwa gharama ya nyumba moja ya gavana au naibu wake zingeweza kujengwa zahanati nyingine 40 kwa gharama ya nyumba zote tatu karibu zahanati nyingine 80 zingejengwa. Hawaoni tatizo la jirani!

Wilaya ya Ilala wameamua kujenga hospitali mpya ya wilaya kwani ile ya Amana yenye uwezo wa kuhudumia watu 200 tu leo hii inahudumia karibu watu 1,000! Gharama ya ujenzi wa hospitali hiyo mpya ni kama shilingi milioni 300. Nyumba moja ya gavana ingeweza kujenga hospitali nyingine nne au kujenga hospitali nyingine kubwa zaidi na ya kisasa zaidi! Hawaoni tatizo!

Naweza kutoa mifano mingine mingi ya kuonyesha nini kinaendelea kwa jirani yetu aliyekaa pale mlangoni katika umaskini wake.

Tatizo la nyumba za gavana si tu kutumika kwa sheria ya manunuzi, si suala la nani anastahili, bali inahusiana moja kwa moja na maadili (ethics) ya utajiri na nafasi ya mtu.

Huko Marekani baada ya hali mbaya ya uchumi kuingia, mwaka jana makampuni karibu makubwa yote yamelazimika kujifunga mikanda. Posho zimepunguzwa, mikutano ya fahari imepunguzwa, walikuwa na ndege za kuhudumia mabosi wao wameuza au wamerudisha walikokodi, yote ni katika kuonyesha kuwa wanawajali wale watu wengine ambao wamepoteza kazi zao na wanaishi maisha magumu.

Wakati Rais Obama ameamua kukutana na wakuu wa makampuni ya magari kutafuta namna ya kuwasaidia wakurugenzi wa makampuni hayo badala ya kutumia madege yao makubwa, iliwapa kuendesha magari yao kutoka Detroit hadi Washington DC! Huko zamani katika utajiri wao walikuwa wanadandia ndege zao za makampuni na kwenda kokote wanakotaka kwa starehe zao!

Lakini sisi Watanzania katika umaskini wetu hatujali tena. Ati tunakubaliana na maneno ya kipuuzi kuwa “mikataba inasema hivi”.

Wamarekani pamoja na kuelewa mikataba inasema nini wamejikuta wanapunguza mambo ya anasa kwa vigogo wao kwa sababu haiwezekani kigogo wa kampuni anaishi kitajiri wakati watumishi wake wananyang'anywa nyumba na hawana uhakika wapi watakula!


Ndiyo maana binafsi naona suala la Gavana Ndulu na wenzake ni mithali tu ya hali yetu kama taifa na jinsi gani tumewadekeza watawala wetu kwa kuamini kuwa kwa vile wako katika nafasi fulani basi wanastahili anasa wakati wananchi wanaishi maisha magumu kila siku.

Endapo tunakubaliana na hoja za Ndulu alizozitoa kwa Kamati na tukazibariki basi tusishangae siku si nyingi wakataka anunuliwe helikopta ya kumharakisha kufika kazini, tusishangae akaomba kikosi cha mabodigadi wa kininja ili kuhakikisha usalama wake, asije akatekwa (utadhani Ballali alivyofanya ufisadi wake alikuwa amefungwa pingu!).

Ni lazima kama taifa tuanze kuwabana hawa viongozi uchwara wanapotumia fedha zetu kuendeleza maisha yao ya anasa kama yule tajiri.

Tusiwaache wakae katika mahekalu yao wamevaa mavazi yao ya zambarau na kitani safi huku mamilioni ya watu wetu wanaishi mlangoni na kutamani angalau waombe maji ya kunywa humo ndani! Chama Cha Mapinduzi kimebariki hili, wabunge wake wamekubali hili (hakuna aliyehoji hadi hivi sasa na kutaka lirekebishwe).

Ati watu wanaona sawa mtu analipwa dola elfu kumi na tano kwa mwezi na posho kibao halafu bado anapewa nyumba ya kufuru, ati kwa vile anastahili! Mwaka huu ni wa uamuzi. Tuna uamuzi wa kuwarudisha wabunge na viongozi hawa hawa wenye kuendeleza falsafa hii ya ukoloni mambo leo!

Tuna uamuzi wa kuendelea kuwashangilia viongozi uchwara wenye kuendeleza utawala wa kifisadi au kuwakataa! Uamuzi ni wetu. Tusije kusubiri kama Lazaro!

Baba wa Taifa Mwalimu Nyeyere alisema kuwa “kabla ya wachache wetu hawajaishi katika anasa, wengi wetu wapate kwanza mahitaji yao muhimu”.

Leo hii Chama Cha Mapinduzi na serikali yake vimeamua kugeuza kinyumenyume falsafa hiyo; leo hii wameamua kuwa “wachache wetu waishi katika anasa, wakati wengi wetu bado wanahangaika kupata mahitaji yao muhimu!” Tusipowakatalia, wataendeleza sera hii potofu mwaka huu.

Binafsi nalaani, napinga, na sioni namna yoyote ya kuhalalisha matumizi ya fedha zetu kuwajengea paradiso gavana na wenzake katika kutekeleza mpango ulioandaliwa chini ya utawala wa kifisadi wa Benki Kuu chini ya Ballali!
 
Hata mimi nampenda sana huyu jamaa.lakini je amekuruhusu utumie Mala yake maana yeye mwenyewe ni mwenzetu humu jamvini na huamua atoe nini na aache nini.
 
Imagine Mzee Mwanakijiji ama mwananchi yeyote yule mwenye uchungu na maskini Watanzania akasimama kwenye majukwaa na kuanza hotuba yake kwa kusema "Ndugu zanguni ......" na kubwabwaja yote aliyoyaandika Mwanakijiji. Wananchi wengi mno watapata msisimko na kuvutiwa na hotuba kama hii. Tunahitaji good orators watakaoweza kukonga nyoyo za wananchi kama anavyofanya Mwanakijiji kwa maandishi. It is a challenge indeed.
 
Hata mimi nampenda sana huyu jamaa.lakini je amekuruhusu utumie Mala yake maana yeye mwenyewe ni mwenzetu humu jamvini na huamua atoe nini na aache nini.

Sorry, I always get excited and carried away! Mzee atanisamehe kwa dhambi hii I am sure.
 
Hivi kuna mtu anaweza kunipa sababu kwa nini Tanzania na nchi tunaojiita sisi maskini, mishahara ya viongozi wetu na marupurupu yao huzidi yale ya viongozi wa nchi tajiri duniani?..
 
Hivi kuna mtu anaweza kunipa sababu kwa nini Tanzania na nchi tunaojiita sisi maskini, mishahara ya viongozi wetu na marupurupu yao huzidi yale ya viongozi wa nchi tajiri duniani?..
Kwasababu kwa nchi zetu siasa ni ajira na kwanza ni ajira ya hali ya juu sana. Watu wanakimbilia kwenye siasa muda wa jioni na wanataka ku-capitalize kabla hakujawa giza. Wanaokwenda kwenye siasa ni wachache sana ambao wapo pale kwa ajili ya Watanzania au wapiga kura wao. Lakini wengi wanakwenda kwa maslahi yao binafsi na hasa ya kipato. Wengine pia wako humo ili kuwa na influence na mawaziri ili waweze kuendesha biashara zao kwa upendeleo kama vile upendeleo wa kutumia bandari na pia kujua nini kinachjiri katika bajeti ili afaidike na mabadiliko yoyote yanayotokana na budget au sheria au kanuni fulani fulani zinazotungwa kwa influence yao.
 
hivi kuna mtu anaweza kunipa sababu kwa nini tanzania na nchi tunaojiita sisi maskini, mishahara ya viongozi wetu na marupurupu yao huzidi yale ya viongozi wa nchi tajiri duniani?..

ubinafsi uliovuka mipaka na kutokuzipenda kwa dhati nchi zao na watu wake.
 
Kama wanavyosema washashi, that right there is some Ennio Morricone composition. "The Ecstacy of Gold" style.

Tatizo la kwanza, wanaojua hawajali, kwani wananufaika na mfumo uliopo na hawana morals za kushtushwa na hili.

Tatizo la pili, wanaojua na kujali ni wachache na hawana influence ya kutosha kuleta mabadiliko.

Tatizo la tatu, wanaojua, kujali na kuwa na influence ya kutosha kuleta mabadiliko wako negligible, outnumbered and despirited.

Tatizo la nne, majority ya wanaotakiwa kutiwa uchungu na hizi habari hawazijui vya kutosha.
 
Gharama ambayo wengine tunalipa (as I found out today) ni kubwa mno kuliko. Ni gharama inayoendana na machozi. Lakini lazima katika wawepo watu ambao wataweza kumuambia mfalme kwamba yuko Uchi. It is not popular, it is offensive, it is combative and what have you.. but somebody got to do it.

Tatizo ni kama hilo analosema Kiranga..na JK mwenyewe amewahi kulizungumzia ni wale asilimia 70 ambao wapo wapo tu.
 
Hivi kuna mtu anaweza kunipa sababu kwa nini Tanzania na nchi tunaojiita sisi maskini, mishahara ya viongozi wetu na marupurupu yao huzidi yale ya viongozi wa nchi tajiri duniani?..
Mkandara, Tanzania inaelezewa kuwa ni nchi masikini, Uswisi ni nchi tajiri.
Kufuatia umasikini wa Tanzania, matajiri na watu wa Uswiss wakaamua kukusanya michango ya huko kuwasaidia Watanzania kupitia shirika fulani la misaada.

Matajiri hao, wakatuma tiketi kwa masikini 10 wanaosaidiwa na Waswisi hao, kwenda ziara ya mwezi mmoja Uswisi kuishi kwa matajiri. Masikini hao kumi wakachaguliwa nami nikabahatika kuwa miongoni mwao.

Tukafika huko Uswisi na kuona maisha ya matajiri hao, kusema ukweli ni basic. Matajiri Uswisi wanaendesha baiskeli kwenda kazini, wanatumia public transport, wanakula natural foods, organic etc. Kwa vile walijua sisi ni masikini, basi si misaada hiyo kila tuendapo.

Ilipofika zamu ya Waswiss hao kutembelea Tanzania, tuliwapeleka pale Jumba la Makumbusho, Opp. IFM. Siku hiyo ilikuwa siku ya semina fulani ya wabunge wote pale Karimjee, wazungu wakashaangaa kuona yale ma VX mengi ya ajabu!. Wakauliza wakajibiwa ndio magari ya Wabunge wetu.
Tangu pale, wafadhili wetu wakaamini kumbe Tanzania sio masikini ki hivyo.

Jamaa akasema sisi ni matajiri, ila mbunge wa Uswisi, hawezi kuown 4x4 kubwa hizo. Wakasema tulifikiri tunaisaidia nchi masikini, kama umasikini wenyewe ni huo walioushuhudia, waliporudi, walireview misaada yao kwa Tanzania.

Hivyo naungana na wewe Tanzania sio masikini, ila watu wake ndio masikini wengi na matajiri wachache.
 
ubinafsi uliovuka mipaka na kutokuzipenda kwa dhati nchi zao na watu wake.


Ubinafsi mwingine unatia haya jamani! hivi kiongozi mf. huyo gavana, hawezi ku-protest akijengewa au kununuliwa gari, nyumba, fenicha za gharama iliyokufuru!!
 
Gharama ambayo wengine tunalipa (as I found out today) ni kubwa mno kuliko. Ni gharama inayoendana na machozi. Lakini lazima katika wawepo watu ambao wataweza kumuambia mfalme kwamba yuko Uchi. It is not popular, it is offensive, it is combative and what have you.. but somebody got to do it.

Tatizo ni kama hilo analosema Kiranga..na JK mwenyewe amewahi kulizungumzia ni wale asilimia 70 ambao wapo wapo tu.

MM Gavana si anateuliwa na Rais? Sasa umefikiri nini kama mkulu mwenyewe amekaa kimya.
 
Hakuna uzalendo wala nini we jiulize wanawake wangapi huko Kabanga na Bunazi wanafariki kwa kukosa matibabu, halafu hawa jamaa wanakarabati nyumba kwa mabilioni. Nikuwanyonga tu ndo dawa halafu jamaa wanamsifu gavana nduru ijui kwa yapi kama thamani ya shilingi ndo inazidi kushuka tu. Huyu nae ni mburura tu.

Me nadhani nae ANYONGWE tu. Ndo maana wachina wanendelea ingawa kwao masikini wapo pia. Kigogo akileta wizi ananyongwa hadharani. Kagame naye kawa shikilia kule kwake ni kujiuzuru tu. Hapa kwetu ni kulindana tu, akifanya kosa anaamishwa wizara ili akaharibu kwingine, kelele zikizidi anapewa ubalozi akapumue nje. Huyu wa kwetu zake ni kucheka na kutabasamu tu. Mzee.. acha kuuza meno fanya kazi!

Hali ikiendelea hivi bongo mi nasali novena kwa siku nane kumwomba Mungu atuletee dictator ili awapindue hawa jamaa. Shwaini. Kazi ipo!
 
Hakuna uzalendo wala nini we jiulize wanawake wangapi huko Kabanga na Bunazi wanafariki kwa kukosa matibabu, halafu hawa jamaa wanakarabati nyumba kwa mabilioni. Nikuwanyonga tu ndo dawa halafu jamaa wanamsifu gavana nduru ijui kwa yapi kama thamani ya shilingi ndo inazidi kushuka tu. Huyu nae ni mburura tu.

Me nadhani nae ANYONGWE tu. Ndo maana wachina wanendelea ingawa kwao masikini wapo pia. Kigogo akileta wizi ananyongwa hadharani. Kagame naye kawa shikilia kule kwake ni kujiuzuru tu. Hapa kwetu ni kulindana tu, akifanya kosa anaamishwa wizara ili akaharibu kwingine, kelele zikizidi anapewa ubalozi akapumue nje. Huyu wa kwetu zake ni kucheka na kutabasamu tu. Mzee.. acha kuuza meno fanya kazi!

Hali ikiendelea hivi bongo mi nasali novena kwa siku nane kumwomba Mungu atuletee dictator ili awapindue hawa jamaa. Shwaini. Kazi ipo!

Nafasi ya kumpata huyo Dicteta tutaipata iwapo tutachangua mtu mwingine awe Rais. Hebu niambie Kikwete ambaye amemchagua huyo Ndullu amekaa kimya halafu eti anataka Kipindi cha pili. Atatufanyia nini? Kama si kuongeza wafujaji wa mali tena.
 
akiharibu mtu tusisubiri hadi rais aseme; wakati mwingine we have to pressure the individual to act.

Hivi katika viongozi wetu kuna hata moja ameshajiuliza kwanini "mimi (boss) nina mshahara mkubwa na marupurupu mengi" kupita wafanyakazi wengine na hata uwezo wa kampuni yenyewe?

Je ni uwezo wake au? perfomance yake? au basi tu kwakuwa ana nafasi bahati yake..

Do we really do reflections? do we reflect the realities around us?
 
Back
Top Bottom