Tatizo la Lipumba ni kuitwa Ibrahimu au Abrahamu?

mkigoma

JF-Expert Member
Jul 26, 2011
1,180
309
Watanzani hatujapata kuwahi kupata mgombea wa Urais mwenye sifa nzuri na asiye na kashfa mtu muadilifu kitaifa na kimataifa tangu uanze mfumo wa vyama vingi zaidi ya Prof Ibrahim Lipumba lakini kwa mtu imekuwa vigumu kukubalika ndani ya nchi yake tofauti na nje, Je tatizo ni uelewa mdogo wa wapiga kura? au ni Jina lake la Ibrahimu?
 
Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
13,631
23,368
We Mkigoma si ni kada wa CCM? Sasa swali lako tutakujibu nn wakati wewe mwenyewe kura yako unampa JK? Ungekuwa unampa Lipumba labda leo hii angekuwa Rais wa JMT
 
TUKUTUKU

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
11,769
4,030
Watanzani hatujapata kuwahi kupata mgombea wa Urais mwenye sifa nzuri na asiye na kashfa mtu muadilifu kitaifa na kimataifa tangu uanze mfumo wa vyama vingi zaidi ya Prof Ibrahim Lipumba lakini kwa mtu imekuwa vigumu kukubalika ndani ya nchi yake tofauti na nje, Je tatizo ni uelewa mdogo wa wapiga kura? au ni Jina lake la Ibrahimu?

Wewe nadhani hujui historia vizuri ya LIPUMBA,kulingana na nyuzi uliyoitoa unaonekana unasumbuliwa na udini.Kwa kifupi huyu jamaa ni mzaliwa wa mabama huko urambo Tabora,huyu jamaa amekaa nje ya nchi kwa muda mrefu,kwa bahati mbaya aliathiriwa sana na mila na desturi za kizungu na alipokuwa anarudi kwao hata wazazi wake walikuwa wanamshangaa sana kwa jinsi alivyokuwa alionekana mtu wa majivuno.Matokeo yake alianza kupoteza mvuto katika jamii ya kabila la kinyamwezi na hivyo kumfanya asikubalike kabisa alipoamua kuwa mwanasiasa.Mfano mzuri ni matokeo ya uraisi ya 1995 katika eneo alilozaliwa alikuwa mshindi wa tatu kitu ambacho ni cha ajabu kwani wagombea wenzake walifanikiwa kuongoza katika maeneo waliozaliwa mfano Mrema kule kilimanjaro aliongoza,Mkapa kule Mtwara aliongoza.
"Charity begins at home"ndiyo kitu kikubwa kinanchomwangusha huyu jamaa!kibaya zaidi huyu jamaa hana mizizi ya kisiasa kama wenzake,kwani hajawahi kugombea udiwani wala ubunge,ukilinganisha na wagombea wengine kama Dr Slaa,Kikwete,Mkapa,na Mrema.Jamii haimnyimi kura kwa sababu ni muislamu,bali hana mvuto na mizizi ya kisiasa katika jamii ya kinyamezi na nchi kwa ujumla.
 
SEAL Team 6

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
655
118
Leo hii CUF ni CCM B tunasubiri kuona mchakato wa Uraisi ndani ya CCM Lipumba kushirikishwa katika vikao.
 
Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,623
4,278
Seif Shariff Hamadi kamtoa kafara huyu jamaa! nyie subirini uchaguzi utakao kuja 2015 kama kwenye historia ya vyama vingi atakuwepo huku bara! atakua ameshasahaulika, jamaa yake sasa hivi anakula bata kwa mrija.
 
Arafat

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
2,582
755
Watanzani hatujapata kuwahi kupata mgombea wa Urais mwenye sifa nzuri na asiye na kashfa mtu muadilifu kitaifa na kimataifa tangu uanze mfumo wa vyama vingi zaidi ya Prof Ibrahim Lipumba lakini kwa mtu imekuwa vigumu kukubalika ndani ya nchi yake tofauti na nje, Je tatizo ni uelewa mdogo wa wapiga kura? au ni Jina lake la Ibrahimu?

Tatizo ni Unafki wake yeye mwenyewe binafsi na chama chake cha CUF
 
Arafat

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
2,582
755
Seif Shariff Hamadi kamtoa kafara huyu jamaa! nyie subirini uchaguzi utakao kuja 2015 kama kwenye historia ya vyama vingi atakuwepo huku bara! atakua ameshasahaulika, jamaa yake sasa hivi anakula bata kwa mrija.

Na whisky mkuu Nape alitupa taarifa
 
buyegiboseba

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
535
145
Prof Lipumba hana traits za Siasa ypo ki analylist zaidi(wa uchumi) anaweza kuchambua vizuri matatizo ya kiuchumi tuliyonayo lakini hana uwezo wa kisiasa wa kuyaadress fuatilia speech zake utagundua nisemacho hapa,Huyu prof angefaa sana kuwa kwenye jopo la tume ya mipango ya nchi angeng'ara sana, siasa haiwezi analeta uchumi katika kila kitu,Igunga katumia punda akidhani anaikonomize, wenzie walitumia chopa na mashangini,siasa ni kipaji vile vile sio usomi tu.
namuomba JK kwa vile tayari wana ndoa na CUF amtumie huyu prof kwa ushauri huenda mchango wake ukatufaa kabla nae hajawa off record.
 
Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,537
1,303
Pamoja na ukweli ya kwamba Lipumba ni mgombea BORA ambae siku zote huwa hapati kura za kutosha, sababu kuu ni kwamba tangu mwanzo cuf ilikuwa inajulikana kuwa chama cha kidini kitu ambacho kilichangiwa sanaaa na wafuasi wake hasa kwenye mikutano ya hadhara kutokana na mavazi tu wa wafuasi wa cuf ni hii ikawa ndio msumari kwa hiki chama vinginevyo LIMUMBA anstahili haki yake, si tu kwa uwezo hata elimu yake, pili ajaribu sasa kwenda ili mikoa ya bara hasa kanda ya kaskazini na kanda ya kati KWANI cuf iNAONEKANA ni kama dawa ya MALARIA VILE
 
Tata

JF-Expert Member
Dec 3, 2009
5,800
2,712
Watanzani hatujapata kuwahi kupata mgombea wa Urais mwenye sifa nzuri na asiye na kashfa mtu muadilifu kitaifa na kimataifa tangu uanze mfumo wa vyama vingi zaidi ya Prof Ibrahim Lipumba lakini kwa mtu imekuwa vigumu kukubalika ndani ya nchi yake tofauti na nje, Je tatizo ni uelewa mdogo wa wapiga kura? au ni Jina lake la Ibrahimu?

Tunampa Profesa Ibrahimu Lipumba changamoto ya kwenda kugombea ubunge kwao Urambo kwanza ili aanze kupata uzoefu wa kushinda uchaguzi.
 
Felixonfellix

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
1,672
180
akuabli kwenda tu akafundishe uchumi katika chuo chochote hapa tz
anaweza kwenda na Muslim pale Morogoro
nasema hiyvo kwa sababu thread imekaa kidini zaidi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom