Msaada: Nina tatizo la kuwashwa ndani ya Uume

Northern empire

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
358
459
Habari ndugu zangu.

Niende moja kwa moja kwenye mada Mimi ni kijana Wa miaka 29 nina tatizo LA kuwashwa kwa ndani ya uume hasa ninapokojoa huku uume ukiwa umesimama baada ya kumaliza kukojoa Mara nyingi huwa naanza kuhisi nawashwa kwa ndani kwenye njia ya mkojo.

Tatizo hili lilianza takriban miaka kumi iliyopita ila kwakuwa huwa lilikuwa linatokea mara moja moja mfano kwa mwezi linaweza kutokea Mara moja nikawa silichukulii maanani. Na likitokea huwa nawashwa kwa muda kama dakika ishirini mpaka arobaini kisha linaisha lenyewe.

Sasa naomba msaada kwani huwa likija linaninyima furaha kwani huwa nahisi mkojo unataka kutoka alafu nikienda kukojoa unatoka mdogo kisha nahisi kuwashwa na baaada ya muda mfupi nahic unataka kutoka tenaa. Yaani mpaka nichukue muda walau Wa SAA ndio hutulia.

Ndugu zangu mwenye ushauri au dawa aniambie huenda ikanisaidiaa
 
Mkuu nenda hospitali kapime UTI na pendelea kunywa maji mengi na maji ya madafu ,maji ya miwa kusafisha kibofu cha mkojo. Utakuwa unayo maradhi yanayo tokana katika njia ya mkojo. Kapime hospitali kisha uje hapa utupe majibu umeambiajwe huko hospitali?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom