Tatizo la kuwashwa mwili mara kwa mara- Fahamu chanzo, pata ushauri na tiba ya tatizo hili

Mkuu tupo wengi wa namna hii nami nimerumia si tu sabuni hata dawa nimemeza bila mafanikio. Hali huwa inakuwa mbaya zaidi hasa wakati wa mvua kama kipindi hiki au kwenda kwenye sehemu zenye ubaridi kama mbeya rushoto arusha na kagera.
 
Mimi kuna mama alinipa dawa ya kienyeji nikanywa lakini hakunionyesha mti. alimambia hadi nmpe hela. niliondoka sijapata hela. yule mama alikuwa anaitwa mama bahati. ntarudi kumtafuta kule kyaruyonga. Mkuu utazunguka hospital zote hautapata dawa. yaani mimi nilisaidiwa hadi na ndugu na jamaa. mara watu waniambie minyoo,areji mara waseme amoeba. ilikuwa inanisumbua sana hasa asubuhi. mtu unajikuna huku unasikia utamu kwa mbali. nilikaa miaka 4 bila kupona but toka 2000 hadi leo sijaugua tena.
 
hizo ni allergy,kuna wengine wana allergy ya sperm,bila condom ni vidonda chini zikiwamwagikia ndani ya k.kuna wengine wana allergy ya machozi,yakitoka ni vidonda.kuna wengine wana allergy ya maji,wakioga wana washwa.tiba yake kwa kweli siijui,maybe sidano za kila siku
 
Dawa za minyoo nilishameza sana bila mafanikio. Nikiwa Dar nikioga maji moto kidogo haisumbui lakini huku Arusha ni balaa. Natamani hata nisioge.

sio minyoo wala nini. huko arusha watafute wamasai watakupa dawa hakika utapona. hamna dawa ya kutibu huo ugonjwa hospital za bongo hamna dawa. niamini mimi. mimi nlisota nao we acha tu. dawa niliyopewa ya kunywa nilikukunywa kwa wiki moja lita5 za dawa. hadi leo. siku ukienda bukoba nipm nikuelekeze kwa mama bahati akupe dw
 
Tatizo hili lilinisumbua sana miaka ya 1986 nikiwa mashuleni boarding. Sikutumia dawa yoyote hali ya alergy hiyo ya maji hasa ya baridi ilikwisha yenyewe baadaye sana lakini. Wakati mwingine wataalam wa tiba hushauri kutumia dawa fulani za kundi la antihistamine ambazo zamani za chroloquin zilikuwa zinatumika kuzuia kuwashwa na tiba ya chloroquine. Antihistamine zingine huleta usingizi na zingine kama vile bromodiphenhydramine na dexchlorpheniramine hazisababishi usingizi kabisa.
 
Hii inaitwa acquagenic uticaria, naomba Google afu atapata maelezo mazuri. Lakini mara nyingi no specific matibabu, kikubwa unatakiwa upunguze exposure kwa majimaji kwa muda mrefu.

Kuoga tumia short time na tumia cotton towel and cotton cloths hata mashuka ya kutandika. Pale inapozidi meza antihistamine mfano cetirizin tabs 10mg od 5/7. Ila Google hiyo itakusaidia kupata maelezo mazuri.

All the best
 
Nilikuwa na tatizo hilo, na sasa limepungua kwa kiasi kikubwa sana bila kutumia dawa yoyote. Nilishauriwa kuacha kula vyakula vyenye mafuta mengi sana (fat) hasa nyama. Nikaambiwa kuwa ikiwa ninataka kula nyama ikiwezekana basi niwe naibanika kwanza na nitoe mafuta mafuta yote. NIlipunguza sana ulaji wa nyama na ile hali ikawa inapungua sana. Na sasa imepungua kwa kiwango kikubwa sana maybe 98%.

Ningekushauri ujaribu hiyo, inawezekana ngozi yake ina mafuta mengi sana kama nilivyokuwa mimi. Na pia kama ni home tumia mafuta ya kupikia yanayotokana na mbegu/mimea kama pamba au alizeti....haya machafu ya nyama kama korie achana nayo.
 
Pole mkuu. Fuatilia zaidi hizo dawa za asili ndio zina uhakika wa kukusaidia kwa kweli. Nami nina tatizo linalofanana na lako kidogo, huwa nawashwa sana miguuni na mapajani, hasa baada ya kutembea kwa muda mrefu na kuvaa nguo zinazobana kama skin tight etc.
 
Habari wana jamvi...jamani naomba kujua kama kuna dawa inayoweza kutuliza ama kuponyesha mwili kuwashwa....mdogo wangu anawashwa mwili mzima na anajikuna sana hasa sehemu za paja
 
Wakati mwingine huwa ni allergy (mzio) wa vitu kama sabuni anayoogea, mafuta ya kupaka au body spray. Jaribu kubadirisha sabuni au mafuta yakupaka au body spray anayotumia. Sina utaalam zaidi na hili ila haya machache nayafahamu na yamewahi kumtokea mtu wangu wa karibu.
 
Mara nyingine mtuu anawashwa mwili kwa sababu ya minyoo nenda duka la dawa leo ununue dawa ya minyoo dozi 1 ambayo utaitumia kesho asubuhi kabla ya kula kitu chochote watanzania wengi hawana tabia ya kula dawa za minyoo
 
dah mambo ya dawa tena kabla hujajua tatizo nini ndio shida...anyway ngoja ntambadirishia mafuta na sabuni nione inakuwaje
 
Salaam wanabodi.

Nimekuwa nasumbuliwa na tatizo la kuwashwa mwili mara kwa mara nilikwenda hospital wakapima mkojo na damu hawakuona kitu,

Tatizo hilo limenianza muda mrefu kama miaka mitano iliyopita lakini mpaka leo sijapata tiba.mwili unawasha wote kwa vipindi tofauti tofauti hata nikijikuna haisaidii mpaka upoe wenyewe.Je tatizo ni nini na tiba ni ipi? Msaada tafadhali!
 
Back
Top Bottom