Tatizo la kuwashwa mwili mara kwa mara- Fahamu chanzo, pata ushauri na tiba ya tatizo hili

hata mimi wakuu, nawashwa mwili mzima km mtu aliemwagiwa upupu, sasa nimejikuta kila baada ya siku3 nakunywa kidonge kimoja cha centrizene (kidonge cha aleji), nikishakunywa tu nakaa hizo siku bila kuwashwa, sasa imekuwa ni tabia ya kunywa dawa ili nisiwashwe, nahofia sumu itazidi kujaa mwilini maana miaka 2 sasa nakunywa dawa tu.
kaka nimetumia cetrizine miaka tisa since 2002 june na matumizi kama wewe kila bada ya siku tatu au nne hospitali zote nilikwenda hapa town lakini no solution. Mwaka huu mwezi wa nne nikitia timu SAMUNGE nikapiga kikombe cha babu since then sijaona muwasho wala mkuno na miezi miwili sasa sijagusa cetrizine!
 
kama bado hujapata ufumbuzi wa tatizo lako, tuwasiliane mimi nitakupatia natural remedies from Forever living products.
please advice kama bado unahitaji
 
kaka nimetumia cetrizine miaka tisa since 2002 june na matumizi km wewe kila bada ya siku tatu au nne hospitali zooote nilikwenda hapa town lkn no solution. Mwaka huu mwezi wa nne nikitia timu SAMUNGE nikapiga kikombe cha babu since then sijaona muwasho wala mkuno na miezi miwili sasa sijagusa cetrizine!

yaani huwezi amini jinsi nilivyokuwa nampinga babu, but for this, i have to go, lazima nifike samunge, ila nikishapata kidonge sitatoa udenda km mzee wa kiraracha kweli? natania tu, mkuu lazima niende loliondo.
 
Una allergy mkuu kama sio maji au mafuta unayotumia!
mkuu hii tatizo lilianza gafla tena kupitia mwanangu yy ndio alianza ikaamia kwangu dr akasema ni minyoo nimempa dawa za minyoo na kupima choo na damu akuna k2 na mm imenianza nimekunywa dawa za minyoo ola mafuta ninayotumia ni location nivea for over 10yrs cjabadilishaga maji nimechimba kisima changu sipo sure sana
 
hata mimi wakuu, nawashwa mwili mzima km mtu aliemwagiwa upupu, sasa nimejikuta kila baada ya siku3 nakunywa kidonge kimoja cha centrizene (kidonge cha aleji), nikishakunywa tu nakaa hizo siku bila kuwashwa, sasa imekuwa ni tabia ya kunywa dawa ili nisiwashwe, nahofia sumu itazidi kujaa mwilini maana miaka 2 sasa nakunywa dawa tu.

nimemeza ivyo vdonge lakini akuna nafuu yoyote ile mpaka creme ya kupaka akuna k2
 
Naombeni ushauri wenu madaktari wa jukwaa hili,

Mimi nawashwa sana na mwili kila baada ya kuoga,yaani dakika tano baada ya kuoga huwaga ni za shida sana kwangu.

Nakumbuka nilipata tatizo hili kwa mara ya kwanza 2001 wakati huo kijijini alinitambaa mdudu yule anaitwa slug anatembea kama Kono kono ila hana shell.

Nilitoka lenge lenge kama nimeungua moto na mwili uliwasha sana yaani sana nilikimbia straight hospitali na nilipewa dawa pale pale baada ya muda kidogo nilitulia.

Nikapewa dozi nikatumia,ilipita muda kidogo tatizo lilirudi tena sasa ni kila baada ya kuoga.

Nilirudi hospitali nikaambiwa ni fungus sugu na minyoo nikala dawa lakini wapi!

Nikarudi tena Hapa Dar nikapewa tiba ile ile lakini wapi.

Siamini kama haitibiki hii kitu.

Msaada wenu wanajukwaa hili la JF Doctor ni wa muhimu.

Natanguliza shukrani zangu.

=================
Matatizo Mengine
=================

Jamani naombeni msaada,

Nina tatizo la kuwashwa mwilini alafu nikijikuna hiyo sehemu inavimba lakini baada ya dakika kadhaa panarudi panakuwa sawa na muda mwingine hadi kichwani napakuna sana huku muwasho ukihama hama kadiri ninapojikuna.

Nilishawahi kwenda hospitali fulani wakanipima wakasema nina allergy ya nyama ng'ombe na mayai wakanipa dozi ya mwezi mzima huku wakinishauri niache vitu hivyo kabisa! nimefanya hivyo lakini tatizo lipo palepale.

Wadau naombeni msaada wenu.

Itakua ni dryness. Jaribu kuoga na shower gel yenye moisturizer au kupaka mafuta ya dry skin.
Sababu lingine maybe maji tu yenyewe. cheki tatizo lilianza lini, kama ulihama au kusafiri hivi karibuni jaribu ku-link.
Kula samaki nyingi kuliko nyama (kama 150 to 250g 2 or 3 times a week) inasaidia kupunguza dryness.
Kama kuwasha kunaendelea pata ushahuri wa daktari (maana hapa sio hospitali, tunashahuriana tu kutokana na experiences)
 
Wana JF. Binafsi nnatatizo la luwashwa mili mzima pindi nnapo toka kuoga.

Mara nyingi hunitokea nikioga maji ya baridi, lakini pia sometime hunitokea hata kwa hot water, sijajua tatizo nini ila nshaenda hosp nikapewa dawa lakini hali hajabadilika had sasa. Msaada tafadhali.
 
wana jf. Binafsi nnatatizo la luwashwa mili mzima pindi nnapo toka kuoga. Mara nyingi hunitokea nikioga maji ya baridi, lakini pia sometime hunitokea hata kwa hot water, sijajua tatizo nini ila nshaenda hosp nikapewa dawa lakini hali hajabadilika had sasa. Msaada tafadhali.
Duh! Mkuu tatizo ka langu aisee! Ila me uwa nafanya ka napasha miguu moto inapungua kidogo! Acha wataalamu wamwage maushauri hapa
 
Poleni sana waungwana!
siku moja nilisikikiza kipindi cha afya radio moja walikuwa wakizungumza juu ya tatizo la kuwachwa mara tu mtu unapotoka kuoga:-

Sababu
Ni allegy inayosababishwa na bacteria ambao aidha wanakuwemo kwenye maji au kwenye kifaa kinachotewa maji hasa magudulia yenye mfuniko mdogo ambayo hutunza uchafu ambao ambao husababisha fungus ambao mwisho wa siku ndio huleta mwasho mwilini. Pia huweza kutokea kwenye mabomba kutokana na mifumo mingi ya maji kutokuwa salama mfano mabomba ya maji safi kupasuka sehemu ambayo ni makutano na bomba la maji taka etc!

Tiba:
Hiyo ni allegy ivo unashauriwa kutumia anti-allegy lakini pia unaweza tumia shower gel ambayo hutengeneza layer laini inayokuwa ni kinga kwako wakati wa kuoga!

Naomba kuwasilisha, mtaniwia radhi hzo ni point chache ambazo nilizidaka siku hiyo sina utalaam wowote wa kiafya kwa hiyo sitegemei swali la kitaluma! Asanteni.
 
Poleni sana waungwana!
siku moja nilisikikiza kipindi cha afya radio moja walikuwa wakizungumza juu ya tatizo la kuwachwa mara tu mtu unapotoka kuoga:-
Sababu
Ni allegy inayosababishwa na bacteria ambao aidha wanakuwemo kwenye maji au kwenye kifaa kinachotewa maji hasa magudulia yenye mfuniko mdogo ambayo hutunza uchafu ambao ambao husababisha fungus ambao mwisho wa siku ndio huleta mwasho mwilini. Pia huweza kutokea kwenye mabomba kutokana na mifumo mingi ya maji kutokuwa salama mfano mabomba ya maji safi kupasuka sehemu ambayo ni makutano na bomba la maji taka etc!

Tiba:
Hiyo ni allegy ivo unashauriwa kutumia anti-allegy lakini pia unaweza tumia shower gel ambayo hutengeneza layer laini inayokuwa ni kinga kwako wakati wa kuoga!

Naomba kuwasilisha, mtaniwia radhi hzo ni point chache ambazo nilizidaka siku hiyo sina utalaam wowote wa kiafya kwa hiyo sitegemei swali la kitaluma! Asanteni.[/QUOTE mkuu hayo yote nshafanya, kununua vyombo vipya,kunywa anti alege ,nimeshindwa tu kuogea maji ya uhai na kilimanjaro. Tatizo liko palepale.
 
Pia kama unatumia hizi sabuni za dukani za kuogea kama Lux, na nyinginezo nyingi, hizi huwa zina mchanganyiko wa kemikali za aina nyingi ambapo huenda ukawa na allergy na mojawapo, hivyo basi acha kuogea hizi sabuni na tumia sabuni zenye natural products, kama vile zile za mwarobaini nk, zinapatika maduka ya vyakula asilia.
 
Jaribu kubadili sabuni. Jaribu dettol Origal Tshs 2,500/= hadi 3000/= Supermarket. Achana na sabuni za kutandazwa Manzese,buguruni etc halaf wanauza pieces 3 buku. May be this can work.
 
Nina tatizo linalonisumbua kwa muda mrefu na kuninyima raha kabisa. Kila nikimaliza kuoga, mwili wote unawasha sana kwa dakika kati ya 10 na 20. Na nikijikuna mwili unavimba, yaani sehemu ninayojikuna inavimba. Nimetumia karibu kila aina ya sabuni, nimetumia maji ya moto na ya baridi bila mafanikio. Mbaya zaidi nikitumia wash cloth. Nataabika, kila nikitaka kuoga mpaka nijishauri mara mbili mbili. Naombeni msaada kwa mwenye uelewa na hili.
 
Mkuu una minyoo, pole sana.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom