Tatizo la kuwashwa mwili mara kwa mara- Fahamu chanzo, pata ushauri na tiba ya tatizo hili

Chimunguru

JF-Expert Member
May 3, 2009
10,680
4,345
1592222296794.png


Habari JF Doctor na wana jamii wote.

Mdogo wangu wa kiume (23yrs) ana tatizo la kuwashwa mwili mzima tokea mwaka 2002. Nimezunguka naye takribani hospitali zote kubwa hapa Dar lakini hatujafanikiwa kupata ufumbuzi wa tatizo lake.

Kwa ufupi ni kwamba alianza tu kuwashwa jichoni, macho yakavimba, akaenda hospital (Burhani) akapatiwa dawa za kutuliza allergy (cetrizine) ile hali ikatulia kwa siku mbili tu, ya tatu mwasho ukarudi tena.

Tukaenda Aga Khan akapimwa kuanzia choo, mkojo, damu lakini hakukutwa na minyoo, wala gonjwa lolote la zinaa akapewa tena cetrizine na ndizo anaendelea nazo mpaka leo kutumia, miaka nane sasa ule mwasho bado upo.

Akijikuna pale panapowasha panavimba mithili ya mdudu amekukojolea au mithili ya mtu aliyewashwa na washawasha, na ni mwili mzima unakuwa unawasha, mpaka anywe cetrizine ndo muwasho unatulia, hii dawa hutuliza kwa km siku nne tu baada ya hapo muwasho pale pale. Alishameza dozi za fungus kama mara nne hivi kwa siku kumi na tano lkn tatizo bado lipo pale pale.

Hofu yangu ni kuwa hizi cetrizine zinaweza zikamletea madhara in a long run. Sasa daktari saidia hapo yawezekana ni nini sababu ya huu ugonjwa?

WADAU WENGINE WENYE TATIZO HILI:

Tatizo la mwasho wa ngozi na matibabu
KUJIKUNA ngozi sio jambo la kawaida jinsi baadhi ya watu wanavyodhani.
Ukikumbwa na hali hii, nenda ukamuone daktari kwa sababu inaweza kuwa dalili ya tatizo kubwa la kiafya.
Wataalamu wanaonya kuwa kuwasha kwa ngozi ya mwili kunakopelekea mtu kujikuna hakufai kupuuzwa.

“Miongoni mwa matatizo ya kiafya ambayo yanasumbua watu wengi duniani na kuwanyima raha ya maisha, ni ngozi kuwasha. Kwa baadhi ya watu, hili linaweza kuwa tatizo sugu. Ingawa ni la kiafya, baadhi ya watu hulihusisha na imani potofu kwa kukosa habari sahihi,” asema mtaalamu wa maradhi ya ngozi, Dkt Epha Swaka.

Anasema kwamba kuna sababu nyingi zinazochochea tatizo hili na baadhi zina madhara makubwa na hata kuhatarisha maisha.

Udhaifu wa kinga
Miongoni mwa sababu za kutokea kwa mwasho wa ngozi baada ya kuoga ni za kimazingira na baadhi zinahusiana na hitilafu katika mfumo wa kinga ya mwili wa mhusika. Huwa ni moja ya dalili za mwanzo za Ukimwi.

“Tatizo hili linaweza kuwa ni dalili za magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza kama vile matatizo ya figo, ini, tezi shingo, matatizo ya mfumo wa damu, kisukari, saratani na msongo wa mawazo,” aeleza Dkt Swaka.

Mazingira machafu
Tafiti zimebainisha kuwa sababu nyingine ni uchafuzi wa mazingira, kemikali zenye sumu zinazopatikana katika moshi wa tumbaku, mifuko ya plastiki, dawa za kufanyia usafi majumbani, dawa za kuua wadudu au vumbi ndani ya nyumba inayobeba vimelea vya maradhi.

Mzio (Allergy)
Hii hufanya mwili kuathirika na kutokea kwa mwasho pindi mwili unapopata msisimko, hali ambayo hujulikana kama mzio. “Mzio huanza pale mfumo wa kinga ya mwili unapobainisha mwili umevamiwa na kemikali na kuamuru seli husika kujibu kwa kuzalisha kemikali maalumu ambazo husababisha ngozi kuwaka kwa lengo la kuvunja nguvu za kemikali vamizi,” asema Dkt Swaka.

Watu wengi wana mzio wa vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na dawa za tiba, kemikali zinazotumika kutengenezea sabuni, vipodozi, aina fulani za vyakula, kemikali zinazowekwa katika maji kama vile ‘chlorine’, maji ya kuoga yenye chumvi nyingi na kemikali zinazotumika katika utengenezaji wa nguo, ikiwa ni pamoja na taulo ya kuogea.

Vyakula
Vyakula kama vile mayai, maziwa, samaki, nyama, karanga, vyakula vitokanavyo na unga wa ngano, kahawa, pombe na baadhi ya vyakula na vinywaji vinavyotengenezwa viwandani kwa kutumia kemikali vinaweza kusababisha ngozi kuwasha. Hali hii pia inaweza kutokea kutokana na kula vyakula vyenye mchanganyiko wa vikolezo kama pilau na viungo vingi.

Wataalamu wanasema watu wengi hawatumii kiasi cha kutosha cha matunda, mboga na mafuta yanayotokana na mimea au samaki, jambo ambalo huathiri vibaya afya ya ngozi.

Sumu mwilini
Tatizo jingine linalochangia mwili kuwasha wakati wa kuoga ni kutotumia kiasi cha kutosha cha maji ya kunywa kila siku. Hali hiyo inafanya mwili kuwa na upungufu wa maji na kuathiri vibaya afya ya ngozi na uwezo wake wa kuondoa sumu mwilini.

Ngozi isiyokuwa na afya njema inashindwa kutunza kiasi cha kutosha cha unyevu na kusababisha ukavu. Ngozi inapokuwa kavu, husisimka kupita kiasi wakati wa kuoga na kusababisha mwasho.

Maradhi ya zinaa/fangasi
Kuwashwa sehemu za siri kunaweza kuwa dalili ya maradhi ya zinaa. Bila kujali jinsia, mwasho unaweza kusababishwa na ugonjwa wa ngozi, magonjwa ya zinaa au mzio.

Sababu kuu za kuwashwa makalioni ni kutojisafisha vizuri, kula vyakula vyenye viungo vingi sana, kuhara, vidonda kwenye njia ya haja kubwa, maambukizi ya fangasi, minyoo na kadhalika.

Mara nyingi mwasho sehemu za siri huhitaji matibabu ya hali ya juu zaidi, ikiwa unawashwa kwa muda mrefu ni vyema kuzungumza na daktari.

Kuwashwa uume au sehemu zingine za siri za mwanaume husababishwa na sababu zilezile zinazosababisha mwasho sehemu zingine za mwili. Maambukizi hasa ya magonjwa ya zinaa ndio chanzo kikuu cha kuwashwa uume. Sababu nyingine ni maradhi ya fangasi, ugonjwa wa upele, kuwepo kwa chawa, mzio na maambukizi ya bakteria.

Kwa wanawake, mwasho unaweza kusababishwa na fangasi waitwao Candida. Dalili kuu ni kuwashwa ukeni, kuvimba na kutoa uchafu mweupe kama maziwa ukeni.

Saratani
Saratani ya ngozi na damu inaweza kusababisha ngozi kuwasha na kufanya mtu kujikuna.

Wasiwasi (Generalized Anxiety Disorder)
Ni ugonjwa ambao unatokana na hofu ya matukio fulani. Wakati mwingine husababisha kujikuna sehemu mbalimbali hata sehemu za siri.

Ugonjwa wa Sjogren (Sjogren’s Syndrome)
Ni ugonjwa katika mfumo wa kinga ya mwili unaoathiri tezi zinazosaidia mwili kutengeneza unyevunyevu kwenye macho na mdomo. Ugonjwa huu huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume.

Kisukari
Ni ugonjwa unaosababishwa na kasoro katika utengenezaji wa Insulin au utendaji kazi wake. Kisukari kilichokomaa kinaweza kusababisha maumivu ya tumbo, kichefuchefu, kizunguzungu na kuwashwa sehemu za siri.

Sababu zaidi
• Matatizo ya ngozi kama kukauka (xerosis), kuchomeka, makovu na kuumwa na wadudu
• Maradhi ikiwemo saratani ya damu, matatizo ya figo, kukosa madini.
• Matatizo ya neva
• Maradhi ya akili
• Mimba

Ufanyeje?
1. Wanaume kuosha vizuri uume, na wale ambao hawajatahiriwa wanapaswa kuosha kwa umakini zaidi hadi sehemu za ndani za ngozi.

2. Ziweke sehemu zako za siri kuanzia ndani ya makalio katika hali ya usafi na ukavu, kwa maana unyevunyevu unaweza sababisha maambukizi. Matumizi ya poda ya ‘Cornstarch’ yanaruhusiwa hasa kipindi cha joto kali.

3. Vaa nguo isiyobana sana, iliyotengenezwa kwa vitu asilia kama pamba. Badili nguo ya ndani (chupi) angalau kila siku.

4. Vaa kondomu kila unaposhiriki ngono na mwanamke usiyejua hali yake kiafya kiujumla.

5. Wanawake wanapaswa kuosha sehemu za siri kuanzia mbele kwenda nyuma ili kuzuia bakteria kutoka njia ya haja kubwa kuingia ukeni.

Hali ikizidi
Kulingana na tovuti ya www.mayoclinic.com, mtu anapaswa kumuona daktari;
• Ngozi ikiwashwa kwa zaidi ya wiki mbili bila kutulia.
• Hali inakuwa mbaya na kukuzuia kutekeleza majukumu yako ya kila siku na kukukosesha usingizi
• Mwili unaanza kuwasha ghafla na haufahamu chanzo chake
• Kuwashwa kunaandamana na dalili nyingine kama vile uchovu mwingi, kupunguza uzani wa mwili, kukojoa sana, kuhisi joto jingi au rangi ya ngozi kuwa nyekundu.

Kupunguza mwasho
• Kunywa maji kwa wingi
• Kuoga kwa haraka na kutotumia maji moto
• Kutotumia sabuni zilizo na marashi kali
• Kujipaka losheni zisizo na kemikali kali baada ya kuoga
• Kuepuka kutumia sabuni zilizo na marashi kufua nguo.
• Wataalamu wanasema watu walio na umri mkubwa hasa kuanzia miaka 65 huwashwa na ngozi kwa sababu huwa inabadilika kuwa nyepesi na isiyodumisha kiwango cha maji kinachohitajika mwilini.
• Mtu anaweza kuwashwa na ngozi wakati anapotumia au baada ya kutumia dawa fulani kama ‘aspirin’, za kutibu msukumo wa damu au saratani.


1592222170066.png


BAADHI YA MICHANGO YA WADAU KUHUSU TATIZO HILI:
Unatumia maji ya kisima au bomba? Kama umeshatumia yote na bado tatizo liko pale pale basi jaribu kubadilisha joto la maji unayotumia.

Hiyo ni allergy tu ambayo itaisha baada ya muda fulani.Mi mwenyewe nilikuwa nayo lkn iliisha yenyewe.

If symptoms persist then seek medical advise!
===

Itakua ni dryness. Jaribu kuoga na shower gel yenye moisturizer au kupaka mafuta ya dry skin.

Sababu lingine maybe maji tu yenyewe. cheki tatizo lilianza lini, kama ulihama au kusafiri hivi karibuni jaribu ku-link.

Kula samaki nyingi kuliko nyama (kama 150 to 250g 2 or 3 times a week) inasaidia kupunguza dryness.
Kama kuwasha kunaendelea pata ushahuri wa daktari (maana hapa sio hospitali, tunashahuriana tu kutokana na experiences)
===

Hii inaitwa acquagenic uticaria, naomba Google afu atapata maelezo mazuri. Lakini mara nyingi no specific matibabu, kikubwa unatakiwa upunguze exposure kwa majimaji kwa muda mrefu.

Kuoga tumia short time na tumia cotton towel and cotton cloths hata mashuka ya kutandika. Pale inapozidi meza antihistamine mfano cetirizin tabs 10mg od 5/7. Ila Google hiyo itakusaidia kupata maelezo mazuri.

All the best
===
1.Acha kabisa kuoga maji baridi- mimi nilipoacha kuoga maji baridi nilipata nafuu kubwa sana.

2.Jitahidi sana mwili usitapate baridi wakati bado haujakauka vizuri,jifunike vizuri mara baada ya kutoka kuoga na ninakushauri ununue BATHROBE mimi lilinisaidia sana.

3.Nunua Anti allergy kama CETIRIZINE AU LORATIDINE (mojawapo kati ya hizo) ziwepo karibu muda wote na uzitumie pale unakapoona kuwasha kunazidi na huwezi kuvumilia,naimani ukienda Pharmacy watakuelekeza namna ya kutumia.

kwa bahati mbaya tatizo hili kama zilivyo allergy nyingine halina tiba ila unaweza kupunguza adha unayoipata kwa kiasi kikubwa kama ukichukua tahadhari za kuto expose mwili wako mara baada ya kutoka bafuni (mimi nilikuwa nawashwa hata nikinyeshewa na mvua!) na kama bado ukiona tatizo linaendelea nenda hospitali yoyote iliyo karibu.
===
Dawa ingine ya Muwasho siyo lazima uwe wa mwili tu, bali kuna sehemu mbalimbali za mwili ambazo

zimejificha na fangasi uenda kujihifadhi katika sehemu hizo nazo unaweza kutumia maji ya aloe vera kwa

kutibu . Kwa jinsi gani unaweza kujizuia au kujitibu na muwasho kwa kutumia aloe vera. Jinsi ya kuandaa maji

ya Aloe vera kwa ajili ya kutoa muwasho na bateria.Chukuwa vikwanya vitano vya alovera kisha safisha kwa

maji safi, kata vipande hivyo kwenye sufuria ya kilo moja. Jaza maji kisha uweke jikono kwa ajili ya

kuchemka. Epua na uyaweke pembeni kwa ajili ya kpoa aukuwa na hali ya uvuguvugu. Toa majani ya

aloe vera katika sufuria na kisha weka katika ndoo tayari kwa kuonga.


Angalizo

Baada ya kuoga unatakiwa kukaa na maji hayo mpaka yatakapo kauka mwilini pia ni dawa ya harara na kufanya ngozi kuwa nyororo. Angalia Picha chini ya Aloe Vera.
View attachment 144519
===
Kwenda kupima ni jambo jema zaidi.Ila kwa dalili zako kuna uwezekano mkubwa sana damu yako itakuwa na over acidity(yaani kiwango cha acid/tindikali kwenye damu ni cha juu kuliko kawaida).Hii husababishwa na mambo mengi sana kama vile ulaji wa vyakula vibovu na matumizi ya madawa mara kwa mara;

Vyakula vibovu huweza kuwa vile vya kusindikwa viwandani kama vile juice,soda,tomato source nk,ulaji wa nyama kwa wingi,ulaji vya vyakula vya kukaangwa kwa wingi,unywaji wa pombe,uvutaji wa sigara na mengine ambayo si ya asili.
Madawa yanaweza kuwa ya antibiotic,diclofenac,panadol,dawa za kuongeza nguvu za kiume,uzazi wa mpango na mengine kama hayo.

Ili kuondoa tatizo unahitaji kula vyakula vya asili na kuachana na vile nilivyotaja hapo juu,kunywa maji mengi,mboga za majani zisiive sana kama vile spinach,celery,broccoli, juice za matunda kama vile parachichi pamoja na mbegu yake iliyosagwa,juice ya caroti,juice ya tikiti,juice ya papai na embe.Epuka sukari ya viwandani,epuka chumvi ya viwandani/chumvi ya unga na badala yake tumia ile ya mawe.

Kama utakuwa serious kwa kufuata ninayoeleza,kuanzia mwezi mmoja utakuwa umepona kabisa.

Karibu.
===
Kama upo kanda ya kaskazini kuna daktari bingwa wa allergy ana clinic binafsi pale YMCA, Amepatwa na allergy ya kitu fulani hapo nyumbani, sasa sambamba na kumpeleka kwa daktari bingwa wa allergy, hebu pia jaribu mbinu hii:

Allergy management by elimination: mwanzishie dawa ya minyoo, asipopata nafuu ufuate hatua hizi moja baada ya nyingine. Best wishe kaaaka
1. Safisha chumba anacholala na sebule anapokaa kwa umakini mkubwa.
2: badilisha mashuka na mablanketi yote anayotumia, mnunulie matandiko mapya
3: badilisha mafuta ya chakula mnayotumia au mpe chakula kisicho na mafuta kabisa, ale michemsho ya vyakula organic au vya asili.

4: badilisha sabuni ya kuoga na kufulia pamoja na tooth paste
Hatua hizi zitekelezwe moja baada ya nyingine hata kwa interval ya wiki moja moja ili kutathmini maendeleo.

Dada yangu alipona allergy kwa kubadilisha sabuni ya kuoga, kutokunywa fanta na mafuta ya kupikia, na mtoto wangu jaribio moja tu la kumbadilishia blanketi na sabuni ya kuoga alipona mazima!
===
Vipele vinakutokea ameneo gani hasa?

Kuna kipindi nilikua nawashwa sana na mwili na kutokewa vipele flani vinakua vyekundu, mwanzo nilijua ni maji ya kuogea nayotumia(ya chumvi) ikanibidi niwe nanunua yale ya boza(hayana chumvi) lkn tatizo liliendelea..... nikapima labda ni magonjwa ya zinaa, minyoo lakini wapi.

Kuna jamaa akaniambia jambo ambalo hadi leo lilinisaidia sana.

Kuna wakati upande wa pembeni tumboni huwa panauma.... sikutilia mkazo.... ila akaniambia ni dalili za figo kufeli ndo maana unapata magonjwa ya ngozi..

Dawa yake acha kutumia vinywaji kama soda, energy na pombe kali(kwa wakati huo ndo ilikua vinywaji vyangu, kiroba na redbull au energy)
Kisha nianze dozi ya maji, baada ya kusikia balaa la figo kufeli.... nilianza dozi ya maji kwa nguvu zote, sa1 hadi sa5 nahakikisha lita2 zimekata, napumzika, sa7 hadi sa11 nakata zingine2 kisha napumzika, sa1 hadi muda wa kulala nakata zingine2.

Kwa kweli matokeo yalikua mazuri, upele ulipona, maumivu sikipata tena.

Kwa hiyo ndugu, unaweza jua una magonjwa ya ngozi(vimelea) kumbe ni tatizo la sumu mwilini.

Mimi sina desturi ya kwenda hospitali wala kunywa midawa, napopewa ushauri wa njia za vyakula huwa nazingatia sana, hata malaria naitibu kwa machungwa tu.
===
Hili ni tatizo lililo nisumbua kwa miaka kama sita na hakuna dawa ilio nisaidia lakini nikushauri vtu vchache vlivo nisaidia had now nko fresh

1.Jaribu kubadirisha maji kama unaoga ya baridi jarbu kutumia maji ya moto.
2.Punguza mda unaotumia kuoga ili kupunguza contact na maji kwa mda mrefu
3.Tumia dodoki soft na usijisugue sana
4.Subiri ukauke ndio ujipake mafuta
5.Tambua mazingira yanayo chochea tatizo mfano mimi mikoa ya baridi ndio ilio kua inaniathir zaid.
Ni ayo tu.
===
Poleni sana waungwana!
siku moja nilisikikiza kipindi cha afya radio moja walikuwa wakizungumza juu ya tatizo la kuwachwa mara tu mtu unapotoka kuoga:-
Sababu
Ni allegy inayosababishwa na bacteria ambao aidha wanakuwemo kwenye maji au kwenye kifaa kinachotewa maji hasa magudulia yenye mfuniko mdogo ambayo hutunza uchafu ambao ambao husababisha fungus ambao mwisho wa siku ndio huleta mwasho mwilini. Pia huweza kutokea kwenye mabomba kutokana na mifumo mingi ya maji kutokuwa salama mfano mabomba ya maji safi kupasuka sehemu ambayo ni makutano na bomba la maji taka etc!

Tiba:
Hiyo ni allegy ivo unashauriwa kutumia anti-allegy lakini pia unaweza tumia shower gel ambayo hutengeneza layer laini inayokuwa ni kinga kwako wakati wa kuoga!

Naomba kuwasilisha, mtaniwia radhi hzo ni point chache ambazo nilizidaka siku hiyo sina utalaam wowote wa kiafya kwa hiyo sitegemei swali la kitaluma! Asanteni.
===
Ninafahamu sababu mbili za hili tatizo lakini zote zinahusiana na allergy.

Ya kwanza ni allergy kwenye maji, kitaalamu inaitwa 'aquagenic urticaria'. Kuna baadhi ya watu ambao wakikutana na maji huwashwa sana, wengine hupata hata maumivu ya ngozi na wengine hata wakinywa maji wanapata maumivu kooni. Hii hutokana na miili ya watu hawa kutopatana na maji.

Wanaweza wakatumia dawa za allergy (antihistamines) kama chlorpheniramine (piriton) au cetrizine nk, ili kutuliza lakini hazitibu. Matibabu yake ni kuepuka maji, simaanishi usioge lakini oga kwa muda mfupi kadiri utakavyoweza na epuka kunyeshewa na mvua.

Ya pili inahusishwa na uwepo wa kemikali aina ya sodium lauryl sulfate kwenye vitu kama shampoo, sabuni, cream za kunyolea nywele, na hata kwenye shower gel, hii nayo husababisha allergy ikiwa mtu anayeitumia hapatani na hii kemikali, matokeo yake huwashwa baada ya kutumia hivi nilivyovitaja. Matibabu ya hii ni kutumia sabuni au shampoo ambazo ni sodium lauryl sulfate - free. Ukinunua sabuni au shampoo angalia kama haina hiyo kemikali na nunua ukatumie.
===
PIA UNASHAURIWA KUSOMA MADA HII:
- Tatizo la kuwashwa mwilini baada ya kuoga: Fahamu chanzo, ushauri na tiba - JamiiForums
 
Mi nadhani kuna kitu huwa anakula ambacho ana allegy nacho. Mwambie ajichunguze vizuri - siku muwasho ukianza tu, akumbuke amekula nini na nini. Na inaonekana ni chakula anachokipenda maana huu muwasho ni wa muda mrefu.

Kuna ndugu yangu alikuwa akila karanga tu, atawashwa na kuvimba sana. Tulipogundua, mpaka leo karanga hagusi na lile tatizo limeisha

Ingawa jibu langu si la kisayansi zaidi, is worth trying, inaweza kumsaidia.
 
@Sinyolita,

Thanks kwa mchango wako Sinyolita, itabidi nikae nae nimuulize ni nini anapendelea kula kwa sana ajaribu kuacha tuone responce inakuwaje
 
Mi nadhani kuna kitu huwa anakula ambacho ana allegy nacho. Mwambie ajichunguxe vizuri - siku muwasho ukianza tu, akumbuke amekula nini na nini. Na inaonekana ni chakula anachokipenda maana huu muwasho ni wa muda mrefu.

Kuna ndugu yangu alikuwa akila karanga tu, atawashwa na kuvimba sana. Tulipogundua, mpaka leo karanga hagusi na lile tatizo limeisha

Ingawa jibu langu si la kisayansi zaidi, is worth trying, inaweza kumsaidia
ndugu hizi imani za kutukaza kula baadhi ya vyakula kwa madai ni areji ni mbaya sana, Mungu alimpa mwanadamu ruhusa ya kula, hata miye nilikuwa sioti nywele kwa mda wa miaka 3 nikiwa mdogo wakadai ati nisile samaki aina ya kambale, na kitimoto yaani n yama ya nguruwe, lakini ilikuwa ni ngumu kidogo, kwenye kitimoto, nikaenda church,
nikaombewa na sasa sina tatizo la namna hiyo, vitu vingine ni roho chafu tu
 
ndugu hizi imani za kutukaza kula baadhi ya vyakula kwa madai ni areji ni mbaya sana, mungu alimpa mwanadamu ruhusa ya kula, hata miye nilikuwa sioti nywele kwa mda wa miaka 3 nikiwa mdogo wakadai ati nisile samaki aina ya kambale, na kitimoto yaani n yama ya nguruwe, lakini ilikuwa ni ngumu kidogo, kwenye kitimoto, nikaenda church,
nikaombewa na sasa sina tatizo la namna hiyo, vitu vingine ni roho chafu tu

Mungu aliumba wanadamu,magonjwa na vifo.vyote hivyo aliviweka ili tusijisahau na tuwe karibu nae pindi vinapotusibu,.akatujalia imani ili tumwangukie na kumwangalia yeye.akatupa akili ya utambuzi toka enzi za adamu na hawa na kutupa ruhusa ya kuvipa majina vile alivyoviumba na pia kivisifu.

Pia aliumba kazi ili binadamu wategemeane na akazibariki ,navile vile kuwaonyeshea kidole wale wazitumiavyo ambavyo sivyo,nakuwaambia hawata uona ufalme wake [mafarisayo,watoza ushuru] na pia kupitia watendaji wake,aliwakumbusha binadamu umuhimu wa kumpa kaiza kwa yaliyo yake kaiza na kumpa mola yaliyo yake.

pia watendaji hao hao walikumbusha umuhimu wa afya na kusema mwenye afya hamuitaji daktari bali ni kwa wale walio wagonjwa.[musa aliinua nyoka wa shaba na kusema uumwapo na hawa basi muangalie huyu nawe utapona,.kuzingatia hilo ndio maana alama yao ni msalaba na nyoka] tafsiri ya imani ya dini inaharibiwa,.bongo nilipata mgonjwa ambaye ndugu zake walikataa asiongezewe damu,kisa ni Shahidi,...,.sitaki mjadala wa kiimani, ila dini inatumiwa vibaya na kugharimu maisha ya watu,.inapaswa kuchanganya elimu zote,.ya dunia na ya kidini[ a.ya mwenzako changanya na yako,.]
 
ni tatizo ambalo limejitokeza kwangu takribani miaka mitatu iliyopita hadi sasa! mara tu nimalizapo kuoga ninaanza kuwashwa mwili mzima kwa muda usiozidi dakika 15 na wakati mwingine unapojikuna vipele vidogovidogo hutokea. tatizo hili linaninyima raha mno kwa anaefahamu dawa anisaidie na pia si mbaya kama utanieleza chanzo cha tatizo.
 
ni tatizo ambalo limejitokeza kwangu takribani miaka mitatu iliyopita hadi sasa! mara tu nimalizapo kuoga ninaanza kuwashwa mwili mzima kwa muda usiozidi dakika 15 na wakati mwingine unapojikuna vipele vidogovidogo hutokea. tatizo hili linaninyima raha mno kwa anaefahamu dawa anisaidie na pia si mbaya kama utanieleza chanzo cha tatizo.

I thought niko peke yangu who have this problem!!mzee am glad that u posted this topic,ngoja tuone wengine wana ujuzi gani juu ya hili
 
Unatumia maji ya kisima au bomba? Kama umeshatumia yote na bado tatizo liko pale pale basi jaribu kubadilisha joto la maji unayotumia.Hiyo ni allergy tu ambayo itaisha baada ya muda fulani.Mi mwenyewe nilikuwa nayo lkn iliisha yenyewe.
If symptoms persist then seek medical advise!
 
ni tatizo ambalo limejitokeza kwangu takribani miaka mitatu iliyopita hadi sasa! mara tu nimalizapo kuoga ninaanza kuwashwa mwili mzima kwa muda usiozidi dakika 15 na wakati mwingine unapojikuna vipele vidogovidogo hutokea. tatizo hili linaninyima raha mno kwa anaefahamu dawa anisaidie na pia si mbaya kama utanieleza chanzo cha tatizo.

I have the same tatizo,nilifanya medical check up ya haja kubwa nikambiwa kuwa nina minyoo na Amoeba pamoja na alergy.......nikapewa dawa! You cant believe, nilipona kabisa but this lasted for only few days na sasa tatizo lipo vilevile na nafirikia sijui sasa nifanyaje!!

Alafu nikienda DSM, Arusha na Moshi maji ya kule hayawashi kabisa but nikioga maji ya huku Shinyanga......wajamani iyo kero ya mwasho ninayopata sisemi!!!! Maji ya huku ni ya bwawani/mvua si unajua huku shy??

Sijajaribu kubadili joto la haya maji kwa kuyachemsha,,,sipendi sana maji ya moto,,,,naoga all the time maji baridi.....embu watalaam tupeni ushauri jamani tupo wengi tunateseka sana na hii hali. Nami nawasilisha!
 
mimi naona kama una allergy na sabuni unayotumia, kemikali zinazotumika katika sabuni hizo hazipatani na ngozi yako.

hivyo basi jaribu kubadilisha na kutumia hizi sabuni zenye virutubisho vya kiasili (with natural ingredients) kwa mfano asali, avacado, na kadhalika. sabuni hizi hupatika mara nyingi katika maduka ya kina mama wajasiriamali
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom