Tatizo la kuwashwa mwili mara kwa mara- Fahamu chanzo, pata ushauri na tiba ya tatizo hili

Naomba niandike kwa herufi kubwa ili tu- experience kitu apa


Ilianza kama masihara mwanzoni mwa disemba 2020, mpaka kuja kustuka baadae nkaona nateseka nikafika duka la dawa kubwa tu lenye wataalamu na lina garama ndogo sana kwa dawa zao.... Nikamueleza pale muhudum akasema iyo itakua fangasi maana nilikua nawashwa mwili maeneo ya kwapani, mapajani, sehemu za mbavu, sehemu ya kitovo karibu na mavuzi na pumbu liliota vipele au niseme uvimbe maana vilikua vimeumuka ambavyo kuna muda vilikua vinawasha na uume ulikua na upele na hadi kwenye kichwa cha uume...


Dozi ya kutosha akanipa nikatumia ndani ya siku 3 miwasho ikaisha na vipele kwa pumbu na uume vikapungua siku ya nne mzigo ukaanza upya....

Nikamwona daktari kwa mara ya kwanza nikapima mkojo na haja kubwa nikakutwa na uti pamoja na minyooo dokta akanipa dozi akasema hiii kiboko ya minyooo... Nikasema poa.... Siku 2 nikawa poa siku ya 3 mzigo ukaanza upya na dozi ndo inaelekea mwisho...


Nikaenda hospital ingne baada ya kumaliza dozi wakati huo hapo katikati ya dozi ni kujikuna mwanzo mwisho hasa nikitoka kuoga na muda wa kulala then saa 1130 alfajiri ndo nakua poa siwashwi kabisa then usingizi unakuja mpaka saa 1 muda wa kazi za watu. Japo na mchana miwasho inatokea ndo vile hakuna namna tu.


Nikamwona daktari na kumuonesha dawa zote nilizotumia akashauri nikapime mkojo na damu ili kuchek magonjwa ya zinaa, nikachek pale majibu uti bado ipo na damu iko poa... Akasema itakua mchafuko wa damu pia alleji... Nikaandikiwa sindano kama dozi 2 ivi siku 3 na ingine siku 5.. Na vidonge vya kutosha kwa ajili ya uti na dawa ya kupaka siku iyo ni 31/12/2020 naumaliza mwaka na kuanza mwingine nikiwa na mzigo wa dawa ila nkaona poa tu, afya kwanza.... Sindano ya siku ya kwanza hadi ya 3 niko poa ya 4 wadau hali ikalipuka kwa speed ile ile mpaka sio poa nilipiga simu kwa daktari akanielekeza dawa ingne ya kupaka na sindano yake na cetrizen wakati huo sijamaliza ile dozi ingne... Ila sikwenda kuitafuta..

Me ni mtu wa kampani na wadau katika starehe za apa na pale kwa iyo mwaka mpya tuliamua kufrahia home kwa mshikaji tukia na wadau wa kutosha kama marafiki... Siku ya tarehe 4 nilikutana na mmoja ya wadau tuolokua nao kwenye mkesha akaniuliza mbona siku hiyo skua natupia pombe nikamweleza nilikua na dozi.... Nikamweleza hali yangu kiujumla... Akanambia pia na yeye alikua na shida kama hiyo na alitumia dawa na akapona japo ye ni wa kike, baada ya apo akaenda kunichukulia creem inaitwa skderm-creem na sabuni ya kuogea inaitwa protex ile ya kijani... Toka nimeitumia siku hiyo tarahe 4 mpaka leo sijakua ni miwasho ka ilivokua apo nyuma... Japo vilepe vya kwenye uume na pumbu bado vipo je kuna dawa ya kukausha?

Note : japo kwa sasa nahisi miwasho kwa mbali sana nahisi ni kwa kua nimejaribu kuacha kuitumia leo ni siku ya 4 ili nijue je natakiwa niendelee na creem iyo ndo yawe mafuta yangu au vp... Swali kwenu pia kutumia izo dawa za kupaka kwa muda mrefu hakuna madhara?

Mwisho ni kwamba ugojwa huu unaambukiza kwa experience yangu na watu wa karibu niliongea nao kupitia nguo pia hata sex. Maswali yaendeleeee
 
Naomba niandike kwa herufi kubwa ili tu- experience kitu apa

Ilianza kama masihara mwanzoni mwa disemba 2020, mpaka kuja kustuka baadae nkaona nateseka nikafika duka la dawa kubwa tu lenye wataalamu na lina garama ndogo sana kwa dawa zao.... Nikamueleza pale muhudum akasema iyo itakua fangasi maana nilikua nawashwa mwili maeneo ya kwapani, mapajani, sehemu za mbavu, sehemu ya kitovo karibu na mavuzi na pumbu liliota vipele au niseme uvimbe maana vilikua vimeumuka ambavyo kuna muda vilikua vinawasha na uume ulikua na upele na hadi kwenye kichwa cha uume..
Poa mimi ninaugonjwa kama huu bado mpaka sasa unanisumbua sana yaaaani unawasha sana unajikuna mpaka mpk unabandua kingozi lakini bado panawasha tu.

Ebu acha nami niinunue hiyo dawa nijaribu kuitumia
 
Poa mimi ninaugonjwa kama huu bado mpaka sasa unanisumbua sana yaaaani unawasha sana unajikuna mpaka mpk unabandua kingozi lakini bado panawasha tu

Ebu acha nami niinunue hiyo dawa nijaribu kuitumia
Mkuu ulishapona huu ugonjwa, Kama ulipona ulitumia dawa gani??
 
Naomba niandike kwa herufi kubwa ili tu- experience kitu apa

Ilianza kama masihara mwanzoni mwa disemba 2020, mpaka kuja kustuka baadae nkaona nateseka nikafika duka la dawa kubwa tu lenye wataalamu na lina garama ndogo sana kwa dawa zao.... Nikamueleza pale muhudum akasema iyo itakua fangasi maana nilikua nawashwa mwili maeneo ya kwapani, mapajani, sehemu za mbavu, sehemu ya kitovo karibu na mavuzi na pumbu liliota vipele au niseme uvimbe maana vilikua vimeumuka ambavyo kuna muda vilikua vinawasha na uume ulikua na upele na hadi kwenye kichwa cha uume..
Mkuu huu ugonjwa na Mimi umenipata yaani nawashwa haswa, tulizo langu limekuwa citrizen . He wewe ulishapona na ulitumia dawa gani?
 
Ajaribu kucheki.inaweza kua alergy. Nilishawahi kupatwa na kitu kama hicho mwili mzima kuwashwa hasa ukivua nguo.nilipima kila kitu mpka nikaenda legency hospital wakachukua damu iende south africa kwa vipimo.wakasema hamna kitu. Nikaenda agha khan kwa mtaalamu wa magonjwa ya ngozi.akaniangalia akasema ni wadudu wanaitwa scabies. Akanipa dawa ya kupaka ndo nikapona.sikuamini. sababu nilichoma sindano za kila aina sikupona. Nakushauri tafuta specialist wa magonjwa ya ngozi.
Dawa inaitwaje
 
Wakuu habari za wakati huu,kuna jamaa yangu amechanganyikiwa na asijue afanye nini kiasi kwamba ameanza kuhisi kama pengine tatizo lake ni la kurogwa ama halina tiba japokuwa mimi nimemuaminisha kuwa hakuna kinachoshindikana chini ya jua....
Vipi rafiki yako alipona?
 
Mkuu ulishapona huu ugonjwa, Kama ulipona ulitumia dawa gani??
Ndy yangu ukweri hu ugonjwa asikudanganye mtu hauna dawa bali ni mazingira tu nihisi ndo sababu...

Mimi nilienda hospital fulani pale kibaha matibabu niliambiwa 55 elf.nikagahili mazima.

Nikanunua sabuni ya kuogea protex na mafuta ya nazi nikawa napaka, hali yangu ikaanza kuimarika.

Now nipo mwanza naona hali yangu naona inazidi kuimalika sijikuni kama nilipo kuwa pwani naona hapo pia hali ya hewa inachangia (mazingira )

Ukweri usiku nilikuwa nasumbuka sana yani baada tu ya kuoga unajikuna mpaka ngozi unaihurumia usiku hakuna kulala.jamani ugonjwa mwingine mpaka karaha, bora kusimuliwa kuliko yakukute.

Kwangu nahisi kuoga maji yaliyo tuama mfano maji ya mvua yaliyo tuama muda mrefu kwenye karo, pia kutosafisha visima mara kwa mara ndo sababu.

Yangu ni hayo tu waungwana.
 
Kama kuna mtu bado hii hali inamsumbua... akanunue dawa inaitwa BBE ni dawa ya upele ni ya maji.. inauzwa elf 2 kwa uku nilipo... alooioo imenisaidia kwa aslimia 98.. sa iv nalala usingiz saaaf.. yasimkute mtu kuwashwa kwa namna hii.. maana kama ni dawa hadi za sindano nshatumia sana na iyo nlkua nayo.. nilivoshauriwa kutumia mfululizo.. sikuamin kilichotokea... maana nlitumia ile skderm ilinisaidia kwa muda ila baadae nayo ikadunda
 
Ni tatizo baya linatesa sana tumehangaika kwa muda, tumeenda hospital tumepewa dawa na kuchomwa sindano lakini wapi. Tumetumia sabuni na dawa za kupaka za kila aina tatizo lipo. Kuhusu HIV ni negative. Naomba wataalamu mtusaidie au yoyote anayejua tiba ya tatizo hili.
 
Ni tatizo baya linatesa sana tumehangaika kwa muda, tumeenda hospital tumepewa dawa na kuchomwa sindano lakini wapi. Tumetumia sabuni na dawa za kupaka za kila aina tatizo lipo. Kuhusu HIV ni negative. Naomba wataalamu mtusaidie au yoyote anayejua tiba ya tatizo hili.
Pole,
1: Muwasho uko sehemu gani zaidi ya mwili?
2: Watu wangapi kwenye familia wana muwasho?
3: Kuna mtu alikuja hapo kwako akiwa na shida hiyo?
4: Kuna mtu alienda sehemu akakuta kuna watu wanawashwa?
5: Kuna kitu kipya mnakula au kupaka?
6: Ni mara ya kwanza kutokea au huwa kuna matatizo ya aina hiyo mara kwa mara?
 
Ungeandika ulitumia dawa,sindano na sabuni gani ili wanaoshauri wasirudie ulichotumia
 
Back
Top Bottom