Tatizo la kuwashwa mwili mara kwa mara- Fahamu chanzo, pata ushauri na tiba ya tatizo hili

Wana Jf kwa anayefaham dawa nzuri ya allergy aniambie maana nasumbuliwa na ttzo la kuwashwa na kutokewa na viupele sehem mbali mbali ya mwili
Hili tatizo nami lanisumbua sana. Nilipata matibabu lakini bado halijatengemaanazidi kuhaha na vipimo
 
Vipele vinakutokea ameneo gani hasa?

Kuna kipindi nilikua nawashwa sana na mwili na kutokewa vipele flani vinakua vyekundu, mwanzo nilijua ni maji ya kuogea nayotumia(ya chumvi) ikanibidi niwe nanunua yale ya boza(hayana chumvi) lkn tatizo liliendelea..... nikapima labda ni magonjwa ya zinaa, minyoo lakini wapi.

Kuna jamaa akaniambia jambo ambalo hadi leo lilinisaidia sana.

Kuna wakati upande wa pembeni tumboni huwa panauma.... sikutilia mkazo.... ila akaniambia ni dalili za figo kufeli ndo maana unapata magonjwa ya ngozi..

Dawa yake acha kutumia vinywaji kama soda, energy na pombe kali(kwa wakati huo ndo ilikua vinywaji vyangu, kiroba na redbull au energy)
Kisha nianze dozi ya maji, baada ya kusikia balaa la figo kufeli.... nilianza dozi ya maji kwa nguvu zote, sa1 hadi sa5 nahakikisha lita2 zimekata, napumzika, sa7 hadi sa11 nakata zingine2 kisha napumzika, sa1 hadi muda wa kulala nakata zingine2.

Kwa kweli matokeo yalikua mazuri, upele ulipona, maumivu sikipata tena.

Kwa hiyo ndugu, unaweza jua una magonjwa ya ngozi(vimelea) kumbe ni tatizo la sumu mwilini.

Mimi sina desturi ya kwenda hospitali wala kunywa midawa, napopewa ushauri wa njia za vyakula huwa nazingatia sana, hata malaria naitibu kwa machungwa tu.
 
pole mno Anderson,yes jitahidi kumwona daktari wa masuala ya ngozi,ingawa ni gharama jitahidi afya yako ni muhimu,ila wanafamilia wa JF wanaweza kusaidia kuitafuta dawa atakayo kuandikia doctor ,elewa familia hii imetawanyika mno hapa duniani.please do that .
 
Ngozi inakuwa kavu na kuwasha. Kwa muda huu kupunguza mwasho unaweza kunywa piriton moja ukiamka asubuhi lakini nenda kwa daktari
Mm hupata shida hii nikioga kisha nikajifuta maji na taulo hasa nyakati za usiku. Mwili hiwasha kwa muda fulani haizidi 30min hv
 
Nasumbuliwa na vipele na vinawasha sana au nimoja ya dalili ya hiv
Umepiga pa moto mkuu.??
Pole sana..

Sidhani kama ni dalili ya HIV coz mie nilisumbuliwa navyo sana utotoni inaweza kuwa ni magonjwa ya ngozi..

Acha kubandua hovyo ..
 
Mimi kuna mama alinipa dawa ya kienyeji nikanywa lakini hakunionyesha mti. alimambia hadi nmpe hela. niliondoka sijapata hela. yule mama alikuwa anaitwa mama bahati. ntarudi kumtafuta kule kyaruyonga. Mkuu utazunguka hospital zote hautapata dawa. yaani mimi nilisaidiwa hadi na ndugu na jamaa. mara watu waniambie minyoo,areji mara waseme amoeba. ilikuwa inanisumbua sana hasa asubuhi. mtu unajikuna huku unasikia utamu kwa mbali. nilikaa miaka 4 bila kupona but toka 2000 hadi leo sijaugua tena.
Tujuzane ndugu yangu tunapata shidaa
 
Wakuu habari za wakati huu,kuna jamaa yangu amechanganyikiwa na asijue afanye nini kiasi kwamba ameanza kuhisi kama pengine tatizo lake ni la kurogwa ama halina tiba japokuwa mimi nimemuaminisha kuwa hakuna kinachoshindikana chini ya jua.

Ipo hivi,jamaa anasumbuliwa na MIWASHO sehemu mbalimbali za mwili wake anasema huwa inamtokea sana especially usiku anavyokuwa kajipumzisha,anasema pia huwa hata mchana kunakuwa kama kuna vitu vinachoma choma katika mwili wake,mfano anasema kichwani,mapajani,anawashwa katika njia ya haja kubwa na muda mwingine huwa kama kuna vitu vibatembea katika sehemu hizo tajwa mpaka mikononi.Ameanza kupata hii tabu takribani miezi sita sasa.

Alivyoanza kupata haya matatizo mwanzoni ndipo mateso ya madaktari akaanza kukumbana nayo.Amekwenda kwa mara ya kwanza hospitali mganga akasema wampime magonjwa ya ngono kwanza wakihisi atakuwa na KASWENDE au HIV lakini hakuwa nayo,dokta akasema ni fungus akapewa madawa ya mwezi mzima unakunywa kimoja kila siku then ni gharama,baada tu ya kumaliza dose vikatulia.amekaa kama mwezi miwasho ikaanza,kaenda hospital wakasema itakuwa ni minyoo tena wakasema minyoo sugu na akapewa dawa ya minyoo sugu(jina nimelisahau ni zaidi ya mabendazole na albendazole) kanywa siku tatu lakini hazijamsaidia na miwasho inaendelea.

Ndugu zangu wataalamu hususani medical officers msaada kwa huyu rafiki yangu,atumie dawa gani? Mimi nahisi atakuwa na fungus sugu maana amesema hata ulimi muda mwingine huwa kama kuna tuvidonda tunakuja na kupotea,je hakuna kipimo kweli cha kuchunguza fungus maana kuna jamaa aliniambia hakipo? Msaada maana kama ni wadudu wanaendelea kumuathiri ndani kwa ndani.
[HASHTAG]#Dogo[/HASHTAG] G
 
Back
Top Bottom