Tatizo la kuwa na harufu mbaya kinywani (bad breath) - Chanzo, dawa za kuzuia na ushauri

Ni matumaini yangu kuwa ni wazima wa afya na mnapambana kulijenga taifa kwa wagonjwa, majeruhi na waliopata majanga au matatizo mbalimbali poleni sana Mungu yuko pamoja nanyi.

Bila kupoteza muda twende kwenye mada ndugu wanajf nimekuwa na tatizo la kunuka kinywa hasa kwa mwaka huu imefikia hatua hadi mpenzi wangu na rafiki zangu wakaribu na wenye mapenzi mema wameniambia kuhusu kutoa harufu mbaya kinywani.

Kwa kweli najisikia vibaya sana kwa tatizo hili kuna jino la chini (gego) limechimbika na kuoza naombeni ushauri wenu nifanyeje kinywa changu kiwe safi na kisinuke angali nasukutua mara mbili au tatu kwa siku? Asanteni sana na natanguliza shukrani wakuu
Nitafute nipate kukutibia unayo maradhi ya mdomo aka (halitosis).Nitafute kwa wakati wako nipate kukutibia ili uweze kupona.
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili mzizimkavu. Au boonyeza hapa.Mzizi Mkavu
 
Asante mkuu kwa ushauri wako.
Mkuu nitafte nikuunganishe na mtaalam wa kinywa, ana dawa nzuri sana na utaleta mrejesho.
Dawa yake 100% ni mitishamba na ameitafiti kwa miaka 5 kwa kushirikiana na Daktari toka Usa.
Wameipaki vizuri mno.
Mimi nilipatwa na tatizo la meno kuwasha sana, nilitumia siku 3, tatizo lilikoma sasa ni mwaka.
Kuna watu waliokuwa na matatizo ya midomo kunuka sana, wengine meno kuoza hiyo dawa imewaponya.
 
Habarini.

jamani mwenzenu nina tatizo hilo la kutoa harufu mbaya kinywani kusema kweli linaninyima raha kabisa hapa majuzi nimemaliza kutumia mouth wash moja inaitwa MEDI-ORAL nilifikiri ingemaliza tatizo lakini naona bado.

Tafadhalini naomba msaada wa nini nifanye/kutumia ili niondokane na tatizo hili, kusema kweli linaninyima uhuru wakati wa mazungumzo.
 
Tatizo laweza kuwa sio kinywa tatizo linaweza kuanzia tumboni unakojaza vyakula visivyosagika kirahisi na matokeo yake vinaoza na kushindwa kutoka kwa njia ya haja kubwa hivyo unabaki kutembea na choo tumboni na harufu kutokea kinywani.

Kama unakula vyakula vigumu kusagika tumboni kama nyama na vyakula vyenye gesi nk.tafadhali acha sasa fanya hivi asubuhi kunywa maji ya uvuguvugu halafu ufanye mazoezi kidogo hata ya kuruka kamba baada ya muda utapata choo na mchana kula chakula chepesi na usiku baada ya muda hilo tatizo litaisha.

Pia nyama ngumu zinazonasa kwenye meno sometimes zinaoza na kusababisha hiyo shida possibly matatizo chanzo chake kinasababishwa na hayo mambo mawili.
 
Habarini.
jamani mwenzenu nina tatizo hilo la kutoa harufu mbaya kinywani kusema kweli linaninyima raha kabisa hapa majuzi nimemaliza kutumia mouth wash moja inaitwa MEDI-ORAL nilifikiri ingemaliza tatizo lakini naona bado.

Tafadhalini naomba msaada wa nini nifanye/kutumia ili niondokane na tatizo hili, kusema kweli linaninyima uhuru wakati wa mazungumzo.
Aisee pole sana ndugu.

Swali lingine, hivi utajijuaje kama unatoa harufu mdomoni, manake unaweza jitamba unaongea sana kumbe unatoa harufu mdomoni halafu hujui.

Njia sahihi ya kujua kama unatoa harufu mdomoni wewe mwenyewe ni zipi jamani???
 

Similar Discussions

14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom