Tatizo la Kuvimba Miguu: Chanzo, Ushauri, dawa na tahadhari (pamoja na wajawazito)

Nimeshasemaga humu tuna mabingwa wa kila idara tajwa humu!

Yani ikishindikana tatuzi la jambo lako humu ni bora hata usingezaliwa hapa Tanzania!

Kama haujatosheka na majibu subiria kwani bado cjawaona baadhi WanaJF!

Pole Kaka!
 
.......I mean atapona kwa kutumia dawa, vile vile mjaribu kwenda hospital ya agha khan mama apate kipimo kinachopima viungo vyote vya mwili, hapo tatizo litagundulika kwa urahisi.

Nimewafahamu watu kadhaa nao walikuwa wanaumwa umwa na kupewa vidonge na hawakupona..........lakini baada ya kupata kipimo hicho wakagundua ugonjwa mapema na kutatua tatizo.

wagonjwa na ndugu wa wagonjwa wengi huwa hawawezi kuwasiliana vizuri na wahudumu wa afya - mkienda tena hospitali muongee vizuri kwa kirefu na daktari muangalie uwezekanowa vipi zaidi. na dawa anazotumia kwa sasa ni dawa gani?
nakubaliana na mdau hapo juu kuhusu matatizo ya moyo, figo na kadhalika.
 
Ndugu wataalam na wenye uzoefu, kuvimba miguu wakati ukiwa na ujauzito ni kitu cha kawaida na je kinatibikaje? Hii imetokea katika ujauzito wa miezi kati ya tano na sita. Nitashukuru sana.
 
Ndugu wataalam na wenye uzoefu, kuvimba miguu wakati ukiwa na ujauzito ni kitu cha kawaida na je kinatibikaje? Hii imetokea katika ujauzito wa miezi kati ya tano na sita. Nitashukuru sana.

Kuvimba kwa miguu wakati wa ujauzito huitwaToxicosis (gestosis). Hii ni hali ya wanawake wajawazito, kutokana na sumu (toxemia) ya vitu hatari, ambayo ni sumu katika mwili wa mama mjamzito wakati wa maendeleo ya kukuwa kwa mimba, hali hii huambatana na dalili nyingi ambazo husababiswa na kushindwa kufanya kazi kwa mfumo mkuu wa neva, moyo na mishipa na matatizo ya ugonjwa wa metabolic.

Kwa hali hiyo basi toxicosis imegawanyika katika sehemu mbili. toxicosis ya mapema mwa mimba kati ya mwezi wa kwanza mpka wa tatu, na toxicosis inayoanza baadae. yaani baada ya miezi mitatu.. Katika hali hiyo dalili zake hutofautiana.. Toxicosis zianzazo mapema ni kawaida kuonekana katika miezi mitatu ya kwanza,lakini huenda wakati mwingine mpaka mwanzoni mwa mwezi wa nne wa ujauzito hata wa tano.

Toxicosis inayotokea baada ya miezi mitatu ya mimba mara nyingi huwa inasababishwa na mabadiliko makubwa katika mwili wa mjamzito, ambyo kwa upande mwingine tunasema ni kama sumu (toxemia) ndani ya mwili., Na niwakati huo tunaona dalili zote za mimba kwa mjamzito. kwa wakati huo hiyo huesabika sasa kama fisiologia ya kawaida katika mwili wa mwanamke.
sababu halisi na njia ya sumu (toxemia) mapema mwa mimba si hazijulikani bado. Bila shaka ukweli kwamba toxemia ni udhihirisho wa majibu ya mabadiliko ndani ya mwanamke katika kuendeleza mimba. Sababu kubwa zifanyazo toxicosis itokee mapema kwa wanawake wajawazito ni kwamba hawapati usingizi wa kutosha, kazi nyingi, lishe duni, kuvuta sigara, matumizi mabaya ya pombe.


Dalili za mapema za toxicosis katika mimba ni mwanamke analalamika na hali ya udhaifu, usingizi, kuwashwa, huzuni, na afya duni, na mate kwa wingi kuongezeka, kupoteza hamu ya kula, mabadiliko ya hisia ladha, kichefuchefu, kutapika, na kupoteza uzito. Mengine lakini ni mara chache hutokea, sura ya ugonjwa wa ngozi (ngozi vidonda), pumu, wanawake wajawazito (mabadiliko ya reactivity ya bronchi), na mkazo wa misuli (kukakamaa).

Kutapika wakati wa ujauzito ni moja ya madhihirisho ya kawaida ya toxemia katika mimba. kiwango cha maambukizi ya kutapika wakati wa ujauzito ni 60%, ambapo 10% unahitaji matibabu. Kutapika kawaida hutokea wakati wa wiki ya kwanza hadi wakati mwingine wiki ya 20 ya mimba. Kawaida,kuanza kutapipika mapema husababisha hali kuwa ngumu.

Hali ya kutapika imegawanyika katika makundi matatutofauti, . Kundi la kwanza ni lile rahisi Kutapika hutokea zaidi ya mara 5 kwa siku, mara nyingi baada ya kula. Kwa ujumla hali ya mwanamke hubakia kawaida, na kupoteza uzito wa kilo si zaidi ya 3. kundi la pili ni kutapika kwa wastani. Kutapika hutokea mara 10 kwa siku (ukiwa na njaa au baada ya kula) na kupoteza uzito kwa wiki 2 inaweza kuwa 3 kwa kilo moja. hali ya mwanamke mjamzito ni inazidi kuwa mbaya. kiwango cha mapigo ya moyo kuongezeka, wakati shinikizo la damu hupungua kinyume chake. Tatu , Kutapika hutokea mara 25 kwa siku. Hii husababisha , kuishiwa maji na uzito haraka hasara wakati wa ujauzito (kupoteza uzito huweza kufikia kilo 10). Ngozi yake inakuwa kavu na huru, kinywa chake harufu mbaya, joto la mwili huongezeka, mapigo ya moyo huongezeka, shinikizo la damu itapungua, kuna uchovu kwa ujumla.

Drooling (ptyalism) ni dalili ya pili ya kawaida ya toxemia mwanzoni au katikati mwa mimba, na mara nyingi ahuongozana na kutapika wakati wa ujauzito. Katika baadhi ya matukio, mate ni makali kiasi kwamba husababisha mwanamke mjamzito kupoteza lita zaidi ya 1.5 ya mate. Pamoja na mate,mwili hupotezaprotini na chumvi za madini, NA HII NDIYO SABABU KUBWA YA KUVIMBA MIGUU. Hali hiyo ikiendelea, mwanamke mjamzito huitaji matibabu.

Kuzuia toxicosis mapema ni kutibu kwa wakati unafaa magonjwa sugu, kuondoa uchovu wa akili, na kuweka mazingira mazuri. Kumbuka kuwa sumu mwilini (toxemia) -ni ishara ya matatizo. Wakati una dalili cha kwanza kuwasiliana na wataalam-gynecologist. Katika kipindi hiki mazoezi ya kutembea ni muhimu sana.

Wakati wa toxicosis ni muhimu sanawa kula kidogo lakini milo mara kwa mara. Chakula lazima kiwe cha baridi na kifurahie. Kupima mwenyewe uzito wako mara kwa mara, kama uzito wako ukipungua sana- si ishara nzuri. lazima uwasiliane na daktari wako mapema. Pamoja na afya mbaya, mimba huhitajika kutunzwa, kwa sababu wakati mwingine toxemia likiendelea, huwa kali zaidi. Lakini mtoto akianza kupigapiga tumboni huhisi kuwa ni furaha kwa maisha yako ya baadaye.
 
baada ya kuwa nimekuelezea , kwa hali yako wewe dada inabidi ukamuone daktari. utapimwa mkojo kama unapoteza proteini nyini. itakupbidi upunguze vyakula vya proteini, zaidi daktari atakuelezea
 
vicent ni kweli mtu akipoteza protein anavimba miguu yaani kunakuwa na water retention, lakini si kweli mtu akipoteza chumvi anavimba miguu the vise versa is true. mtu anapokuwa mjamzito baadhi ya homoni za kike oestrogen huongezeka ili kulinda mimba, na zingine kuzuia kupata mimba wakati unamimba pamoja na kazi hizo pia hufanya kazi ya kuhifidhi maji mwilini hivyo maji huongezeka na kusababisha kuvimba miguu na matatizo ya presha kwa mama wajawazito, kuna faida pia kwa kuongezeka kwa maji mwilini maana damu inakuwa nyingi na kumzuia mama asipoteze damu na kufa anapojifungua, nakushauri umuone daktari maana hapo ni uhai wa watu wawili kwa hiyo inahitaji care ya pekee.
 
madaktari mpo? Kama mznavyojua mie ni mjamzito miezi mitano karibia sita sina tatizo lolote lile ila najishangaa kuona miguu yangu inavimba!
Je hili ni tatizo? Nimekosa amani kabisa maana nayoelewa miguu ina vimbaga dakika za mwishoni
yaani karibu na kujifungua




0
 
madaktari mpo? Kama mznavyojua mie ni mjamzito miezi mitano karibia sita sina tatizo lolote lile ila najishangaa kuona miguu yangu inavimba!
Je hili ni tatizo? Nimekosa amani kabisa maana nayoelewa miguu ina vimbaga dakika za mwishoni
yaani karibu na kujifungua




0
pole sana, kuvimba ni miguu peke yake ama na sehemu nyingine kama uso na mikono hasa vidole? ni vyema kufika hospiali kupimwa pressure yako iko vipi, wakati mwingine huwa ni kuvimba miguu kusiko na madhara, inaitwa innocent edema of pregnancy, lakini hili tunalisema pindi tunapofika hospitali kupimwa pressure, protini kwenye mkojo, na vingine kama daktari atakavyoonelea.
 
pole sana, kuvimba ni miguu peke yake ama na sehemu nyingine kama uso na mikono hasa vidole? ni vyema kufika hospiali kupimwa pressure yako iko vipi, wakati mwingine huwa ni kuvimba miguu kusiko na madhara, inaitwa innocent edema of pregnancy, lakini hili tunalisema pindi tunapofika hospitali kupimwa pressure, protini kwenye mkojo, na vingine kama daktari atakavyoonelea.
ni miguu peke yake, kuna wakati inavimba na
kuna wakati inaabhia
 
Kama kuvimba miguu ina ambatana na Hypertension na Proteinuria na dalili ya EPH Gestosis. Hii ni hali mbaya kwa mama mjamzito. Inahitaji ufwatilaji mzuri kipindi cha uja uzito na ifikapo karibu na kujifunguwa.

Kama ni kuvimbaa miguu tu, utahitaji kufanya mazoezi ya wakati wa ujauzito. Good Luck.
 
mi nakushauri uende NIMRI,kitendo cha kutoonekana kwa tatizo hakimaanishi huan vijidudu/vimelea vya matende.soma elephatiasis
 
Hello!Bwana mimi nilishawahi umia GOTI nilipokuwa kidato cha pili nikiwa timu ya shule pale TAMBAZA Sec miaka hiyo!
Nilihangaika na huo mguu kwa zaidi ya mwaka na nusu nikiwa nimepelekwa hospital mbalimbali bila kupona.
Kuna siku moja nikiwa nimekaa nyumbani barazani kwa nyumba za National Housing pale Magomeni,alipita BIBI Mmoja ambaye simfahamu alisimama na kuniangalia jinsi mguu ulivyojaaa na kuniuliza nilifanya nini mpaka mguuu ukawa hivyo!!!!Nilimuelzea ilivyotokea na tiba nilizotumia
huwezi amini alinipa tiba ya Ajabu halafu haikuwa na gharama yoyote.
Aliniambia nitafute mti wa Mlonge,nichimbe mzizi wake mpka nipate Mzizi mkubwa kisha niukate,halafu niumenye mfano wa mtu anavyo menya Mhogo kisha yale magamba yake niyatwangwe kwenye kinu kidogo,kisha zile kambakamba zake nizungushie kwenye goti na kuufunga na gripe bandage mpka mwisho,ila nikifike mwisho wa bandage nifungue na nitakuwa nimepona kabisa.
Nilifanya hivyo na cha ajabu nilivyo kuwa nafunga hiyo bandage niliona mguuu kama unawaka moto,na nilipofika mwisho wa kujifunga nikaanza kufungua kama alivyo agiza na Mguuu alikuwa umepona kabisa kiasi cha kuwafanya watu waliokuwa wanaona ninachofanya kushangaa na wengine kutoaamini.
Toka siku hiyo mimi ni mzima hadi leo imeshapita zaidi ya miaka 22 mi nipo salama kabisa.
Naomba ujaribu kufanya hivyo ndugu inaweza kukusaidia maana hata nilipokuwa JKT wenzangu wengi niliwaeleza kuhusu tiba hiyo na waliweza pona kabisa ANKLE na MAGOTI.
POLE SANA NAOMBA KAMA HUJALI JARIBU HIYO TIBA.
mti wa mlonge ukoje na unapatikana wapi?
 
Ahsante kwa maelezo kwani kusaidia ni moyo na si kama waganga wa kienyeji wanaokana hata kama kitu kinajulikana kwa wote
 
jaman kuna ndugu yangu anavimba miguu na uso na mikono na miguu ufa ganzi na anaweza kupitisha cku nzima bila kukojoa
 
Aisee, hizo ni dalili za renal failure(figo kushindwa kufanya kazi)....... aende hospitali haraka kwa madaktari..... its important awahi kwenda mkuu
 
Ma Dr WA humu JF naomba msaada kwa anae fahamu hili tatizo na ufumbuzi wake. Asanteni.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Habari jf doctor,

Naomba kuuliza, hivi kuvimba miguu kwa wajawazito inatokana na nini??? Hasa kwenye miezi ya 4-6. Je huwa kuna tatizo ama ni kawaida???

Dr. MziziMkavu, Dr. HIPPOcratesocrates na wengineo naomba msaada wenu!

Asante
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom