Tatizo la Kuvimba Miguu: Chanzo, Ushauri, dawa na tahadhari (pamoja na wajawazito) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la Kuvimba Miguu: Chanzo, Ushauri, dawa na tahadhari (pamoja na wajawazito)

Discussion in 'JF Doctor' started by Dadii, Apr 20, 2011.

 1. Dadii

  Dadii Senior Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 142
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Habari zenu wapendwa, mimi nina matatizo ya mguu wangu wa kushoto kuvimba kwenye kifundo juu ya kisigino ( ANKLE) nimejaribu kutumia dawa za hospitalini na hata za mitishamba lakini bado sujapata nafuu.

  Wakati mwingine unanyweaa,na wakati mwingine unajaa, nahisi maumivu mpaka kwenye goti na kwenye nyonga.

  Nilienda Aga Khan nikapewa dawa mara 2 amabazo zinacost laki 180,000 wakidai kuwa cells za maeneo hay ya mguu zimekuwa leakage (worn out).

  Nimemaliza dawa natakiwa nifuate zingine, lakini bado hazijanipa tija na doctor amesema nikimaliza nifuate. lakini alishangaa kwanini sijapona kwa ile dose ya kwanza.

  Tafadhari wandugu mwenye aidea ya dawa ya haya maumivu (ugonjwa) msaada tafadhari, tatizo ni la muda wa miaka 3 nyuma.

  Natanguliza shukrani za dhati kwa msaada wenu, Mungu awabariki sana.

  NIlishapiga X-ray hakuna tatizo, nlishapima vipimo pale Muhimbili kuangalia kama tatizo matende au bacteria wowote au fungas hawakuona chochote.

  Nilisha check blood kama kuna tatizo lolote lakini hatukuapta chochote, full blood picture hatukupata dalili za ugonjwa wowote.

  Ila tatizo au history ya ugonjwa ulianza kuvimba kwa mguu bila kuumia, kujikwa wala kuteuka.

  Akhsante wana jamii, kwa msaada wenu.
  =============
  Tatizo linalorandana na la juu:
  =============
  Kwa wajawazito:
  Ushauri kwa mhusika juu:
   
 2. U

  Upanga Senior Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 135
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Hello!Bwana mimi nilishawahi umia GOTI nilipokuwa kidato cha pili nikiwa timu ya shule pale TAMBAZA Sec miaka hiyo!

  Nilihangaika na huo mguu kwa zaidi ya mwaka na nusu nikiwa nimepelekwa hospital mbalimbali bila kupona.

  Kuna siku moja nikiwa nimekaa nyumbani barazani kwa nyumba za National Housing pale Magomeni,alipita BIBI Mmoja ambaye simfahamu alisimama na kuniangalia jinsi mguu ulivyojaaa na kuniuliza nilifanya nini mpaka mguuu ukawa hivyo!!!!Nilimuelzea ilivyotokea na tiba nilizotumia; huwezi amini alinipa tiba ya Ajabu halafu haikuwa na gharama yoyote.

  Aliniambia nitafute mti wa Mlonge,nichimbe mzizi wake mpka nipate Mzizi mkubwa kisha niukate, halafu niumenye mfano wa mtu anavyo menya Mhogo kisha yale magamba yake niyatwangwe kwenye kinu kidogo,kisha zile kambakamba zake nizungushie kwenye goti na kuufunga na gripe bandage mpka mwisho, ila nikifike mwisho wa bandage nifungue na nitakuwa nimepona kabisa.

  Nilifanya hivyo na cha ajabu nilivyo kuwa nafunga hiyo bandage niliona mguuu kama unawaka moto,na nilipofika mwisho wa kujifunga nikaanza kufungua kama alivyo agiza na Mguuu alikuwa umepona kabisa kiasi cha kuwafanya watu waliokuwa wanaona ninachofanya kushangaa na wengine kutoaamini.

  Toka siku hiyo mimi ni mzima hadi leo imeshapita zaidi ya miaka 22 mi nipo salama kabisa.

  Naomba ujaribu kufanya hivyo ndugu inaweza kukusaidia maana hata nilipokuwa JKT wenzangu wengi niliwaeleza kuhusu tiba hiyo na waliweza pona kabisa ANKLE na MAGOTI.

  POLE SANA NAOMBA KAMA HUJALI JARIBU HIYO TIBA.
   
 3. Wit

  Wit JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 417
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu Upanga heshima kwako, asante kwa hiyo tiba lkn bado nina swali dogo,hii dawa unaweza kutumia sehemu yeyote iliyoshtuka kny mguu au ni mpaka iwe enka?je,hapo uliposema kufunga na bandage unaacha walau dk chache au ni kitendo cha kufika mwisho tu na kutoa?asante sana nitajaribu naamini nitasaidika pia
   
 4. U

  Upanga Senior Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 135
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Kwa jinsi nilielewa mimi ni sehemu ya uvimbe hususa GOTI na ANKLE si unajuwa huwa ni tofauti na uvimbe wa kupigwa rungu!
  Kwa vile sikupata muda wa kumuhoji yule BIBI mimi nilikimbilia kuufuata ule mti na kuutumia kwenye magoti na Ankle,kuhusu kuacha kidogo au kufungua mara tu ukifika mwisho,jibu lake ni kwamba utasikia moto mkali utakaokufanya ifike tuuu mwisho wa bandage kwa sababu huta tamani
  hiyo bandage ikae hapo hata dak mbili hivyo utafungua mara tuuu ukimaliza funga.
   
 5. Dadii

  Dadii Senior Member

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 142
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Akhsante mkuu Upanga je huu mti wa mlonge naweza kuupata maeneo gani? ili hilo zoezi lianze mara moja maana nishataabika sana mkuu Upanga. Ubarikiwe.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. N

  Nsagali Member

  #6
  Sep 21, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wanandg wa JF nilikuwa napenda kujua tatizo ambalo linawapata akina mama wengi kuvimba miguu wakati mjamzito huwa ni ugonjwa au ni kawaida lazima avimba miguu na usababishwa na nini
   
 7. Wang'wise

  Wang'wise JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 273
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Una sababishwa na ujauzito
   
 8. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kula vyakula vyenye chumvi nyingi..
   
 9. Kwetu Iringa

  Kwetu Iringa JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 359
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kuna sababu 2 kuu:
  • Mimba inazuia damu na lymph visipande kutoka miguuni kwenda kwenye moyo kupitia veins
  • Ugonjwa kama high blood pressure
  Wengine wasaidie
   
 10. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nsagali, ni kweli kwamba akina mama wengi huwa wanapata matatizo ya kuvimba miguu wakati wa ujauzito. Wengi wa hao ni kawaida katika maana ya kwamba haisababishwi na ugonjwa wa aina yoyote.

  Wakati mimba inapokuwa kubwa huweza, tumbo la uzazi (uterus) hukandamiza mishipa ya damu inayorudisha damu kwenye moyo (veins) au ile mishipa inayobeba maji damu (lymph) kutoka kwenye miguu, hii hufanya damu na hayo maji damu kushindwa kurudi yote kwenye moyo na kujikusanya sehemu ambazo ni dependent hasa miguuni na kusababisha uvimbaji wa miguu (dependent oedema). uvimbaji huu ni ule ambao sana uko kwenye sehemu ya mguu chini kifundo cha mguu (ankle oedema), kama miguu ikivimba kupanda juu hadi kwenye mapaja au juu zaidi hii huwa ni dalili ya ugonjwa.

  Magonjwa ambayo yanaweza kusababisha uvimbe miguuni na sehemu nyingine za mwili wa mama mjamzito ni pamoja na:-
  1. shinikizo la damu la ujauzito (pre-eclampsia).
  2. magonjwa ya figo - hii mtu huvimba, pamoja na miguu, uso pia.
  3. magojwa ya ini - haya husababisha pia maji kujaa kwenye ukuta wa mbele wa tumbo (ascites) lakini pia mwili wote waweza kuvimba
  4. Ukosefu wa protein kwenye damu (hypoproteinaemia kwa sababu yoyote).
  5. Ugonjwa wa moyo (heart failure) n.k.
  Ni vizuri mama anapovimba miguu aende hospitali kwa ajili ya uchunguzi, atatibiwa kulingana na tatizo litakalogundulika.

  kama ni ile dependent edema, anachotakiwa ni kutosimama kwa muda mrefu na hata akikaa awe ana'elevate' miguu asiining'inize, pia wakati wa kulala asipende kulalia mgongo (yaani kichalichali - supine) kwani hii husababisha mfuko wa uzazi (uterus) kukandamiza hiyo mishipa ya damu na kusababisha uvimbe miguuni kama nilivyoeleza juu.

  Natumaini nimekusaidia mkuu. Wengine karibuni.
   
 11. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160


  Asanta sana dokta
   
 12. N

  Nsagali Member

  #12
  Sep 22, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante kwa msaada wako ndg
   
 13. Loyal_Merchant

  Loyal_Merchant JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 589
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mama yangu anaumwa na miguu hali ambayo imepelekea miguu yake kuvimba katika joints za visigino/ enka na pindi uibonyezapo inaacha vishimo mahala palipobonyezwa.

  Ameenda hospitali na kupimwa sukari na BP na kukutwa vipo kawaida. wakampa dozi ya vidonge atumie kwa siku 30 na kumwambia arudi baada ya kumaliza. Zimebaki siku 4 amalize dozi lakini hali ipo palepale. Je, tatizo laweza kuwa nini?

  Madaktari naombeni msaada.
   
 14. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #14
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ....Je mama ni mtu mzima sana au!! Babu yangu (R.I.P) alikuwa na tatizo kama hilo, lakini yeye alikuwa na miaka 82, figo zake zilikuwa na matatizo. Miguu ilikuwa inabonyea, mwishoni ikawa inatoa maji. Mama atapona tu, mpe pole.
   
 15. Loyal_Merchant

  Loyal_Merchant JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 589
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  si mtu mzima sana, ana miaka 45. kwa hiyo unaniambia atapona tu bila kutumia dawa yoyote?
   
 16. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Ameshawahi kucheki figo?mara nyingi huchangia tatizo kama hilo
   
 17. n

  ngwana ongwa doi Member

  #17
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Matatizo yanayosababisha miguu kuvimba yako mengi kama matatizo ya figo,magonjwa ya moyo,upungufu wa damu,matatizo ya damu kuganda,overweight, nk.Kujua nini kinamsababishia hali hiyo ni ngumu mpaka hosp.may be kama hawaja check figo,moyo,wingi wa damu waangalie inaweza kuwa ndiyo cause.

  Pia afanye mazoezi ya kutembea tembea kwani kukaa muda mrefu miguu huzidi kuvimba,akiwa amekaa weka kitu miguu iwe juu kuzidi level ya moyo ulipo,punguza chunvi kwenye vyakula.

  Matibabu yatategemea cause ya tatizo mrudi hosp.
   
 18. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135

  .......I mean atapona kwa kutumia dawa, vile vile mjaribu kwenda hospital ya agha khan mama apate kipimo kinachopima viungo vyote vya mwili, hapo tatizo litagundulika kwa urahisi.

  Nimewafahamu watu kadhaa nao walikuwa wanaumwa umwa na kupewa vidonge na hawakupona..........lakini baada ya kupata kipimo hicho wakagundua ugonjwa mapema na kutatua tatizo.
   
 19. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #19
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Pole sana. Hebu google edema uone visababishi. Miguu inabonyea kama papai bivu kwa sababu maji yanasambaa na hayasafirishwi ipasavyo. Mtafutie daktari wa moyo.
   
 20. Loyal_Merchant

  Loyal_Merchant JF-Expert Member

  #20
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 589
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  thanx wote kwa ushauri mlionipa, hyo tarehe 4 baada ya dozi alopewa kuisha tutarudi tena hospitali na kufanya uchunguzi zaidi juu ya tatizo lake.
   
Loading...