Tatizo la kuuma kwa visigino | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la kuuma kwa visigino

Discussion in 'JF Doctor' started by ggg, Nov 5, 2010.

 1. ggg

  ggg Member

  #1
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanajamii, naomba mnisaidie kama kuna mtu anafaham wapi ninaweza kupata tiba au tiba ya hili tatizo


  mama yangu akitembea, visigino umuuma, na akikaa vinauma kwa ku''pwita", alikwenda hospital akambiwa kuwa ni mnene sana, so apunguze uzito kwa kufanya mazoezi. lakin mpaka sasa hali ni mbaya, kwani anashindwa hata kutembea.jamani kama kuna msaada mwingine ninaweza kuupata naomba mnisaidie. ana uzito wa kilogram 90, umri ni miaka 46 na urefu wa mita 1.5
   
 2. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kuna kipimio cha kuongoza uzito mzuri kiafya mtu kuwa nao kinaitwa BMI (Body Mass Index). BMI inakokotolewa kutumia uzito (kilo) na urefu wa mtu (meta). BMI = Uzito/kimo/kimo (uzito gawa kwa kimo gawanya tena kwa kimo).

  Mwongozo
  BMI 25 au pungufu - safi
  BMI 25 - 30 - overweight
  BMI zaidi ya 30 - Obese

  Ukikokotoa takwimu za mama yako ulizotoa utapata BMI ya 40, yaani ni obese. kwa hakika uzito wake ni mkubwa mno na ndiyo maana hospitali wakashauri kuupunguza. Kwake BMI ya 25 inadai kilo pungufu ya 58. Lakini kupungua kokote kutamfaa.

  Kasheshe ni namna ya kupunguza - wengi tu tunapata tabu sana na suala hili, mimi nikiwa moja wapo.

  Natumaini nimeeleweka na angallau kwa kiwango fulani nimesaidia.
   
 3. r

  rmb JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  umesomeka vizuri mdau! tatizo kubwa ni mazoezi na vyakula tunavyotumia
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kuhusu matatizo ya mama yako kuuma visigino nakushauri mwambie apake kwenye hivyo visigino vya unyayoni apake hina itamsaidia kuondosha maumivu. kuhusu Unene alionaoa Mama mwambia apate Asali mbichi,Maji ya Uvuguvugu glasi moja na siki ya Apple. Matumizi chukuwa kijiko

  kimoja cha asali na kijiko kimoja cha hiyo siki ya apple changanya na maji ya uvuguvugu Glasi moja . kila anapokula chakula mwambie awe anakunywa hiyo dawa pamoja na chakula tonge chakula pamoja na kunya hiyo dawa kidogo kidogo mpaka anapomaliza chakula awe amalize na hiyo dawa akitumia hiyo dawa kwa muda wa miezi 3 basi atapunguwa huo unene wake.
   
Loading...