Tatizo la kutopata ujauzito kwa mwanamke chanzo kikiwa kwa mwanaume tiba yake ipo?

lee van cliff

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,809
2,000
Habari wapendwa mabibi na mabwana. Habari za kazi Madaktari na Wauguzi
Kwa miaka nenda miaka rudi wanawake wasipopata ujauzito, lawama zote wamekua wakitupiwa wao.

Hi ni mbaya Sana kwa sababu Mara nyingine tatizo huwa liko kwa mwanaume.
Uchunguzi wa wataalamu ulikuja kubaini kuwa hata mwanaume anaweza kuwa sehemu ya tatizo.

Sasa swali langu linatokana na Mimi mwenyewe kua ndio muhanga. Bila kuficha Wala kudanganya Nina watoto wawili nataka mtoto wa tatu na baadae wa nne tumeshindwa kumpata. Kwa ushirikiano na uwazi kabisa tumeenda wote kupima tatizo pimeonekana upande wangu.

Maswali:
Je, kwa mwanaume kutokuweza kuingiza mimba matibabu yapo? Kwa sababu siku zote tunasikia matibabu ni kwa mwanamke tu.

Nina watoto wawili, sina shaka nao, ukiwaona hata bila kuuliza ni photocopy yangu kwa sura, kuongea, tabia na matendo.

Je, ni nini kilichosababisha nipate tatizo la kutokutia mimba ya tatu. Kwa watoto hao wawili sina shaka na mzazi mwenzangu. Uhakika ni 100 asilimia.

Naomba kujua kama matibabu yapo kwa tatizo la mwanaume kutokuweza kutia mimba.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
5,884
2,000
Anatoa tiba ya uhakika au ndo biashara...ebu wale walienda kwake wakafanikiwa waje watoe ushuhuda.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nina rafiki yangu alikuwa na tatizo kwa muda mrefu la kutotia mimba wanawake akaenda kwa Dokta Ndodi akapewa madawa akatumia.

Sasa hivi ana watoto wawili. Ila anasema dawa zao zina gharama sana kuliko hata za hospitali, laki tano tano au laki saba saba zitakutoka mara kadhaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom