Tatizo la kutokwa na uchafu ukeni- Pata ufafanuzi wa kina, ushauri na tiba ya tatizo hili

KingPin

Member
Jul 21, 2009
11
3
1589103759465.png
UFAFANUZI WA JUMLA WA TATIZO HILI
Hakika mapenzi ni matamu hakuna asiyelifahamu hili na mapenzi kwa kawaida hushirikisha vishiriki ngono kama kupapasana, kubusiana na hata mambo fulani ya kula koni na kuzama chumvini. Hakika uke ni sehemu muhimu sana ya mwanamke inayoweza kuamsha hisia za mwanamme wake ama kuzipoteza, kumthaminisha ama kumshusha thamani endapo mwanamke atashindwa kujiweka katika hali ya usafi ama kukabiliana na matatizo ya kutokwa na uchafu ukeni. Hivyo kwa kutambua hili leo nimeamua kuandika mada hii ili kuwasaidia wale wote wenye tatizo kama hili.

Kimsingi wanawake wote hutokwa na uchafu kidogo ukeni ambao ni mweusi kama maji, maziwa au njano ambao humfanya ama awashe au atowe harufu mbaya pale anaposhindwa kukabiliana na hali ya usafi wake. Hata hivyo, wanawake wengi kipindi cha ujauzito hukumbwa na hali hii mara kwa mara na huwashwa. Uchafu husababishwa na mambo mbalimbali ambapo mengi husumbua japo si hatari. Zifuatazo ni aina za uchafu ambao wengi huwakumba na jinsi unavyoweza kukabiliana na tatizo hilo.

Mwanamke aliye na tatizo la kutokwa na aina hii ya uchafu hujikuta ananuka na kujikuna sehemu zake za siri, na huu unawezekana kuwa ni ugongwa wa Trichomos kwani pindi anaposikia haja ndogo hujisikia kuchomwa sana na maumivu ambapo wakati mwingine hujikuta anavimba.

Uchafu wa aina hii huonekana kama picha kushoto inavyoonyesha hivyo mwanamke ambaye atakumbwa na tatizo kama hili ni rahisi kumfanya mpenzi wake apoteze hamu ya kushiriki naye tendo la ndoa na kama ni mpenzi basi huweza kujikuta kila kukicha anashindwa kudumu na mwanaume kwani hukimbiwa kutokana na kushindwa kwao kukabiriana na tatizo hilo.

Endapo una tatizo hili ni muhimu sana kuhakikisha unaweka viungo vya uke wako katika hali ya usafi wa kutosha, na ni vema unaposafisha uke wako uhakikishe unatumia maji ya uvuguvugu pamoja na siki au maji la limao yaliyochanganywa na maji ambapo unapaswa kutumia vijiko 3 vya siki kwenye maji lita moja yaliyochemshwa. Ni muhimu mgojwa asafishe uke wake mara moja hadi tatu kila siku mpaka apone!

Hata hivyi endapo tatizo hilo linakuwa kubwa, mgonjwa anapaswa kutumia dawa za kuchomeka ukeni ambazo zina metronidazole au dawa zingine zinazoshauriwa na trichomonas. Ikiwa hali mbaya sana anapaswa kumeza metronidazole kwa kiasi cha gram mbili [meza kwa mpigo].

Aidha, inawezekana kuwa mwanaume ana ugonjwa pia wa trichomonas ingawa hajisikii hali ya kuumwa hata kidogo hivyo endaapo mwanamke atarudiwa na ugonjwa huu mara baad a ya kujitibu basi anapaswa kurudia kumeza gram mbili za metronidazole, lakini ni kama ugonjwa huo mkubwa.

Hali hii inapojitokeza kwa mwanamke hujikuta anawashwa sana ukeni na midomo ya uke huwa na rangi nyekundu na huuma sana ambapo pindi mhusika napotaka kukojoa husikia maumivu makali sana. Hali hii huwakumba sana wanawake wajawazito pamoja na wale wenye ugonjwa wa kisukari, wale waliokuwa wakitumia antibiotics au vidonge vya kuzuia ujauzito.

Endapo una tatizo hili ni muhimu sana kuhakikisha unaweka viungo vya uke wako katika hali ya usafi wa kutosha, na ni vema unaposafisha uke wako uhakikishe unatumia maji pamoja na sikiau GV vijiko viwili kwa nusu lita au kutumia vidonge viwili vya nystatin vya kuchomeka ukeni au dawa nyingine ya thrush kama siyo kuweka maziwa mgando yaliyochachuka kwenye uke husemakana ni dawa nzuri ya kienyeji inayotibu tatizo hili.

Aina za uchafu wa ukeni usio wa kawaida
Kikawaida uke wa mwanamke una bacteria wa kawaida wazuri waishio katika tunda hilo kwa ajili ya ulinzi.

Kitu chochote kitakacho haribu uwiano wa bacteria wa kawaida waishio katika uke kinaweza kuleta mabadiliko katika rangi,Harufu, au muundo wa uchafu utakaotoka katika uke.

Uchafu wenye damu au rangi ya kahawia
Hi ni dalili ya mzunguko wa mwezi wa mwanamke uliovurugika na Mara chache ni dalili ya cancer ya servix au aina nyingine ya cancer iitwayo endometrial cancer. Mwanamke mwenye tatizo hili atatoa damu nyingi uken na kuumwa nyonga.

Uchafu wa njano au kijani wenye harufu mbaya
Endapo uchafu ukatoka kama mapovu,wenye rangi ya kijani au njano ukiambatana na harufu mbaya ,Hi ni dalili ya Trichomoniasis .Maambukizo ya (parasitic) yanayotokana na Ngono zembe.dalili ingine ni kuwashwa wakati wa kutoa haja ndogo.

Uchafu mweupe ,wa njano au kijivu wenye harufu ya samaki
Uchafu wa aina hii ni dalili ya maambukizi ya bacteria (vaginosis) .Mwanamke mwenye tatizo hili atasikia miwasho au maumivu ,kuvimba kwa uke au sehemu ya nje ya uke (vulva)

Uchafu wenye rangi ya mawingu au njano
Hi ni dalili ya ugonjwa wa kisonono (Gonerhea) mwanamke atatokwa na damu katikati ya Siku zake, Atatokwa na mkojo bila kukusudia na kupata maumivu ya nyonga.

Uchafu mweupe mzito kama jibini
Hi ni dalili ya maambukizi ya aina ya fungas (yeast infection)
Na dalili zingine atakazozisikia mwanamke huyu ni kuvimba na maumivu kwenye sehemu za nje za siri (vulva) Kuwashwa na maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa
===
BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA KUHUSU TATIZO HILI

Kuna binti mrembo wa haja maringo meeeeeeengi.

Baada ya kumpigia misele sana, alikubali. Siku ya kwenda kula tunda la mti wa kati nilihisi kutapika! Baada ya kuwasha gari kama dakika 5 hivi, ulianza kutoka utando mweupe kama vile mtoto mchange amecheua au matapishi ya kuvimbiwa "maziwa mgando".

Huo uchafu ulikuwa unanuka (harufu mbaya). Yeye alidai kwamba alikuwa hajapata hiyo kitu siku nyingi sana.

Nilipokutana naye baada ya siku kadhaa, hali ya uchafu ni ule ule!

Kuna jamaa wameniambia inawezekana huyo shi anatumia panadol wakati wa siku zake. Nilipomuuliza binti amekataa matumizi ya panadol.

Kwasasa huo uchafu haunuki ila upo!!

Hii kitu inasababishwa na nini?
---
Kuna dem nimekutana nae siku zake za hatari lakin leo siku anatokwa na damu kidogo imechanganyikana na uchafu jeh tatizo nini kwake.

Ameblid tareh 19 mwez uliopita mpaka 21 ...
Nimesex nae siku yake ya 12 ambayo ni tarehe 30 mwezi uliopita... tukaendelea

Tukapiga show siku yake ya 14 na 16 ambayo ni jana...

Lakini jana ameshinda anakojoa tu pia kuna vdamu ametokwa mpaka leo asubui.

Damu inayotoka ni sio kali ni vidogo dogo na uchafu kama rangi ya shahawa.

Nikaamua nije kuomba ushauri humu jf wadau minisaidie mawazo

Pia analalamika akiinama anahisi kibofu kinajibana .

Ushauri wenu wadau

Pia mwez uliopita alitumia dawa ya clomitab.

Sent using Jamii Forums mobile app
===
MAONI, UFAFANUZI NA USHAURI KUTOKA KWA WADAU

Hili tatizo la kutokwa na uchafu unaotoa harufu mbaya sehemu za siri. Kitaalamu hali ya mwanamke kutokwa na majimaji (vaginal fluids) yenye rangi nyeupe au ya njano, ni hali ya kawaida na wala siyo tatizo endapo majimaji hayo siyo mazito sana na wala hayatoi harufu mbaya.

Lakini endapo majimaji yanayotoka yapo katika hali ya ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia, yanatoa harufu kali na yanawasha, basi hiyo ni ishara ya ugonjwa uitwao Vaginosis.

Majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia inayowezesha viungo vya uzazi vya mwanamke kujisafisha na kuutoa uchafu wa seli zilizokufa na mabaki ya damu ya hedhi nje ya mwili.

Pia huvikinga viungo vya uzazi dhidi ya maambukizi ya bakteria au fangasi wanaosababisha magonjwa. Kwa kawaida huwa hayatoi harufu na huwa na rangi nyeupe au ya njano. Pia huwa na asidi ya Lactic ambayo huzuia kuzaliana kwa vijidudu vya maradhi na huzalishwa kwenye tezi za Bartholin (Bartholin’s glands) zilizopo kwenye shingo ya mlango wa uzazi (Cervix).

Kwa kawaida, mwanamke hutoa kiasi cha gramu 2 za seli zilizokufa kutoka kwenye mji wa uzazi na gramu 3 za ute mwepesi kila siku.

Kiwango hiki huweza kuongezeka au kupungua kutegemeana na mzunguko wa hedhi. Kuna wakati ute huwa mwepesi na unaovutika (kama ute wa yai la kuku) na kuna wakati huwa mzito kiasi na wenye rangi ya njano. Ute huu ni wa kawaida na huwatoka wanawake wote hususan baada ya kuvunja ungo.

Sababu za kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya sehemu za siri
Kuna sababu nyingi ambazo husababisha mwanamke kutoa ute au majimaji yasiyo ya kawaida kutoka kwenye sehemu zake za siri.

- Maambukizi ya bakteria wanaosababisha
magonjwa kama Trichomoniasis, Candidiasis, Gonorrhea
Candida albicans, chlamydia
Hayo yote huweza kusababisha mwanamke kutokwa na uchafu unaoambatana na harufu mbaya.

- Pia mabaki ya vitambaa, tishu au pedi ambazo hazikutolewa wakati wa hedhi huweza kusababisha tatizo hili.

- Usafi wa sehemu za siri usipozingatiwa hususanimwanamke anapokuwa kwenye siku zake za hedhi, huweza kuwa mazalia mazuri ya bakteria wanaosababisha harufu mbaya.

Dalili za ugonjwa wa kutokwa na uchafu ukeni (VAGINOSIS)

Mwanamke mwenye tatizo la Vaginosis huwa na dalili kubwa ya kutokwa na ute na majimaji yasiyo ya kawaida (uchafu) kutoka sehemu za siri.

1. Uchafu huu huwa unatoa harufu kali kama shombo ya samaki au kitu kilichooza na huambatana na maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu.

2. Wakati mwingine uchafu wenye rangi kama ya kijani hutoka.

3. Kuwashwa na kuchomachoma sehemu za siri, mgonjwa asipopatiwa tiba haraka husababisha vidonda sehemu za siri.

4. Mwanamke anapoona anatokwa na ute uliochanganyikana na damu hata kama hayupo kwenye siku zake, hii ni dalili nyingine ya Vaginosis.

5. Maumivu makali wakati wa tendo pia ni dalili za ugonjwa huu.

MATIBABU
Tatizo hili hutibika hospitalini baada ya vipimo vya kitaalamu kuchukuliwa na daktari mwenye uzoefu wa kutosha juu ya magonjwa ya wanawake.

Dawa za kupaka (Ointment/ Cream) na dawa za kumeza (Pills) huweza kutumika kutubu tatuzo hili.

Kumbuka: Ni makosa kutumia dawa bila kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari.
Pia inatakiwa ufike katika kituo chochote cha afya pindi unapohisi unatatizo ili kufanyiwa vipimo na kupatiwa matibabu stahiki kulingana na tatizo litakalokuwa linakusumbua

View attachment 1371492

Karibu tujifunze na
Dr Sylvester John
Tel. No. 0753 518513
Email: johnsylvester022@gmail.com
---
HALI/ MAZINGIRA YA UTE.
UTE UKIWA MKAVU AU UNANATA;

aina ya ute kama huu hauruhusu mbegu za kiume kusafiri na kuingia katika kizazi cha mwanamke hivyo mimba haiwezi kutungwa hapa, Huu ute huwepo mwanamke akiwa hayupo katika kipindi cha joto au kipindi ambacho yai yake bado halijapevuka.

UTE UKIWA NA RANGI YA KRIMU (Cream)
hapo mwanamke anakaribia kuingia katika kipindi cha joto pia yai linakaribia kupevuka bado hawezi kupata mimba.

UTE UKIWA MAJIMAJI AU YENYE UNYEVU UNYEVU;
huu unaweza kusafirisha mbegu ya mwanaume hadi kizazi cha mwanamke na kama imebaki siku mbili au tatu yai kupevuka ukifanya tendo la ndoa hapa kuna uwezo utashika mimba kwa sababu yai likipevuka litakutana na mbegu ya mwanaume ndani ya kizazi kuna uwezo mimba itatungwa. Mwanamke hupata hisia za kufanya mapenzi lakini siyo sana

UTE UKIWA NA RANGI NYEUPE KAMA YAI BICHI;
ute ukiwa katika hali hii ndiyo mzuri kabisaa kwa kusafirisha mbegu za kiume, pia hapa mwanamke ameshafika katika kipindi cha joto hapa tendo la ndoa likifanyika mimba inapatikana kwa asilimia zote kama hakuna vizuizi kutoka Mungu muumba na vizuizi vingine vya afya vinavyozuia mimba kutunga.

Hapa hisia za mwanamke za kufanya tendo la ndoa huwa juu sana na hutamani kufanya mapenzi kila mara especially yai likikaribia kushuka na likishuka.

Ni muhimu sana mwanamke aangalie ute (vaginal mucus) katika kuzifahamu siku zake za kuweza kushika mimba na kutoshika mimba kuliko kutumia calendar ya damu ya mwezi.
Siku za ute ni siku 30 kinyume na siku za damu ya mwezi na pia ni muhimu sana mwanamke kushika ule ute kila siku kwa mkono wake kuangalia rangi na utelezi na harufu.

kwa kiswahili rahisi kabisa
---
KUTOKWA NA UCHAFU UKENI PART 2

Uchafu mzito ulio kama maziwa na wenye harufu mbaya
Huu unawezekana kuwa ugonjwa [uke huwa kama picha inavyoonyesha]unaosababishwa na chembechembe ambazo huitwa haemophilus. Uchunguzi maalum unahitajika ili kupambanua ugonjwa huu na trichomonas. Safisha uke kwa siki na maji kama nilivyosema katika sehemu ya kwanza ya mada hii, lakini unapaswa pia kutumia vidonge vyakuchomeka kwenye uke vya sulphathiazole mara mbili kutwa kwa wiki 2.

Ugonjwa huu unapompata mwanamke kwanza kabisa hukosa amani hata ya kukutana na mwenza wake na hasa kama mwenza huyo ni mtundu katika mambo fulani ya vishirikishi ngono yaani halianzishi hadi apime oil na kuzama chumvini. Hivyo mwanamke yoyote mwenye tatizo hili ni vema asilipuuziye kwa kuamua kushiriki tendo bila kupata tiba hata kama utajisafi vipi.

Uchafu wa majimaji mweusi au rangi ya kijivujivu ambao una damu na harufu mbaya
Mwanamke mwenye ugonjwa huu huwa amefikia hatua mbaya zaidi kwani yawezekana tayari kansa ikawa imeshamtafuna katika maumbile yake ya uke. Hata hivyo kansa sehemu za uke mara nyingi huwapata wanawake walio na umri zaidi ya miaka 40, na dalili ya kwanza inaweza kuwa ni upungufu wa damu mwilini au kutumia hedhi isiyo ya kawaida na kujisikia uzito au kuona uvimbe wenye maumivu katika kinena [kama una hali hii nenda kamuone daktari haraka].

Ugonjwa huu pia huambatani ambapo mtu akipatwa na homa anaweza nkunjwa dawa za kuua vijidudu au kumuona dk.

KIMSINGI: mwanamke yoyote yule ambaye anasumbuliwa na uchafu wa muda mrefu na hata akiutibu haupunguwei licha ya kufanya matibabu ya awali kama nilivyobaibisha hapo juu anapaswa kwenda kumuona daktari.

MUHIMU!

Mwanamke yoyote yule anaweza kuepuka magonjwa mengi ya ukeni endapo atafanya haya yafuatayo:-

Kuweka viungo vya uke wake katika hali ya usafi.
Mwanamke wakati anaogo anatakiwa kuhakikisha anasafisha vema uke wake kwa kutumia maji na sabubi na si kupuuzia kwa kujipapasa tu maana kuna wengine hujifanya kuona kinyaa yaani ataoga kote kisha huko anapanguza na toilet pepar kisha biashara imeisha hii ni mbaya, hivyo hata kama ukiwa kwenye baridi ama ukame wa maji hakikisha hulali bila kusafisha uke wako!

Kojoa baada ya kukutana na mwanaume
Hii ni kwa wale ndugu zangu wanaokwenda uwanja wa taifa kucheza mechi na kushuka dimbani pasipo kuwa na jezi yaani wao ni peku peku sasa wengine wakimalzia tu mechi huinuka kisha kujifuta na toilet paper na kujisafisha kidogo kisha hao wanakamata chupi na kuvaa huku akisindikiza na katoilet peapr chini yaani anaiweka kama vile awekavyo pedi, sasa hii ni hatari kwa majongwa kama niliyoyaeleza kwenye mada zangu.

Hakikisha umejipangusa au kujitawaza vizuri baada ya kwenda choo.
Mwanamke naamini anajua jinsi ya kujisafisha kwani zoezi hili hufundishwa tangu wakiwa wadogo lakini kama haujui ni vema ukajiswafi yaani kujipangusa kutoka mbele kwenda nyuma kwani kujipangusa kwa kwenda mbele husababisha mikroba, ameba au minyoo kwenye uke.Mashosti: KUTOKWA NA UCHAFU UKENI PART II
---
KILA MWANAMKE AJICHUNGUZE MAENEO YAKE YA UZAZI.

Kila mwanamke anapaswa ajichunguze Kila siku maeneo yake ya uzazi.
Vile vile kuchunguza nguo zako za ndani unapokuwa unaivua siku hiyo Kama Kuna uchafu wowote.

kufanya hivyo kunaweza kumsaidia kugundua kusa anatatizo kiafya.Nasema hivi kwani wapo baadhi ambao hawafahamu kuwa Kila siku uwapo Ute Ute unaomtoka ni hali ya kawaida

Ute wa rangi nyeupe ya kahawia Kama chai isiyokolea rangi na huwa hauna harufu mbaya.

Ute huo ni moja ya njia ya uke hujisafisha pamoja na taka za hedhi taka za mwili zilizotoka nje.

Ute huo huzalishwa na kuta za nyumba ya uzazi na kuzifanya tezi za uke kushuka chini kutokana na kani nguvu ya mvutano(gravity)

IKUMBUKWE UTE HUU NI SALAMA KWA MWANAMKE

kutokwa na uchafu mweupe au wakijivu uliokama maziwa ya mgando ni dalili za ugonjwa was fangasi(vaginal candidiasis)

DALILI ZAKE
miwasho ndani na nje ya uke.
kupata hisia za kuwaka Moto wakati wa kukojoa wakati wa kujamiiana na kuvimba ukeni
tishu za uke kuwa nyukundu
kutoka vipele au vidonda ukeni
inakadiliwa wanawake katika maisha ya Kila siku wanahistoria ya huu ugonjwa.
IFAHAMIKE:Tatizo jipi halipo katika makundi ya maradhu yatokanayo na (STI)Ingawa kugusana kwa kujamiiana kunaweza kusambaza.

HATA WANAWAKE AMBAO HAWAJAWAHI KUSHIRIKI TENDO LA KUJAMIIANA WANAPATA HILI TATIZO
unashauriwa mwanamke kutozoea kutia kitu chochote ndani ya uke unapo kuwa unajisafisha au hata sabuni kwani unaenda kuuwa bacteria walinzi na kuruhusu fangasi kustawi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni nzuri, wakumbushe pia kutembelea madaktari wa wanawake mara kwa mara ili kupata mawili matatu kwenye nyanja nzima ya usafi wa mwili na hususani kiungo cha uzazi.

Tunakushukuru sana.
 
Hali majimaji meupe kama maziwa mgando kutoka uken husababishwa na nini? Je inaambukiza na kama ndiyo dalili zake ni zipi kwa mwanaume ? Madhara yake kwa mme na mke ni yapi na tiba yake? Naomben ufafanuz Madaktari.
 
soma post ya mzizi mkavu inahusu maambukizi ya fangus na tiba na dalili na madhara, almost everything
 
2.jpg

KUTOKWA NA UCHAFU UKENI​

Hakika mapenzi ni matamu hakuna asiyelifahamu hili na mapenzi kwa kawaida hushirikisha vishiriki ngono kama kupapasana, kubusiana na hata mambo fulani ya kula koni na kuzama chumvini. Hakika uke ni sehemu muhimu sana ya mwanamke inayoweza kuamsha hisia za mwanamme wake ama kuzipoteza,kumthaminisha ama kumshusha dhamani endapo mwanamke atashindwa kujiweka katika hali ya usafi ama kukabiliana na matatizo ya kutokwa na uchafu ukeni. Hivyop kwa kutambua hili leo nimeamua kuandika mada hii ili kuwasaidia wale wote wenye tatizo kama hili.....

Kimsingi wanawake wote hutokwa na uchafu kidogo ukeni ambao ni mweusi kama maji, maziwa au njano ambao humfanya ama awashe au atowe harufu mbaya pale anaposhindwa kukabiriana na hali ya usafi wake. Hata hivyo, wanawake wengi kipindi cha ujauzito hukumbwa na hali hii mara kwa mara na huwashwa. Uchafu husababishwa na mambo mbalimbali ambapo mengi husumbua japo si hatari. Zifuatazo ni aina za uchafu ambao wengi huwakumba na jinsi unavyoweza kukabiriana na tatizo hilo.

Uchafu wa majimaji wenye rangi mchanganyiko wa kijani na njano au nyeupe.
Mwanamke aliyena tatizo la kutokwa na aina hii ya uchafu hujikuta ananuka na kujikuna sehemu zake za siri, na huu unawezekanai kuwa ni ugongwa wa Trichomos kwani pindi anaposikia haja ndogo hujisikia kuchomwa sana na maumivu ambapo wakati mwingine hujikuta anavimba.

Uchafu wa aina hii huonekana kama picha kushoto inavyoonyesha hivyo mwanamke ambaye atakumbwa na tatizo kama hili ni rahisi kumfanya mpenzi wake apoteze hamu ya kushiriki naye tendo la ndoa na kama ni mpenzi basi huweza kujikuta kila kukicha anashindwa kudumu na mwanaume kwani hukimbiwa kutokana na kushindwa kwao kukabiriana na tatizo hilo.

Endapo una tatizo hili ni muhimu sana kuhakikisha unaweka viungo vya uke wako katika hali ya usafi wa kutosha, na ni vema unaposafisha uke wako uhakikishe unatumia majiya uvuguvugu pamoja na siki au maji la limao yaliyochanganywa na maji ambapo unapaswa kutumia vijiko 3 vya siki kwenye maji lita moja yaliyochemshwa. Ni muhimu mgojwa asafishe uke wake mara moja hadi tatu kila siku mpaka apone!

Hata hivyio endapo tatizo hilo linakuwa kubwa, mgonjwa anapaswa kutumia dawa za kuchomeka ukeni ambazo zina metronidazole au dawa zingine zinazoshauriwa na trichomonas. Ikiwa hali mbaya sana anapaswa kumeza metronidazole kwa kiasi cha gram mbili [meza kwa mpigo].
1.jpg
Aidha, inawezekana kuwa mwanaume ana ugonjwa pia wa trichomonas ingawa hajisikii hali ya kuumwa hata kidogo hivyo endaapo mwanamke atarudiwa na ugonjwa huu mara baad a ya kujitibu basi anapaswa kurudia kumeza gram mbili za metronidazole, lakini ni kama ugonjwa huo mkubwa.

Uchafu ambao uko kama jibini au siagi na unanuka kama uyoga au mkate.
Hali hii inapojitokeza kwa mwanamke hujikuta anawashwa sana ukeni na midomo ya uke huwa na rangi nyekundu na huuma sana ambapo pindi mhusika napotaka kukojoa husikia maumivu makali sana. Hali hii huwakumba sana wanawake wajawazito pamoja na wale wenye ugonjwa wa kisukari, wale waliokuwa wakitumia antibiotics au vidonge vya kuzuia ujauzito.

Endapo una tatizo hili ni muhimu sana kuhakikisha unaweka viungo vya uke wako katika hali ya usafi wa kutosha, na ni vema unaposafisha uke wako uhakikishe unatumia maji pamoja na sikiau GV vijiko viwili kwa nusu lita au kutumia vidonge viwili vya nystatin vya kuchomeka ukeni au dawa nyingine ya thrush kama siyo kuweka maziwa mgando yaliyochachuka kwenye uke husemakana ni dawa nzuri ya kienyeji inayotibu tatizo hili.

Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 
KUTOKWA NA UCHAFU UKENI PART 2

Uchafu mzito ulio kama maziwa na wenye harufu mbaya
Huu unawezekana kuwa ugonjwa [uke huwa kama picha inavyoonyesha]unaosababishwa na chembechembe ambazo huitwa haemophilus. Uchunguzi maalum unahitajika ili kupambanua ugonjwa huu na trichomonas. Safisha uke kwa siki na maji kama nilivyosema katika sehemu ya kwanza ya mada hii, lakini unapaswa pia kutumia vidonge vyakuchomeka kwenye uke vya sulphathiazole mara mbili kutwa kwa wiki 2.

Ugonjwa huu unapompata mwanamke kwanza kabisa hukosa amani hata ya kukutana na mwenza wake na hasa kama mwenza huyo ni mtundu katika mambo fulani ya vishirikishi ngono yaani halianzishi hadi apime oil na kuzama chumvini. Hivyo mwanamke yoyote mwenye tatizo hili ni vema asilipuuziye kwa kuamua kushiriki tendo bila kupata tiba hata kama utajisafi vipi.

Uchafu wa majimaji mweusi au rangi ya kijivujivu ambao una damu na harufu mbaya
Mwanamke mwenye ugonjwa huu huwa amefikia hatua mbaya zaidi kwani yawezekana tayari kansa ikawa imeshamtafuna katika maumbile yake ya uke. Hata hivyo kansa sehemu za uke mara nyingi huwapata wanawake walio na umri zaidi ya miaka 40, na dalili ya kwanza inaweza kuwa ni upungufu wa damu mwilini au kutumia hedhi isiyo ya kawaida na kujisikia uzito au kuona uvimbe wenye maumivu katika kinena [kama una hali hii nenda kamuone daktari haraka].

Ugonjwa huu pia huambatani ambapo mtu akipatwa na homa anaweza nkunjwa dawa za kuua vijidudu au kumuona dk.

KIMSINGI: mwanamke yoyote yule ambaye anasumbuliwa na uchafu wa muda mrefu na hata akiutibu haupunguwei licha ya kufanya matibabu ya awali kama nilivyobaibisha hapo juu anapaswa kwenda kumuona daktari.

MUHIMU!

Mwanamke yoyote yule anaweza kuepuka magonjwa mengi ya ukeni endapo atafanya haya yafuatayo:-

Kuweka viungo vya uke wake katika hali ya usafi.
Mwanamke wakati anaogo anatakiwa kuhakikisha anasafisha vema uke wake kwa kutumia maji na sabubi na si kupuuzia kwa kujipapasa tu maana kuna wengine hujifanya kuona kinyaa yaani ataoga kote kisha huko anapanguza na toilet pepar kisha biashara imeisha hii ni mbaya, hivyo hata kama ukiwa kwenye baridi ama ukame wa maji hakikisha hulali bila kusafisha uke wako!

Kojoa baada ya kukutana na mwanaume
Hii ni kwa wale ndugu zangu wanaokwenda uwanja wa taifa kucheza mechi na kushuka dimbani pasipo kuwa na jezi yaani wao ni peku peku sasa wengine wakimalzia tu mechi huinuka kisha kujifuta na toilet paper na kujisafisha kidogo kisha hao wanakamata chupi na kuvaa huku akisindikiza na katoilet peapr chini yaani anaiweka kama vile awekavyo pedi, sasa hii ni hatari kwa majongwa kama niliyoyaeleza kwenye mada zangu.

Hakikisha umejipangusa au kujitawaza vizuri baada ya kwenda choo.
Mwanamke naamini anajua jinsi ya kujisafisha kwani zoezi hili hufundishwa tangu wakiwa wadogo lakini kama haujui ni vema ukajiswafi yaani kujipangusa kutoka mbele kwenda nyuma kwani kujipangusa kwa kwenda mbele husababisha mikroba, ameba au minyoo kwenye uke.Mashosti: KUTOKWA NA UCHAFU UKENI PART II
 
Kuna binti mrembo wa haja maringo meeeeeeengi.

Baada ya kumpigia misele sana, alikubali. Siku ya kwenda kula tunda la mti wa kati nilihisi kutapika! Baada ya kuwasha gari kama dakika 5 hivi, ulianza kutoka utando mweupe kama vile mtoto mchange amecheua au matapishi ya kuvimbiwa "maziwa mgando".

Huo uchafu ulikuwa unanuka (harufu mbaya). Yeye alidai kwamba alikuwa hajapata hiyo kitu siku nyingi sana.

Nilipokutana naye baada ya siku kadhaa, hali ya uchafu ni ule ule!

Kuna jamaa wameniambia inawezekana huyo shi anatumia panadol wakati wa siku zake. Nilipomuuliza binti amekataa matumizi ya panadol.

Kwasasa huo uchafu haunuki ila upo!!

Hii kitu inasababishwa na nini?
 
da? mkuu nafikiri unge geukia upande wa pili kwa doctor maana hapa si maala pake.
 
Nifangasi kaka wala isikupeshida, ila sasa anatakiwa kumuona daktari, kuna dawa atampa za kudumbukiza ndani. Hilo hata Mimi nshawahi kukumbana nalo.

Huwa unachuruzika kama uji vile. Pole sana.
 
Aisee!! Mngeenda hospitali pia kujua shida ni nini inawezekana na Infenctions

Ila kama hauna harufu inaweza kuwa normal nadhani kitu muhim awe anajisafisha vizuri huko chini.

wakisema mwanamke usafi sio kupaka wanja na shedo jamani ni pamoja na kujiswafi maungo yetu.

ukiwa wajisafisha shurti kidole kiingie mle ndani kwa ufasaha na utaona hata K inatyt kabisa baada ya kujiswafi.
 
Kwani mkuu kifo wewe utakikwepa??

....Kipi sasa, maana #Kifo au #Vifo vipo vya aina nyingi, kifo cha
#UtandoMweupe pia ni aina mojawapo ya Kifo.

In-short nataka tu kukwambia Kifo hakikwepeki, lakini aina ya kifo
ni #chaguo lako either kwa Makusudi au Bahati mbaya.
 
[QUOTaE=ntogwisangu;8005089]Njoo na jukwaa la siasa,achana hizi habari!!Umesikia ya Pinda na Mshahara wake?[/QUOTE]

Shabashiiii! unachanganya habari siyo..?
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom