Tatizo la kutokujua kusoma -Tufanye nini walimu?

Kalimanzira

Senior Member
Aug 15, 2007
100
27
Wana JF na walimu wenzangu,

Nimekuwa nikiwaza na kusikitishwa sana na kasi ya wanafunzi wetu kumaliza Elimu ya Msingi bila kujua kusoma na hata kuandika. Na sasa Serikali imeanzisha mfumo wa kuwatahini mara ya pili wanafunzi walio maliza S/Msingi ili kujua uwezo wao wa KUSOMA. Na ukifuatilia kwa makini wanafunzi hata wa Vyuo Vikuu, usomaji wao ni wa mashaka sana. Je Nini kifanyike? Tusaidiane
 
Hapo ni kushuka kwanza kwa Afisa elimu ya manispaa/wilaya ili tupate overview ya matokeo kwa wilaya nzima alafu tunashuka kwa Mratibu wa elimu wa kata nae atupe overview ya shule za kata nzima na zipo katika hali gani kisha tunamalizia kwenye shule husika ambapo watoto wasiojua kusoma kuona nini tatizo hasa. Kuulizia kama kuna facilities za kutosha ikiwa na maana ya madarasa mazuri, idadi tosha ya waalimu na vitabu kwa maana nyingine kibongobongo hali iwe nzuri hata kwa 60% kwani shule zetu tunazijua. Kama vitu vya msingi vipo hapo tunalia na walimu imekuaje hawajui alafu tunarudi tena kwa waalimu kujua imekuaje wamefaulu huku hawajui kusoma. Ila kiukweli wanafunzi hawajui kusoma kutokana na waalimu wengi wametelekezwa sana
 
Back
Top Bottom