ndiga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2014
- 582
- 592
Wasalaam ndugu zangu !
Mimi ninasumbuliwa na tatizo la kutoka mate ya kuteleza kwenye ulimi wangu na kooni.
Nikinywa kinywaji kama juice au soda basi mate mazito ya kuteleza huwa yananisumbua mpaka itabidi nianze kukwarua kwarua ulimi wangu kwa meno huku nikitema mara kadhaa ndipo hali hupungua.
Nikiwa nimelala huwa nahisi wakati mwingine kama kubanwa na mafua yanayofanya matundu ya pua yangu kuziba harafu nikilala huwa nakoroma sana.
Wakati wa kupiga mswaki asubuhi nikipitisha kidole kooni huwa natoa uchafu mithili ya makohozi mazito na baadaye kama makamasi kamasi na hali hii huendelea wakati wote natema mate ambayo siyo yale niliyozoea kuyaona zamani.
Hali hii nimekuwa nayo kwa muda mrefu kama miaka miwili bila kupata msaada.
Nilikwenda hospitali ya wilaya Ngudu nikamweleza daktari akaniambia kuwa sina tatizo lolote baada ya kuniambia kuachama na kunimulika kwa tochi akanipa mouth wash nitumie.
Kooni siyo kwamba kunauma au kwamba kuna vidonda au kwamba nina kohoa hapana , ila hali ndiyo hiyo inayoninyima amani maana nikienda hospitali naambia sina tatizo na kidogo yule daktari alionekana kuchukulia kawaida tatizo langu.
Nimeona tatizo langu nililete hapa JF Doctor maana hapa kuna wataalamu mbali mbali wa matatizo yanayotukumba binadamu.
ASANTENI NASUBIRI USHAURI, MUNGU ATUBARIKI WOTE.