Mwifwa
JF-Expert Member
- Apr 3, 2017
- 46,876
- 122,112
Jambo la muhimu katika kuchagua mpenzi wako ama awe katika mahusiano au mwezi wako wa ndoa ni lazima/muhimu mkajuana na kutambuana tabia zenu na hatimae kuridhiana na kuingia kwenye mahusiano.
Mnaweza kudumu katika mahusiano kwa muda fulani lengo likiwa ni kuzoeana na kutambuana hizo sifa ambazo kila mmoja anataka mwezi wake awe nazo hasa mwenendo kitabia.
Kumeibuka na mtindo wa kuonesha tabia kwa mpenzi wako ambazo sio tabia halisi ulizo nazo lengo au nia yako ikiwa ni kumvutia huyo mpenzi wako ili aendelee kuwa nawe ilihali hizo tabia sio halisi.
Wengine wanaweza kuwa wawazi na kuonesha tabia zao halisi lakini ikawa ni vigumu wao kutambua madhaifu ya kila mmoja akidhani hana madhaifu.
Siku wakiingia kwenye ndoa ghafla tabia ambazo kila mmoja alikuwa nazo na wakaaminiana kipindi cha mahusianao zinaanza kuonekana zikitoweka na kuibuka tabia zingine mpya ambazo ni kikwazo katika ndoa.
Nini kifanyike kwa wapenzi wakiwa kwenye mahusiano wakitarajia baadae wawe wana ndoa ili kuonesha tabia ambazo ni za kweli wakati wa mahusiano na wakiwa kwenye ndoa, na pia ni mbinu gani itumike kutambua madhaifu ya mpenzi wako pale unaposhindwa kuyatambua na wakati akijaribu kuyaficha hayo madhaifu yake.