Kurunzi
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 9,277
- 9,912
Naomba niwashirikishe kilichonipata ili angalau walio na tatizo kama lililonipata waweze kujua pakuanzia.
Miezi ya hivi karibuni nnapatwa na hali flani ya kukosa pumzi na Kupumua kwa shida, hali hii hujitokeza zaidi wakati wa usiku minapo lala hali hii wakati inajitokeza mara nyingi nikisafisha Koo kwa kukohoa basi napata auheni kidogo lakini hali baadaye inarudi pale pale.
Baada ya kuona hali inaendele kuwa mbaya siku hadi siku ilibidi niende hospital nilienda hospitali ya Rabininsia pale Tegeta baada ya kuongea na Dr na kunifanyia vipimo vya Damu na X-ray hawakuona tatizo lolote hata hivyo Dr. Alinikandikia Dawa za kutumia mwezi mzima (Montelukast tab na Salmetrol inheiler) za kutumia, mbaya zaidi zinauzwa ghali tena na hazipo kwenye bima.
Nilitumia sawa kama nilivyoshauriwa na Dr. Hata hivyo sikupata nafuu yoyote tena hali ilizidi kuwa mbaya sana ikafikia wakati napata kikohozi kikavu nakohoa mpaka tumbo linauma pia kufua nakuwa kama nakoroma (wheezing) ninapolala.
Nakumbuka siku moja nilibanwa sana usiku nikawa nakohoa sana nikakosa kabisa usingizi mpaka kunakucha nilipata wasiwasi nikahisi tatizo la moyo nini au kifua kikuu yaani nilikuwa na mawazo kweli kweli.
Kesho yake asubuhi nikaongea na jamaa yangu akanielekeza hospitali moja ipo Bagamoyo zinga aliniambia ina madaktari wazuri ikabidi nifunge safari mpaka Bagamoyo Zinga ingawa sikuwa na Imani Sana Kama nitaweza kupata matibabu.
Baada ya kunisikiliza ninavyojisikia na kuniuliza maswali hasa juu ya life style yangu bila hata kunifanyia vipimo moja kwa moja aliniambia na tatizo la Acid, ( Acid Reflux) kwakweli siku muelewa kabisa niliona ni wale wale nilijaribu kumwambia kwanini asinipime akasema hapana akasema atanindikka sawa ikiwa Hali haitakuwa vema nirudi.
Alinikandikia Dawa za wiki 2 Omeprozole na Antacid Gel pia aliaambia niache aina flani ya Chakula hasa vinavyosababisha acid nk.
Kiukweli nilijisemea moyoni nitazimeza siku 3 au 4 kama sijapati nafuu yoyote naachana nazo naenda Muhimbili nikafanye uchunguzi wa Moyo.
Nashukuru siku ya 3 baada ya kutumia dawa nikaanza kuona nafuu ile hali kukosa pumzi ikaisha ghafla na kikozi kikaanza kulainika kadri ya siku zinaenda. Hali ikawa nzuri mpaka siku namaliza dawa nilikuwa nipo Safi kabisa.
Nilirudi hospitali kumuona tena Dr lengo likiwa kumshukuru aliniambia hapo ndipo aliponipa somo juu ya huo ugonjwa alisema unaitwa Chronic Acid Flux au GERD alisema ugonjwa huu husababishwa na mambo kadhaa lakini kifupi ni kiasi cha Acid au Digestive acid juices (nyongo) inarudi nyuma kwenye kiumio au Koo na kublock mfumo wa upumiaji au acid inaenda mpaka kwenye mapafu hivyo kusababisha tatizo la kukosa pumzi au kupumua kwa shida nk
Alinisihi ili nisipate tena tatizo hilo nibadilishe mfumo wangu wa maisha napaswa kujiepusha na vyakula vya acid, pombe, heavy meal badala yake nile chakula kidogo mara nyingi, nijiepushe na kula mlo then naenda kulala nipate walau masaa 2 au 3 ndiyo nikalale.
Kweli namshukuru sana kwa sasa nipo na afya njema.