Tatizo la kushindwa kufaulu mtihani wa kuajiri linatokana na nini

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,010
7,764
Habari za Leo wapendwa,
Heri ya siku ya wafanyakazi duniani.

Wapendwa kwanza kabisa nikiri kwamba taifa letu bado ni changa na ili liweze kuendelea linahitaji kuajiri wataalam mbalimbali katika sekta mbalimbali.

Inashangaza sana taifa hili eti linashindwa kuajiri huu ni mkwamo mkubwa katika uwezo wetu wa kufikiri watanzania kwaujumla.

Watu tuliowapa dhamana ya kuongoza wizara zetu wamekwama wanahitaji msaada kutoka akili za nje. Wao ndio wapo karibu na vyanzo vyote vya ajira, sasa wanashindwaje kutengeneza ajira.

Tatizo limeanzia hapo kwenye viongozi wa wizara zetu, wao ndio wameshikiria maliasili za nchi na wapewa dhamana hiyo, wanashindwaje kufikiri ili rasilimali hizo zitengeneze ajira kwa watanzania?

Ni wapi wanapokwama tuwasaidieni, jamani.

Kujiajiri ni kuzuri sana lakini tunatamani kuona watu wakijiajiri katika fani walizosomea ili kukuza sayansi na teknolojia nchini. Sio mtu kasomea mechanical engineering unataka akajiajiri kuendesha bodaboda.

Kwa mfumo huo sayansi na teknolojia haviwezi kukua. Katika Sera ya kujiajiri wawezesheni watu wajiajiri kila mmoja katika fani aliyosomea ndipo tutakapoweza kupata maendeleo endeleavu katika sayansi na teknolojia ndani ya taifa hili.

Imani yangu ipo hapa.
Kujiajiri katika fani uliyosomea na maendeleo endelevu katika sayansi na teknolojia.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom