Tatizo la kupata hedhi nyingi kupita kiasi na athari zake kiafya

Dr Norman

Member
Oct 6, 2019
11
40
Kupata hedhi kupita kiasi ni moja ya matatizo ya uzazi yanayosumbua wanawake wengi. Tafiti zimeonyesha kwa kila wanawake 1000; wanawake 53 kati ya huwa na tatizo la kupata hedhi kupita kiasi. Ni theluthi tu ya wanawake wenye shida ya hedhi hutafuta tiba stahiki kwa daktari wengi hukaa nayo kwa aibu au hofu.

Je ni wakati gani mwanamke anatakiwa kuhisi kuwa anapata hedhi kupita kiasi?
  • Unapata hedhi inayozidi siku 7
  • Unapata hedhi nzito inayofanya ubadiri pedi moja ndani ya masaa mawili
  • Unapata hedhi nzito inayokulazimu kuvaa pedi zaidi ya moja
  • Unapata hedhi nzito inayolowesha hadi nguo za nje
  • Unapata hedhi nzito inayokulazimu kuamka usiku kubadiri pedi
  • Hedhi inayotoka na mabonge
320633_1100.jpg


Sababu gani huweza kuchangia mwanamke kupata hedhi nzito kupita kiasi?
  • Vivimbe kwenye kuta za mji wa kizazi; vivimbe hivi sio saratani huitwa fibroids
  • Yai kupevuka bila mpangilio (Irregular ovulation) ; hali hii husababisha kuta za mji wa mimba zivimbe na kuwa nene hivyo kutoa damu nyingi. Hutokea zaidi kipindi cha kuvunja ungo na kipindi cha kukaribia ukomo wa hedhi
  • Matatizo ya kugandisha damu
  • Matumizi ya dawa za kuzuia damu kuganda
  • Baadhi ya wanawake waliotumia vitanzi (IUD) hasa ndani ya mwaka wa kwanza
  • Maambukizi ya mji wa mimba na mirija ya uzazi (PID)
  • Endometriosis
  • Saratani ya mji wa kizazi; kwa kinamama waliofikia umri wa ukomo wa hedhi. Wakianza kupata hedhi isiyokoma huweza kuwa dalili ya ya saratani ya mji wa kizazi.
Athari za hedhi nzito kupita kiasi kwenye afya
  • Hedhi nzito kupita kiasi huchangia wanawake wengi kupata upungufu wa damu
  • Hedhi kuwa nzito kupita kiasi huweza kuwa ni dalili ambao unahitaji tiba ya haraka
  • Huweza kuchangia kudhoofisha afya ya akili ya mwanamke ikiwemo kujiamini na wasiwasi
Nini hufanyika unapomuona daktari kuhusu tatizo la kupata hedhi kupita kiasi ?
  • Unapomuona daktari atachukua historia ya afya yako kwa ujumla
  • Historia ya afya ya uzazi na mzunguko wako wa hedhi
  • Historia ya dawa zote unazotumia
  • Daktari atahitaji kukufanyia vipimo vya mwili ili kuangalia kama kuna kisababishi kinachochangia hedhi kutoka kwa wingi
  • Daktari naweza chukua damu kupima wingi wako wa damu , kiwango chako cha homoni za uzazi pia na vipimo vingine kulingana na alivyokuona
  • Datari anaweza kukufanyia ultrasound ili kungalia mji wa uzazi na via nyingine za uzazi kama kuna tatizo
Je ni tiba aina gani hutumika kutibu tatizo la kupata hedhi nyingi kupita kiasi?

Tatizo la kupata hedhi nyingi kupita kiasi hutibiwa kulingana na chanzo kilichosababisha tatizo hilo, afya yako kwa ujumla na uchaguzi wako tiba; baadhi ya tiba ni pamoja na :
  • Tiba ya dawa zenye homoni
  • Tiba za dawa za kugandisha damu - Hutolewa iwapo hedhi inayotoka ni nyingi sana
  • Upasuaji wa kuondoa vivimbe vya fibroids
  • Tiba ya kukwangua kuta za mji wa mimba
  • Tiba ya kuziba mishipa ya damu ya mji wa kizazi. Huitwa “uterine artery embolization”

Imeandaliwa na Dr. Norman.
 
Mkuu naomba kujuzwa complication zinazoweza kutokea katika kufanya operation ya kuondoa fibroids zilizopo ndani ya nyumba ya uzazi. Wife anatakiwa kufanyiwa operation soon so nataka nijiandae kisaikolojia.

Thanks
 
Mkuu naomba kujuzwa complication zinazoweza kutokea katika kufanya operation ya kuondoa fibroids zilizopo ndani ya nyumba ya uzazi....wife anatakiwa kufanyiwa operation soon so nataka nijiandae kisaikolojia.Thanks

Kabla ya UPASUAJI WOWOTE kitu muhimu kuangalia huwa ni faida na hasara za operation husika. Upasuaji huu huitwa myomectomy katika tiba.

Hasara za kuwa na fibroids ni pamoja na kutoka damu nyingi wakati wa hedhi, maumivu ya tumbo na mgongo, matatizo ya uzazi. Hivyo upasuaji huwa na umuhimu kufanyika.

Risk za upasuaji wa kutoa fibroid huwa ni adimu sana zinaweza husisha kupoteza damu nyingi wakati wa upasuaji, madhara ya dawa za usingizi (Hutokea mara chache sana), kubaki na kovu la upasuaji na kuhitaji kujfungua kwa upasuaji mimba zote zitakazofuata baadae.
 
Dr Norman,
Thanks mkuu...na hizo njia nyingine tofauti na upasuaji zinapatikana hapa bongo? Na je nasikia kuna tiba ya vidonge pia hili unalizungumziaje? Thanks in advance.
 
Matibabu ya fibroids yameganyika makundi 3 makuu:
1. Matibabu ya fibroids kutumia dawa

2. Matibabu ya fibroids kwa njia ya upasuaji na

3. matibabu ya fibroids kwa njia ya kuziba mishipa ya damu inayohudumia uvimbe

Njia ya upasuaji ndio msingi mkuu wa matibabu wa fibroids maana huleta matokeo mazuri kwa muda mfupi.
Njia ya kuziba mishipa ni utaalamu mpya, Aga Khan huwa wanafanya hiyo huduma. Kitengo cha radiolojia-tiba muhimbili wanataka kuanza kutoa hii huduma.
Thanks mkuu...na hizo njia nyingine tofauti na upasuaji zinapatikana hapa bongo? Na je nasikia kuna tiba ya vidonge pia hili unalizungumziaje? Thanks in advance.
 
Habari wakuu kuna mdada anasumbuliwa na hedhi isiyokatika na humchukua kuanzia mwezi hadi miezi kadhaa kutokuta. Naonbeni ushauri Wa haraka Wa tiba kwa mtaalamu yeyote anayefahamu.

Ahsanteni
 
Habari wakuu kuna mdada anasumbuliwa na hedhi isiyokatika na humchukua kuanzia mwezi hadi miezi kadhaa kutokuta.Naonbeni ushauri Wa haraka Wa tiba kwa mtaalamu yeyote anayefahamu.Ahsanteni
Pole mkuu,em mtag skylat sjui km jina nmepatia,aliwahi toa ushaur fulani ukasaidia tatizo la binti yangu mda kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza ni lazima utafute chanzo cha tatizo

Je anatumia uzazi wa mpango?? Kama ndio ni njia gani anatumia??

Na je hiyo shida ilimuanza lini??

Ameshakwenda hospitali???

Bagwell
 
Matatizo hayo ya hedhi yanasababu kadhaa,ili tatizo liishe lazima ujue tatizo liko wapi hasa,tatizo hilo linaweza kuja moja kati ya yafuatayo
1.uterine fibroids
2.uterine polyp
3.Endometriosis
4.Hormonal imbalance
5.Ovarian cyst

Hivyo vipimo vifuatavyo vinahitajika
1.ultrasound
2.hormonal profile
3.FBP

Kwa sasa wakati unasbr mchakato wa matibabu tumia dawa izi
1.Folic acid 5mg OD for 2 month
2.Inj traxenamic acid
3.COC for a month

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hutojali, Maombi yana tiba bila gharama yoyote. Mwili ni mali yako na maisha ni yako vilevile, uamuzi anao mhusika.
Bwana Yesu a aponya faster shida kama hizo. Njoo kwa Bwana Yesu upate uponyaji wa haraka.

Ubarikiwe!!
 
Kwanza ni lazima utafute chanzo cha tatizo

Je anatumia uzazi wa mpango?? Kama ndio ni njia gani anatumia??

Na je hiyo shida ilimuanza lini??

Ameshakwenda hospitali???

Bagwell
Hospitali kashaenda Mara kadhaa lakini akipata Tiba inakata kwa muda lakini baadae inarudia tens hiyo hali,,kwa maelezo yake anasema hajawahi tumia vidonge wala vitu vyovyote vya uzazi wa mpango
 
Matatizo hayo ya hedhi yanasababu kadhaa,ili tatizo liishe lazima ujue tatizo liko wapi hasa,tatizo hilo linaweza kuja moja kati ya yafuatayo
1.uterine fibroids
2.uterine polyp
3.Endometriosis
4.Hormonal imbalance
5.Ovarian cyst

Hivyo vipimo vifuatavyo vinahitajika
1.ultrasound
2.hormonal profile
3.FBP

Kwa sasa wakati unasbr mchakato wa matibabu tumia dawa izi
1.Folic acid 5mg OD for 2 month
2.Inj traxenamic acid
3.COC for a month

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante kwa ushauri wako Mwana JF
 
Back
Top Bottom