Tatizo la kupata choo kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation). Fahamu chanzo na tiba yake

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,200
4,991
1587964722786.png

BAADHI YA WADAU WENYE TATIZO HILI
Nisaidieni dawa ya kuniwezesha kupata choo cha kawaida, maana ni miaka sasa imepita nimekuwa na hili tatizo la kuwa na choo kigumu kiasi kwamba nasikia haja kubwa na nikienda toilet kujisaidia napata taabu sana..
---
Nilienda hospitali kumuona daktari akanipatia dawa nikazitumia na zilinisaidia sana na akaniambia ninywe sana maji na kwa kweli sasa ivi nakunywa sana maji...

Nikikaa baada ya mda ilo tatizo huwa linanirudia nikinywa dawa huwa linaisha mimi ni mtu wa kunywa dawa....

Imefikia hatua kale kanyama kwenye haja kubwa kametokeza kwa sababu ya kupata taabu wakati wa haja..

Nisaidieni wanajamii wenzangu jinsi ya kuepukana na hili tatizo maana limekuwa kama ni sehemu ya maisha yangu naona kama litakuja kuniletea madhara makubwa mno...
---
Wakuu habari ya Mchana huu. Naomba msaada wenu wa ushauri juu ya tatizo nililolitaja hapo juu.

Ni zaidi ya mwezi mmoja sasa kila nikishikwa na haja kubwa, choo kinakua kigumu sana na napata maumivu makali wakati wa kupushi. Baada ya kuona halii hii inajirudia kila niendapo chooni, niliamua kwenda hospital ambapo nilipewa Flagil na Diclofenac, wakanishaur niwe nakunywa maji mengi pamoja na matunda kwa wingi.

Nilijitahidi kufuata maagizo hayo lakini nikirudi toilet napatwa na hali ileile kwa maumivu makali.

Wikk mbili baadae nikaenda hospital nyingine nikapewa vidonge flani vidogo dogo hivi. Daktar akaniambia hivi ni assistive tu lakini natakiwa nile matunda sana pamajo na maji atleast lita 3 kwa siku.

Kweli vilinisaidia vile vidonge, niliharisha sana. Pia nikawa nakula matunda pamoja na maji mengi.

Sasa vile vidonge vimeisha, nikahisi labda tatizo litakua limeisha pia, hivyo sina haja ya kununu vingine.

Ukiacha mbali sharti la kunywa maji mengi na kula matunda, kazi yangu inanihitaji pia nipate Heavy meal. Lakini bado nikirudi chooni hali inakua ileile. Pia zinaweza kupita hata siku mbili nisijisikie kabisa haja kubwa.

Hali hii inanikosesha furaha kabisa na imenisababishia vidonda sehem ya haja kubaa ambavyo vinashindwa kupona kwa sababu ya tatizo kujirudia.

Naomba Msaada wenu kwa yeyote ambae anafahamu nini cha kufanya, hata kama kuna tiba mbadala.

Natanguliza shukrani zangu.

Asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
===
UFAFANUZI WA JUMLA KUHUSU TATIZO HILI
Ukosefu wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida. Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu. Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?
- Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa.

- Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

NINI HUSABABISHA TATIZO?
Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

NINI KIFANYIKE?
Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo: Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda msalani. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi. Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];castor Oil' muda mfupi kabla ya kwenda kulala. Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.
---

TATIZO LA CHOO KIGUMU KWA WATOTO
Tatizo la kukosa choo watoto wadogo au kuwa na choo kigumu na jinsi ya kulitatua
Watoto wadogo hasa wale ambao bado wananyonya na ndio kwanza wamenzishwa vyakula vinginevyo zaidi ya maziwa, mara nyingi hupatwa na choo kigumu au kukosa choo kabisa hali tunayoiita kimombo, constipation.

Hali hiyo huanza pale mtoto anapoachishwa maziwa ya mama na kuanza kunyweshwa maziwa ya kopo au mengineyo au pia anapoanzishwa kula vyakula vingine zaidi ya maziwa.

Mara nyingi watoto wanaonyonya maziwa ya mama huwa hawasumbuliwa na tatizo hilo, bali tatizo hilo huanza kujitokeza pale wanapoanza kulishwa vyakula vingine zaidi ya maziwa ya mama.

Pia mama ambaye tayari mwenyewe anasumbuliwa na tatizo la kukosa choo, huenda mwanae pia akasumbuliwa na tatizo hilo.

Mtoto mwenye tatizo la kukosa choo huwa anapata choo wa shida huku akisumbuliwa na tumbo na kupata choo kigumu. Wakati mwingine hulia wakati akipata choo huku akijiminya na kukunja uso. Muone daktari iwapo mtoto ana umri wa chini ya mwezi mmoja na hajapata choo kwa siku 4.

Iwapo mtoto wako mchanga au mdogo ana tatizo la kukosa choo au kupata choo kigumu kwanza wasiliana na daktari au mpeleke hospitalini ili upate ushari wa daktari. Pia unashauriwa kujaribu njia zifuatazo:

1. Jaribu kumpa mtoto wako maji safi na salama kuanzia mililita 60 hadi 120 kwa siku. Punguza au ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao inavyokuwa. Ni bora maji ya mtoto yachemshwe na kufunikwa vyema.

2. Iwapo maji hayasaidii, jaribu pia kumpa juisi za matunda. Mpe mtoto wako juisi ya tufaha (apple), pea au prune iliyotengenezwa kwa kutumia maji salama na safi kila siku. Anza kwa mililita 60 hadi 120 kwa siku na punguza au ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao inavyokuwa.

3. Jitahidi kumpa mwanao chakula chenye ufumwele au fiber. Iwapo mwanao ameanza kula vyakula vigumu, basi mpe vyakula vyenye ufumwele kuliko vyakula vyenye wanga, kama vile tumia unga wa shayiri au tunda la apple na pea lililopondwa pondwa vyema na kuwa kama uji. Epuka kumpa mtoto cereal ya mchele au uji wa mchele kama anatatizo la kukosa choo au kufunga choo.

4. Jiepushe kumpa mtoto wako vyakula vyenye wanga na sukari na vyakula vinavyotengenezwa kwa unga uliokobolewa.

5. Mpake mwanao mafuta kidogo sehemu inayotoka choo kikubwa ili kurahisisha utokaji wa kinyesi. Usitumia mafuta ya madini (mineral oil) au dawa za kulainisha choo na za kuharishwa katika kutibu tatizo hilo la kukosa choo la mtoto.

6. Kukosa choo watoto wadogo mara chache huwa kunasababishwa na magonjwa kama vile Hirschsprung ugonjwa wa kumee neva katika utumbo, au Cystic Fibrosis. Muone daktari au mpeleke mtoto wako hospitalini kama tatizo hilo la kukosa choo linaendelea hata baada ya kubadilisha aina ya chakula cha mtoto au linaambatana na dalili nyingine kama vile kutapika au mtoto kukosa utulivu na kuhangaika.

7. Kuna baadhi ya watoto wanakosa choo au kuwa na choo kigumu kutokana na kutumia maziwa ya ng'ombe. Iwapo umetumia dawa na umefuata maelekezo ya kuondoa ukosefu wa choo na hukufanikiwa. Katisha kumpa mtoto maziwa ya ng'ombe kwa siku mbili au tatu, baada ya siku hizo iwapo bado hajaacha choo badi endelea kumpa maziwa hayo, na pengine tatizo hilo halisababishwi na maziwa ya ng'ombe.

8. Mwogeshe au mweke mwanao katika beseni la maji ya uvuguvugu na hakikisha maji yanafika hadi kifuani. Mkande mtoto tumbo lake wakati akiwa majini na njia hiyo husaidia kulegeza misuli ya mwili wa mtoto, na kumsaidia kupata chook wa urahisi.

NB: Ukosefu wa choo kwa watu wazima baadhi ya wakati huandamana na magonjwa kama vile Arthritis, Appendicitis, Cataract, saratani, shinikizo la damu, Rheumatism na kadhalika lakini kwa watoto huenda tatizo hilo likawa halisababishwi na maradhi hayo.

Utafiti unaonyesha kuwa hakuna uhusiano wowote kuhusu kukosa choo mtoto na kupewa nyongeza ya chuma au Iron Supplement. Hivyo usimkatishe kumpa mwanao chuma iwapo anakosa choo. Kwani chum ni muhimu sana katika kuzuia upungufu wa damu mwilini kwa mtoto wako mdogo.
===

MAONI NA USHAURI ULIOTOLEWA NA WADAU KUHUSU TATIZO HILI
Tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu ni jambo tunalolikwepa kwenye mazungumzo yetu ya kila siku. Hata hivyo ni tatizo kubwa katika jamii na mbaya zaidi wengi hawajuwi madhara yake ni nini ya kuendelea kulivumilia tatizo hili.

Kupata choo kigumu au kufunga choo ni ishara ya tatizo lingine baya zaidi mwilini. Kama kuna jambo unapaswa uliepuke kwa nguvu zote basi ni hili. Kwa afya bora kabisa hakikisha unapata choo kila siku mara 2 hata mara 3.

Choo kilaini siyo kigumu na chenye maumivu. Wakati mwingine utakapopata tatizo hili naomba usiwe na aibu kulisema wazi hata kwa boss wako ili upate matibabu kwa haraka. Kufunga choo au kupata choo kigumu ndiyo CHANZO KIKUU CHA UGONJWA WA BAWASIRI kwa waTanzania wengi na hii inachangiwa kwa sehemu kubwa kwa kula ugali wa sembe na kutokunywa maji mengi kila siku. Pamoja na hayo, hakuna ugonjwa rahisi kutibika kama huu ikiwa utaamua kushughulisha kichwa chako kidogo hasa kwa kuangalia unakula na kunywa nini kila siku.

Dawa mbadala 10 zinazotibu kufunga choo au choo kigumu:

1. Mafuta ya Zeituni Mafuta ya zeituni (olive oil) yanatosha kutibu hili tatizo.
Yana radha nzuri mdomoni na ni dawa pia. Kama unaweza yafanye pia kama mafuta yako ya kupikia vyakula vyako mbalimbali, mafuta haya huweza kuliwa pia bila kupitishwa kwenye moto na hivyo ni mafuta mazuri kuweka kwenye kachumbari au saladi mbalimabali.

Matumizi: Chukua kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya zeituni changanya na kijiko kidogo kimoja cha chai cha maji maji ya limau na unywe asubuhi ukiamka tu tumbo likiwa bado tupu. Fanya hivi kila siku mpaka utakapopona.

2. Juisi ya Limau
Juisi ya limau inatumika kutibu tatizo la kupata choo kigumu au kufunga choo.
Chukua maji maji ya limau kutoka katika limau kubwa 3 na uchanganye na juisi ya matunda kupata kikombe kimoja (ml 250) na unywe yote kutwa mara 1 kila siku kwa siku kadhaa mpaka umepona. Ukiacha hilo la kutibu kufunga choo limau ina vitamini C nyingi na hivyo itakuongezea kinga yako ya mwili kwa haraka zaidi (usizidishe hata hivyo).

3. Mazoezi ya kutembea
Kama unataka kupata choo kilaini na cha kawaida basi jitahidi uwe mtu wa kutembeatembea na si kukaa tu kwenye kiti kutwa nzima. Maisha yetu ya kisasa na kazi za ofisini zinatulazimisha kuwa watu wa kukaa kwenye kiti masaa mengi wengine huamua tu kukaa kwenye kiti sebureni akiangalia TV asubuhi mpaka jioni!.

Aina hii ya maisha ni hatari zaidi kwa afya zetu kuliko hata madawa ya kulevya. Jitahidi kila siku uwe unapata muda wa kutembeatembea kwa miguu mpaka dakika 60 au zaidi. Hii itakusaidia kuondoa tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.

4. Vyakula vya nyuzinyuzi (fiber)
Mara nyingi utasikia watu wakisisitiza juu ya umhimu wa kula vyakula vya asili na vyenye nyuzinyuzi. Chakula cha asili kina nafasi kubwa katika kuimarisha afya yako kwa ujumla. Kinachonishangaza ni kuona watu bado wanaendelea kula ugali wa sembe ilihali inajulikana wazi ugali mweupe ndiyo chanzo kikuu cha kupata choo kigumu ikiwemo ugonjwa wa bawasiri.

Ninakusihi sana uanze kula ugali wa dona kuanzia sasa na kuendelea. Hakikisha pia asilimia 80 ya mlo wako kwa siku ni matunda na mboga za majani. Matunda kama ndizi na parachichi ni mhimu ule kila siku kadharika tumia unga au mbegu za maboga.

5. Mshubiri (Aloe Vera)
Mshubiri unajulikana wazi kwa kutibu tatizo hili la kufunga choo au kupata choo kigumu. Ni mhimu utumie mshubiri fresh kabisa kutoka kwenye mmea moja kwa moja kuliko kutumia za dukani au za kwenye makopo. Usitumie zaidi ya vijiko vikubwa viwili vya jeli ya shubiri kwa siku.

Matumizi: Changanya vijiko vikubwa viwili vya jeli ya aloe vera ndani ya kikombe kimoja cha juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani (hasa juisi ya parachichi) na unywe yote kutwa mara 1 hasa nyakati za usiku unapokaribia kwenda kulala kwa siku kadhaa au mpaka umepona.

6. Baking soda Baking soda ni dawa nyingine ya asili nzuri kwa tatizo hili. Inafanya kazi vizuri kwa zaidi ya asilimia 95. Sababu ya bicarbonate iliyomo ndani yake itakusaidia kupumua nje vizuri gesi au hewa yoyote ilisongamana ndani ya tumbo pia inasaidia kupunguza asidi mwilini. Baking soda ni ile wamama huitumia katika kupika maandazi au mikate inapatikana katika maduka ya kawaida hata hapo nje kwa Mangi ipo.

Matumizi: -Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha baking soda ndani ya nusu kikombe cha maji ya uvuguvugu (ml 125) na unywe yote kwa haraka kutwa mara 1 kwa siku 7 hivi au unaweza kuacha siku yoyote kabla kama tatizo litakuwa limeisha.

7. Mtindi
Unahitaji bakteria wazuri zaidi wakati huu unapokabiliwa na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu. Utahitaji pia kuacha kula vyakula vya kwenye makopo (processed sugars and foods). Namna rahisi kabisa ya kuhakikisha mwili wako unapata bakteria wazuri ni kwa kutumia mtindi. Tumia mtindi wowote ule uliotengeneza mwenyewe nyumbani au hata wa dukani (ila wa dukani usiwe umeongezwa vitu vingine ndani yake – sweetened yogurt).

Matumizi: Kunywa kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi wakati wa chakula cha asubuhi na kikombe kingine usiku unapoenda kulala kwa wiki 1 hata 2.

8. Fanya mazoezi ya kusimama na kuchuchumaa (squat)
Fanya mazoezi ya kuchuchumaaa na kusimama (squatting). Hili ni zoezi mhimu kwa mtu anayesumbuliwa na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana. Fanya kuchuchumaa na kusimama mara 25 na upumzike dakika 1 kisha unaendelea tena unachuchumaa na kusimaa hivyo hivyo mara 25 kwa mizunguko mitano (5 rounds) huku ukipumzika dakika 1 kila baada ya mzunguko mmoja.

Fanya zoezi hili kila siku mara 1 na usizidishe sana, ni mara 25 kwa mizunguko mitano inatosha na uzuri ni kuwa unaweza kufanya zoezi hili mahali popote. Wakati huo huo unashauriwa kutumia choo cha kuchuchumaa yaani vile vyoo vya zamani na siyo hivi vya kisasa vya kukaa kama vile upo ofisini. Vyoo hivi vya kukaa ndiyo moja ya vitu vinavyochangia upate pia ugonjwa wa bawasiri (kuota kinyama sehemu ya haja kubwa na kupata maumivu wakati unajisaidia).

9. Matunda
Asilimia 80 ya chakula chacko kwa siku iwe ni matunda na mboga za majani. Unapoumwa na hili tatizo pendelea zaidi parachichi, papai na juisi ya ukwaju. Kula matunda siyo mpaka uumwe au ushauriwe na daktari, fanya kuwa ndiyo tabia yako kila siku na hutakawia kuona mabadiliko makubwa kwa afya yako kwa ujumla.

10. Maji ya Kunywa Maji ni uhai.
Asilimia 75 ya mwili wako ni maji. Asilimia 85 za ubongo wako ni maji. Asilimia 94 ya damu yako ni maji. Hakuna maisha bila maji. Inashangaza sana kuona mtu anamaliza siku nzima au hata siku 2 hajanywa maji! Kama wewe si mpenzi wa kunywa maji ya kutosha kila siku SAHAU KUWA NA AFYA NZURI MAISHANI MWAKO.

Hakikisha unakunywa maji kila siku lita 2 mpaka 3, kidogo kidogo kutwa nzima bila kusubiri kiu na hutaugua tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu. Dawa nyingine nzuri kwa ajili hii ni unga wa mbegu za mlonge
---
UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida.

Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu.

Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?

Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa.

Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

NINI HUSABABISHA TATIZO?

Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

NINI KIFANYIKE?

Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo:

Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda Choo. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi.

Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil' muda mfupi kabla ya kwenda kulala.

Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.
---
Pole sana.
Nilikuwa na hilo tatizo pia, nikaja kugundua ni vidonda vya tumbo ambapo mara nyingi nikiwa natumia dawa (antibiotics kama doxy au cipro) ndio tatizo linakua kubwa sana, na nilikua nakula vzur mboga mboga na matunda.

Solution kwangu ikawa kuziepuka hizo dawa lakini pia KUFANYA MAZOEZI. Trust me ukiwa unafanya mazoezi na unakula matunda vizuri lazima uende toilet almost kila siku.
Hii unatoka nyumban unaenda kazini unakaa kwenye A/C siku nzima na unakula mivyakula yetu hii ya kibongo ni tatzo.

Pia juice ya ukwaju ni kiboko (isiwe chachu sana kama una vidonda vya tumbo).
All the best!
---
Orayt. .!orayt. .to cut the story short .nenda pharmacy au duka la dawa la kawaida tu nunua dawa moja inaitwa bisacodril na tatizo limeshatatuliwa.

Mimi kuna kipindi nilipata hilo tatizo ilikua kama wiki nzima hadi kukaa au kutembea nilikua naumia kwaule ugumu nikaenda hospitali wakanipa hio dawa.

ni tudonge tudogodogo dizain yake kama priton ila reaction yake balaaaa. .kamoja asubuhi kengine jioni ila nilimeza kamoja tu ka asubuhi sijarudia ka jioni ila niliendesha balaa. . na tatizo liliisha kadonge kamoja tu just imagine

Cc Smart911
---
financial services,
1. Punguza matumizi ya nyama ng'ombe na mbuzi au kondoo
2. Kula dona na punguza ulaji wa sembe na wali
3. Dawa za minyoo kutumia mara ya mwisho lini? Tumia dawa za minyoo, tumia ketrax baada ya siku saba rudia dozi.
4. Jitahidi matunda na mboga za majani
5. Ratiba ya kula uifuate.
6. Muda wa kwenda toilet uwe na ratiba
---
Mkuu pole sana

cha kwanza kunywa dawa za minyoo, pili kacheki typhoid pia

Tatu kama unapata choo kigumu dawa yake ni hii, unapokula chakula sindikiza na maziwa mtindi, or fresh maziwa ni the best

Choo kigumu kitakwangua kuta zitatoa damu, mwishowe utajuta

Sent using Jamii Forums mobile app
---
Wangaya, Mkuu matunda unakulaje na maji una kunywaje?

Unapaswa kutenga moja kati ya milo yako mitatu ya siku uweni matunda tu...! Yani kwa mfano asubuhi badala ya kunywa chai basi unajaza mchanganyiko wa matunda kwenye sahani unakula hadi unashiba...! Siyo unakula vimatunda viwili unasema umekula matunda mkuu...!

Kuhusu maji, hakikisha unapoamka asubuhi kabla hata hujapiga mswaki unakunywa maji lita moja na nusu...! Mfano ukiamka saa kumi na mbili asubuhi basi hadi saa kumi na mbili na nusu au saa moja kamili uwe umemaliza lita moja na nusu kisha uendelee na majukumu yake...! Then kwa kipindi cha kutwa nzima hakikisha umekunywa lita moja na nusu tena ya maji...!

Fanya hivi kwa siku tatu alafu tuletee mrejesho hapa....!

Sent using Jamii Forums mobile app
---
Tabu ya kutopata choo kiurahisi

MARADHI YA KUTOPATA CHOO (CONSTIPATION):
Haya ni maradhi ambayo mgonjwa huwa hapati choo kwa wepesi. Haja kubwa inaweza kutoka baada ya siku moja au

mbili au zaidi na ikitoka huwa ni kigumu na hutoka kwa shida na wakati mwingine huwa kama cha mbuzi. Wagonjwa

wengine hupata maumivu wakati wa kwenda haja kubwa.

Mtu mwenye afya nzuri hupata haja kubwa kwa kiwango cha chini mara moja kwa siku. Na choo huwa laini na hutoka bila matatizo.

SABABU ZA MARADHI HUSIKA:
1. Upungufu wa vitamini mwilini hasa vitamin B.

2. Maradhi ndani ya utumbo mpana.

3. Kula vitu vigumu na vikavu kama vile vyakula vya ngano.

4. Upungufu wa ulaji matunda na mboga.

5. Kutokunywa maji ya kutosha.

6. Upungufu wa fibre kwenye chakula zinazopatikana kwenye maganda ya mahindi. 7)

7.Ukosefu wa kufanya mazoezi ya viungo.

TIBA:

Kanuni ya kwanza
1.Chukua glasi moja ya maziwa freshi baridi uchanganye na vijiko viwili vikubwa vya asali na kijiko kimoja kidogo cha mafuta ya habitsoda. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. Dawa hii hufanya choo kuwa laini na kupata haja kubwa kwa wepesi.

Kanuni ya pili:
2.Unga wa sanamaki kijiko kimoja kikubwa, Unga wa tangawizi kijiko kimoja kikubwa, Unga wa habasoda kijiko kimoja kikubwa, na Asali robo lita. Dawa hizi zote zichanganye pamoja kwa kukoroga kwa kijiko. Kula kijiko kimoja kutwa mara tatu.

Kanuni ya tatu:
3.Asali robo lita, na Unga wa Arki susi vijiko vinne vikubwa. Kula vijiko viwili vikubwa kutwa mara mbili.

Kanuni ya nne:
4.Kunywa kwa wingi maji ya Uvuguvugu ya kutosha na pia ule kwa wingi matunda na mboga.

Kanuni ya tano:
5.Kula kila siku asubuhi tende saba kabla ya chakula cha asubuhi. Tende hufanya choo kuwa laini. INSHAALLAH UTAPONA.

CHAGUWA TIBA MOJAWAPO KWAKO WEWE ITAKUWA NI RAHISI KUIPATA TUMIA KWAMUDA WA SIKU 3 HUKUPONA

CHUKUWA MAELEZO YA TIBA INGINE HAPO FANYA HIVYO HIVYO MPAKA UTAKAPO PONA.
---
Inashauriwa kusafisha tumbo lako walau mara moja kwa mwaka ili kujikinga na asilimia 90 ya magonjwa sugu, kwani tafiti zaonesha kuwa magonjwa mengi chanzo chake kikuu ni kutokana na sumu zilizolundikana katika utumbo mpana, kukosa choo ni dalili moja wapo, zoezi hili waweza kulifanya kwa kuamua kula matunda mengi sana yenye utembwe ama fiber au tumia Shake off Phyto fiber
kusafisha tumbo.

Pia kwa kuwa sumu hizo zinakuwa zimeingi katika mzunguko wa damu, inashauriwa kusafisha damu kwa kutumia SPLINA LIQUID Chlorophyly,

SHAKE OFF PHYTO FIBER
Our health is closely linked to the state of our intestines. When one is living an unhealthy lifestyle with poor quality of food and water, drinking and smoking, and insufficient intake of high fiber foods, he is bound to have intestinal tract crisis. The digestive tract gets clogged with fats and toxins and infested with harmful bacteria. This leads to obesity and chronic diseases such as colon cancer, arteriosclerosis, hypertension, liver and kidney diseases, diabetes and heart problems. It is important to cleanse and detoxify our intestines to maintain good health and promote longevity. Health experts have proven that fiber helps a great deal not only in keeping the digestive tract clean and healthy, but also in losing weight by giving the feeling of fullness, absorbing fat, and facilitating metabolism. Thus, we recommend Shake Off Phyto Fiber.

ACTIVE INGREDIENTS
  • PLANT FIBER Provides a feeling of fullness, and helps relieve intestinal toxins like Coprostasis. It relieves diarrhea and absorbs excess water in the intestine.
  • ROSELLE Rich in vitamin C, calcium, iron, riboflavin, niacin, fiber and has anti-oxidants that enhances the beauty of the skin.
  • OATS It acts like a sponge that absorbs the cholesterol. It is rich in bran and fiber which prevents colon cancer.
  • GARCINIA CAMBOGIA Aids in slimming as it suppresses the appetite and increases the body's metabolism. It also regulates blood sugar levels and lowers the blood cholesterol.
  • INULIN Acts as a prebiotic that stimulates the production of good bacteria such as bifidus in the intestines. It also relieves diabetes mellitus by reducing the body's need to produce insulin.

KEY CHARACTERISTICS
  • FAST & EFFECTIVE: See the results in just eight hours.
  • MARVELOUS TASTE: Shake Off comes in two delicious flavors, pandan and strawberry.

  • RELAXES WITHOUT BURDEN: Relief from toxins and excess fats result in an amazing comfort and a relaxing feeling –

View attachment 137042

Splina Liquid Chlorophyll
Edmark Splina Liquid Chlorophyll Our daily diet should consist of20% acidic and 80% alkaline food to maintain a healthy body. A healthy body should have an alkaline PH level of about 7.3 to 7.4.Diets based on acidic food will cause high acid levels in our body. In the long run, this will cause various illnesses such as diabetes, high cholesterol and stroke. To ensure your daily alkaline needs, we recommend Splina Liquid Chlorophyll.
HEALTH BENEFITS
EXCELLENT SOURCE OF NUTRIENTS It is very high in RNA and DNA and has been found to protect against the effects of UV radiation.

    • INCREASES BLOOD COUNTS Assists red blood cell generation to ensure sufficient oxygen and nutrients for cell renewal. It helps to either cool or warm the body and adapt to environmental changes.
    • BOOSTS THE IMMUNE SYSTEM Accelerates tissue cell activity and normal re-growth of cells to help the body heal faster.
    • INCREASES OXYGEN SUPPLY IN THE BLOOD This helps maintain optimum blood flow all throughout the body, and regulates blood pressure to healthy levels.
    • REDUCES WRINKLES AND AGING The results are smoother skin, clearer complexion and youthful looks.
3 MAIN FUNCTIONS
· BALANCING Balances acid-alkali levels, and enhances immunity.
· CLEANSING Cleanses the digestive system, assists in purifying blood.
· NOURISHING Splina is rich in vitamins A, C and E, Zinc, Folic Acid, Calcium, Magnesium and Iron.

View attachment 137041

VIrutubisho hivi kwa sasa vinapatikana katika maduka kadhaa ya madawa, mahitaji yamekuwa mengi, vimekuwa na msaada kwa watu wengi, waweza kuvipata RHODE PARMACY Kariakoo, mtaa wa Congo na Kipata, Core Pharmacy Mtaa wa Lindi na Congo, Grat Pharmacy Mtaa wa Kipata na Mishangu Pharmacy.

Kampuni inatafuta wadau wa kuingia nao ubia kusambaza bidhaa hizi kwa watu wengi zaidi, wasiliana na Mr Bernard 0716927070. Inatoa punguzo kubwa kwa wenye maduka ya madawa ikiwa ni pamoja na bonasi ya gari na nyumba pia.
---
Tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu ni jambo tunalolikwepa kwenye mazungumzo yetu ya kila siku. Hata hivyo ni tatizo kubwa katika jamii na mbaya zaidi wengi hawajuwi madhara yake ni nini ya kuendelea kulivumilia tatizo hili.

Kupata choo kigumu au kufunga choo ni ishara ya tatizo lingine baya zaidi mwilini. Kama kuna jambo unapaswa uliepuke kwa nguvu zote basi ni hili. Kwa afya bora kabisa hakikisha unapata choo kila siku mara 2 hata mara 3.

Choo kilaini siyo kigumu na chenye maumivu. Wakati mwingine utakapopata tatizo hili naomba usiwe na aibu kulisema wazi hata kwa boss wako ili upate matibabu kwa haraka. Kufunga choo au kupata choo kigumu ndiyo CHANZO KIKUU CHA UGONJWA WA BAWASIRI kwa waTanzania wengi na hii inachangiwa kwa sehemu kubwa kwa kula ugali wa sembe na kutokunywa maji mengi kila siku. Pamoja na hayo, hakuna ugonjwa rahisi kutibika kama huu ikiwa utaamua kushughulisha kichwa chako kidogo hasa kwa kuangalia unakula na kunywa nini kila siku.

Dawa mbadala 10 zinazotibu kufunga choo au choo kigumu:

1. Mafuta ya Zeituni Mafuta ya zeituni (olive oil) yanatosha kutibu hili tatizo.
Yana radha nzuri mdomoni na ni dawa pia. Kama unaweza yafanye pia kama mafuta yako ya kupikia vyakula vyako mbalimbali, mafuta haya huweza kuliwa pia bila kupitishwa kwenye moto na hivyo ni mafuta mazuri kuweka kwenye kachumbari au saladi mbalimabali.

Matumizi: Chukua kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya zeituni changanya na kijiko kidogo kimoja cha chai cha maji maji ya limau na unywe asubuhi ukiamka tu tumbo likiwa bado tupu. Fanya hivi kila siku mpaka utakapopona.

2. Juisi ya Limau
Juisi ya limau inatumika kutibu tatizo la kupata choo kigumu au kufunga choo.
Chukua maji maji ya limau kutoka katika limau kubwa 3 na uchanganye na juisi ya matunda kupata kikombe kimoja (ml 250) na unywe yote kutwa mara 1 kila siku kwa siku kadhaa mpaka umepona. Ukiacha hilo la kutibu kufunga choo limau ina vitamini C nyingi na hivyo itakuongezea kinga yako ya mwili kwa haraka zaidi (usizidishe hata hivyo).

3. Mazoezi ya kutembea
Kama unataka kupata choo kilaini na cha kawaida basi jitahidi uwe mtu wa kutembeatembea na si kukaa tu kwenye kiti kutwa nzima. Maisha yetu ya kisasa na kazi za ofisini zinatulazimisha kuwa watu wa kukaa kwenye kiti masaa mengi wengine huamua tu kukaa kwenye kiti sebureni akiangalia TV asubuhi mpaka jioni!.

Aina hii ya maisha ni hatari zaidi kwa afya zetu kuliko hata madawa ya kulevya. Jitahidi kila siku uwe unapata muda wa kutembeatembea kwa miguu mpaka dakika 60 au zaidi. Hii itakusaidia kuondoa tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.

4. Vyakula vya nyuzinyuzi (fiber)
Mara nyingi utasikia watu wakisisitiza juu ya umhimu wa kula vyakula vya asili na vyenye nyuzinyuzi. Chakula cha asili kina nafasi kubwa katika kuimarisha afya yako kwa ujumla. Kinachonishangaza ni kuona watu bado wanaendelea kula ugali wa sembe ilihali inajulikana wazi ugali mweupe ndiyo chanzo kikuu cha kupata choo kigumu ikiwemo ugonjwa wa bawasiri.

Ninakusihi sana uanze kula ugali wa dona kuanzia sasa na kuendelea. Hakikisha pia asilimia 80 ya mlo wako kwa siku ni matunda na mboga za majani. Matunda kama ndizi na parachichi ni mhimu ule kila siku kadharika tumia unga au mbegu za maboga.

5. Mshubiri (Aloe Vera)
Mshubiri unajulikana wazi kwa kutibu tatizo hili la kufunga choo au kupata choo kigumu. Ni mhimu utumie mshubiri fresh kabisa kutoka kwenye mmea moja kwa moja kuliko kutumia za dukani au za kwenye makopo. Usitumie zaidi ya vijiko vikubwa viwili vya jeli ya shubiri kwa siku.

Matumizi: Changanya vijiko vikubwa viwili vya jeli ya aloe vera ndani ya kikombe kimoja cha juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani (hasa juisi ya parachichi) na unywe yote kutwa mara 1 hasa nyakati za usiku unapokaribia kwenda kulala kwa siku kadhaa au mpaka umepona.

6. Baking soda Baking soda ni dawa nyingine ya asili nzuri kwa tatizo hili. Inafanya kazi vizuri kwa zaidi ya asilimia 95. Sababu ya bicarbonate iliyomo ndani yake itakusaidia kupumua nje vizuri gesi au hewa yoyote ilisongamana ndani ya tumbo pia inasaidia kupunguza asidi mwilini. Baking soda ni ile wamama huitumia katika kupika maandazi au mikate inapatikana katika maduka ya kawaida hata hapo nje kwa Mangi ipo.

Matumizi: -Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha baking soda ndani ya nusu kikombe cha maji ya uvuguvugu (ml 125) na unywe yote kwa haraka kutwa mara 1 kwa siku 7 hivi au unaweza kuacha siku yoyote kabla kama tatizo litakuwa limeisha.

7. Mtindi
Unahitaji bakteria wazuri zaidi wakati huu unapokabiliwa na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu. Utahitaji pia kuacha kula vyakula vya kwenye makopo (processed sugars and foods). Namna rahisi kabisa ya kuhakikisha mwili wako unapata bakteria wazuri ni kwa kutumia mtindi. Tumia mtindi wowote ule uliotengeneza mwenyewe nyumbani au hata wa dukani (ila wa dukani usiwe umeongezwa vitu vingine ndani yake – sweetened yogurt).

Matumizi: Kunywa kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi wakati wa chakula cha asubuhi na kikombe kingine usiku unapoenda kulala kwa wiki 1 hata 2.

8. Fanya mazoezi ya kusimama na kuchuchumaa (squat)
Fanya mazoezi ya kuchuchumaaa na kusimama (squatting). Hili ni zoezi mhimu kwa mtu anayesumbuliwa na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana. Fanya kuchuchumaa na kusimama mara 25 na upumzike dakika 1 kisha unaendelea tena unachuchumaa na kusimaa hivyo hivyo mara 25 kwa mizunguko mitano (5 rounds) huku ukipumzika dakika 1 kila baada ya mzunguko mmoja.

Fanya zoezi hili kila siku mara 1 na usizidishe sana, ni mara 25 kwa mizunguko mitano inatosha na uzuri ni kuwa unaweza kufanya zoezi hili mahali popote. Wakati huo huo unashauriwa kutumia choo cha kuchuchumaa yaani vile vyoo vya zamani na siyo hivi vya kisasa vya kukaa kama vile upo ofisini. Vyoo hivi vya kukaa ndiyo moja ya vitu vinavyochangia upate pia ugonjwa wa bawasiri (kuota kinyama sehemu ya haja kubwa na kupata maumivu wakati unajisaidia).

9. Matunda
Asilimia 80 ya chakula chacko kwa siku iwe ni matunda na mboga za majani. Unapoumwa na hili tatizo pendelea zaidi parachichi, papai na juisi ya ukwaju. Kula matunda siyo mpaka uumwe au ushauriwe na daktari, fanya kuwa ndiyo tabia yako kila siku na hutakawia kuona mabadiliko makubwa kwa afya yako kwa ujumla.

10. Maji ya Kunywa Maji ni uhai.
Asilimia 75 ya mwili wako ni maji. Asilimia 85 za ubongo wako ni maji. Asilimia 94 ya damu yako ni maji. Hakuna maisha bila maji. Inashangaza sana kuona mtu anamaliza siku nzima au hata siku 2 hajanywa maji! Kama wewe si mpenzi wa kunywa maji ya kutosha kila siku SAHAU KUWA NA AFYA NZURI MAISHANI MWAKO.

Hakikisha unakunywa maji kila siku lita 2 mpaka 3, kidogo kidogo kutwa nzima bila kusubiri kiu na hutaugua tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu. Dawa nyingine nzuri kwa ajili hii ni unga wa mbegu za mlonge

Sent using Jamii Forums mobile app

KWA UTATUZI WA TATIZO HILI KWA WATOTO WADOGO NA VICHANGA SOMA:
- Tatizo la ukosefu wa haja kubwa kwa watoto wadogo na Vichanga. Fahamu chanzo chake na namna ya kutibu - JamiiForums
 
Kama na kanyama kameisha anza kutoka ni hatari jiandae kufanyiwa oparesheni za mar kwa mara. huo ugonjwa unaitwa ugonjwa wa kuganda kwa choo (Hemoroids) kama sijakosea mimi sio dk. ila nina ufahamu kidogo kwa tatizo lako. mambo ambayo yamepelekea upatwe na tatizo hilo ni pamoja na:

1. kula sana vyakula vya nafaka vilivyokobolewa bila other vitamins zipatikanazo kwenye matunda na mbogamboga.
2. kutokupenda kunywa maji mengi i.e bilauli nane kwa siku.
3. kupendelea kula sana vyakula vya nyamanyama hasa nyekundu. na pengine kula bila mtiririko yaani masaa maalumu ya kula na pia kula usiku sana saa 3 usiku, nne .... na mengineyo ambayo wataalamu wanayajua.

hali hiyo imekupelekea mfumo wa usagaji chakula tumboni mwako kutokuwa mzuri na mara nyingi kuwa na gesi tumboni, kutokujisikia kula kwa kujua umeshiba, kufunga choo na ukienda kigumu ka cha mbuzi. na matatizo mengi yatokanayo. na hizo dawa u nazotumia zinakupa nafuu lakini kutumia dawa kwa kila mara sumu zinazidi kulundikana mwilini kwa sababu kufunga choo maana yake uchafu hautoki nje unabaki ndani.

Cha kufanya jaribu kubadili mwenendo wa maisha yako kwa kujaribu haya.
1. Pendelea kula vyakula visivyo kobolewa kama ngano na ugali wa dona au uji wa dona.
2. Katika maisha yako yote duniani kila siku jitahidi kunywa maji safi na salama bilauli zisizopungu nane au kumi na mbili kwa siku kutokana na muda wa utazigawa katika masaa ambayo ni muafaka kwako.
3. kula matunda kwa wingi kama mapapai, mananasi, embe n.k pia mboga za majani kwa wingi zingatia uandaaji wa mboga za majani kwa afya na virutubisho katika mwili.

4. Jitahidi kula chakula cha usiku mapema iwezekanavyo tena kisiwe kigumu sana.

5. Kwa kuanza kujitibu mwenyewe nyumbani tumia Juis ya ukwaju glass mbili mara tatu kwa siku angalau kwa siku tatu mpaka tano mfululizo. jinsi ya kutengeneza chukua ukwaju kg 1 loweka katika maji ya moto uliyochemsha mikono yako ikiwa safi fikicha huo ukwaju upate juis nzito kisha changanya na asali mbichi (glass 1 kijiko kimoja cha asali kikubwa) kisha tumia hiyo juis yake. Kama una vidonda vya tumbo pengine ukwaju hutauweza jaribu kuchemsha bamia bila kuziunga pengine weka chunvi kidogo kwa ajili ya ladha kisha saga kwenye blenda unywe.

6. Punguza kula mikate mikate na maandazi ya kwenye bekari ukiweza tengeneza mwenyewe vifungua kinywa kama viazi mchemsho mihogo n.k.

7. Punguza mafuta mengi kwenye vyakula unavyokula hasa nyama na na mafuta unayotumia yawe yale ya mimea. Nafikiri ukifuata ushauri utaona mabadiliko ingawa sijamaliza yote ilahaya ni ya muhimu.

Pia kuna thread humu ilikuwepo ya mtu mwenye tatizo kama lako jaribu kuitafuta utaona ushauri mwingi uliotolewa wenye faida.
 
UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida.

Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu.

Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?

Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa.

Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

NINI HUSABABISHA TATIZO?

Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

NINI KIFANYIKE?

Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo:

Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda Choo. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi.

Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil' muda mfupi kabla ya kwenda kulala.

Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate mweupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.
 
Hii ni ''constipation'',na constipation ndiyo chanzo cha magonjwa yote duniani.

Daktari atakueleza ufanye nini. Tatizo ni maji tu. Kunywa maji ya kutosha kusaidia peristalisis. Ukikaa muda mrefu sana,hii pia inaongeza constipation. Kama kazi yako ni kazi katika desk,basi uwe mwangalifu,na ufahamu unahitaji kufanya marekebisho baadaye.

Usinywe uji wa aina yoyote. Sijui kwa nini hyo mtu anakushari kunywa uji. Hiyo itakuongezea tu constipation. Kunywa ukwaju,hii ni bitter drink. Ukwaju,ndimu,limau,vitu kama hivi vitasaidia vipi? Labda kama short-term solution,unatumia hii acidic diet kusaidia digestion.

Kula vyakula laini,kama ugali lazima upikwe kiaina,uwe laini. Kama ukienda South Africa,utaona katika magenge yao ya chakula wanapika ugali laini kuliko wanavyopika hapa Tanzania.

You must be alert. Kama unaanza kuona dalili za constipation,nenda kafanye jogging. Kwa sababu ukichelewa sana,it may be too late.
 
Hiyo ni Constipation ndugu yangu. Kikubwa ni kuwa unahitaji chakula chenye "dietary fibers" kama vila Dona, mboga za majani na matunda. Fanya utaratibu wa kupata matunda na mboga za majani kila siku pamoja na kunywa maji mengi. Punguza kula nyama na badala yake pendelea protein za kutoka kwenye mimea kama vile soya, mbaazi, maharage, choroko, njegere. Jaribu hivi kwa muda wa wiki mbili, utaanza kuona mabadiliko chanya. Kama hutapata mabadiliko, basi, constipation yako inahitaji utalaam zaidi.
 
Pole sana ndg yangu hata mimi nimejifunza mengi sana humu kwani hata kama sijui sasa nimejifunza na nitajitahizi.

Tatizo lako kweli ni hatari na linawakumba wengi sana. Mimi mwenyewe sipendi kabisa kunywa maji naweza kaa hata siku 3 bila kunywa maji na kuhusu mboga za majani ndio sipendi kabisa hivyo kabla sijaingia katika dozi hizo bora nianze kuepukana na hatari hiyo.
 
Mpenzi wa Nyama Choma/Kukaanga?
Punguza matumizi hayo hasa kama chakula kikuu. Ongeza kula maembe, mapapai na Avocado
Ongeza kunywa maji hasa baada na kabla ya kula.
 
Nisaidieni dawa ya kuniwezesha kupata choo cha kawaida,maana ni miaka sasa imepita nimekuwa na hili tatizo la kuwa na choo kigumu kiasi kwamba nasikia haja kubwa na nikienda ****** kujisaidia napata taabu sana..

Nilienda hospitali kumuona daktari akanipatia dawa nikazitumia na zilinisaidia sana na akaniambia ninywe sana maji na kwa kweli sasa ivi nakunywa sana maji...

Nikikaa baada ya mda ilo tatizo huwa linanirudia nikinywa dawa huwa linaisha mimi ni mtu wa kunywa dawa....

Imefikia hatua kale kanyama kwenye haja kubwa kametokeza kwa sababu ya kupata taabu wakati wa haja..

Nisaidieni wanajamii wenzangu jinsi ya kuepukana na hili tatizo maana limekuwa kama ni sehemu ya maisha yangu naona kama litakuja kuniletea madhara makubwa mno...
ahahahahahah ndiyo maana umekuwa bonge, kun.ia huwezi.
kwenye bold hiyo ni ndyamgongo
 
I feel like Zitto Kabwe: nimepewa sumu ya chakula.

Nina kichefuchefu usiku mzima na nina incontinence lakini asubuhi nina mkutano muhimu, siwezi kuacha kuhudhuria na siwezi kwenda kuachia matapishi ghafla kwenye business roundtable.

Ni kitu gani naweza kunywa/kula kikaondoa kichefuchefu na kutapika?

Shukrani za dhati.
 
wewe ni wa jinsia ipi? maana yake umetaja kichefu chefu!
Itawasaidia watoa msaada katika kujikita na eneo la majibu yao.
 
Papai na parachichi kwa wingi. viazi na mboga zenye nyuzinyuzi (roughages) kama kabichi na spinarch ndio ushauri mwepesi. Kunywa maji kwa kwenda mbele. Hicho kichefuchefu kapime mimba. ukiona hali inazidi kamwone daktari.
 
I feel like Zitto Kabwe: nimepewa sumu ya chakula.

Nina kichefuchefu usiku mzima na nina incontinence lakini asubuhi nina mkutano muhimu, siwezi kuacha kuhudhuria na siwezi kwenda kuachia matapishi ghafla kwenye business roundtable.

Ni kitu gani naweza kunywa/kula kikaondoa kichefuchefu na kutapika?

Shukrani za dhati.
Mkuu kwanza utuambie wewe ni nani Mwanamke au Mwanamme? kisha kichwa chako cha habari umesema unataka Dawa ya kutibu ( Constipation Kuvimbiwa) Sasa hayo Maradhi ya kuvimbiwa hayahusiani

na kupewa sumu ya chakula. hayo maradhi ya Kuvimbiwa na tumbo yanweza kuhusiana na hayo Maradhi uliyoyataja mwisho yaani Maradhi ya kichefuchefu na kutapika? sasa tuambiwe kwanza ukweli wako tujuwe wewe ni Male/Female, kisha utuambie una ugonjwa gani ili tuweze kujuwa namna ya kukupa Dawa Asante
 
I feel like Zitto Kabwe: nimepewa sumu ya chakula.

Nina kichefuchefu usiku mzima na nina incontinence lakini asubuhi nina mkutano muhimu, siwezi kuacha kuhudhuria na siwezi kwenda kuachia matapishi ghafla kwenye business roundtable.

Ni kitu gani naweza kunywa/kula kikaondoa kichefuchefu na kutapika?

Shukrani za dhati.

Nakupa mimi huduma ya Kwanza Tumia Matumizi ya kinywaji laini ukwaju katika

kesi ya shinikizo la damu, kutapika,

kichefuchefu na maumivu ya kichwa.

Faida za ukwaju
 
I feel like Zitto Kabwe: nimepewa sumu ya chakula.

Nina kichefuchefu usiku mzima na nina incontinence lakini asubuhi nina mkutano muhimu, siwezi kuacha kuhudhuria na siwezi kwenda kuachia matapishi ghafla kwenye business roundtable.

Ni kitu gani naweza kunywa/kula kikaondoa kichefuchefu na kutapika?

Shukrani za dhati.

Majivu ya jiko la kuni kutwa mara tatu, robo kijiko cha chai.

Hakikisha madaktari bingwa nchi hawapati dawa hii ya siri wasije wakaichakachua, sawa??
 
Kuna majani yanaitwa Zaatari, chemsha unywe

Kwa wale ambao tumbo hujaa upepo na kuuma mnaweza kunywa maji ya moto yaliyochanganywa na asali
 
I feel like Zitto Kabwe: nimepewa sumu ya chakula.

Nina kichefuchefu usiku mzima na nina incontinence lakini asubuhi nina mkutano muhimu, siwezi kuacha kuhudhuria na siwezi kwenda kuachia matapishi ghafla kwenye business roundtable.

Ni kitu gani naweza kunywa/kula kikaondoa kichefuchefu na kutapika?

Shukrani za dhati.

Hiyo heading ni kama haiendani na contents zako. Navyojua constipation ni pamoja na kukosa choo, kuvimbiwa n.k. Sasa hayo ya kichefuchefu yanatoka wapi? ndio maana umeulizwa JINSI yako ili upewe dawa mrua.
Kama ni constipation peke yake kunywa maji kwa wingi kuvimbiwa kutapungua na utapata choo.
 
Kwanza kabisa, tungependa kujua jinsia yako. Pili, kichwa cha habari ni constipation ambayo kitaalamu ni matatizo yanayotokana na choo,ima kuwa kigumu au kutopata kwa wakati mwafaka. Incontinence ni tatizo linalohusu njia ya mkojo, mfano mtu akiwa hapati mkojo kwa flow ya kawaida hiyo ndiyo maana yake. Kwa ufupi ukisema constipation unamaanisha matatizo ya choo, na unapotaja incontinence una maanisha matatizo ya mkojo(urine incontinence).

Kama una constipation nakushauri upate vyakula vyenye fiber nyingi kama nyama, ule matunda kama mapapai, ndizi mbivu n.k. Kama utakula chungwa basi ule na ''nyama'' zake ili zisaidie kama source ya fibers. Usisahau kunywa maji mara kwa mara na epuka vitu kama mikate mikavu isiyo na siagi.

Kichefu chefu ni dalili ya tatizo na si ugonjwa, kinaweza kuwa kimesababishwa na chakula na kwa akina mama hormonal changes. Vinginevyo maelezo yako hayajatupa nafasi ya kukusaidia zaidi kwasababu yanajichanganya.
Nakutakia afya njema.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom