Tatizo la kupata choo kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la kupata choo kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation)

Discussion in 'JF Doctor' started by JamiiForums, Mar 7, 2010.

 1. JamiiForums

  JamiiForums Official Robot Staff Member

  #1
  Mar 7, 2010
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 5,090
  Likes Received: 2,221
  Trophy Points: 280  ===========

  UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida. Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

  Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu. Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

  Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

  MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?
  Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa. Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

  NINI HUSABABISHA TATIZO?
  Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

  NINI KIFANYIKE?
  Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo: Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda msalani. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi. Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

  Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil' muda mfupi kabla ya kwenda kulala. Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.


  =======

  Kukosa choo kwa watoto wadogo

  =========

   
 2. D

  Deck Joel Member

  #2
  Dec 1, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Pole sana mkuu, bila shaka hapa kuna wataalam watakusaidia.
   
 3. B

  Brandon JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 336
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  pole sana. Jitahidi unywe juisi ya ukwaju mara tatu kwa siku glass moja.
   
 4. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  he kama na kanyama kameisha anza kutoka ni hatari jiandae kufanyiwa oparesheni za mar kwa mara. huo ugonjwa unaitwa ugonjwa wa kuganda kwa choo (Hemoroids) kama sijakosea mimi sio dk. ila nina ufahamu kidogo kwa tatizo lako. mambo ambayo yamepelekea upatwe na tatizo hilo ni pamoja na
  1. kula sana vyakula vya nafaka vilivyokobolewa bila other vitamins zipatikanazo kwenye matunda na mbogamboga.
  2. kutokupenda kunywa maji mengi i.e bilauli nane kwa siku.
  3. kupendelea kula sana vyakula vya nyamanyama hasa nyekundu. na pengine kula bila mtiririko yaani masaa maalumu ya kula na pia kula usiku sana saa 3 usiku, nne .... na mengineyo ambayo wataalamu wanayajua.

  hali hiyo imekupelekea mfumo wa usagaji chakula tumboni mwako kutokuwa mzuri na mara nyingi kuwa na gesi tumboni, kutokujisikia kula kwa kujua umeshiba, kufunga choo na ukienda kigumu ka cha mbuzi. na matatizo mengi yatokanayo. na hizo dawa u nazotumia zinakupa nafuu lakini kutumia dawa kwa kila mara sumu zinazidi kulundikana mwilini kwa sababu kufunga choo maana yake uchafu hautoki nje unabaki ndani.

  Cha kufanya jaribu kubadili mwenendo wa maisha yako kwa kujaribu haya.
  1. Pendelea kula vyakula visivyo kobolewa kama ngano na ugali wa dona au uji wa dona.
  2. Katika maisha yako yote duniani kila siku jitahidi kunywa maji safi na salama bilauli zisizopungu nane au kumi na mbili kwa siku kutokana na muda wa utazigawa katika masaa ambayo ni muafaka kwako.
  3. kula matunda kwa wingi kama mapapai, mananasi, embe n.k pia mboga za majani kwa wingi zingatia uandaaji wa mboga za majani kwa afya na virutubisho katika mwili.

  4. Jitahidi kula chakula cha usiku mapema iwezekanavyo tena kisiwe kigumu sana.

  5. Kwa kuanza kujitibu mwenyewe nyumbani tumia Juis ya ukwaju glass mbili mara tatu kwa siku angalau kwa siku tatu mpaka tano mfululizo. jinsi ya kutengeneza chukua ukwaju kg 1 loweka katika maji ya moto uliyochemsha mikono yako ikiwa safi fikicha huo ukwaju upate juis nzito kisha changanya na asali mbichi (glass 1 kijiko kimoja cha asali kikubwa) kisha tumia hiyo juis yake. Kama una vidonda vya tumbo pengine ukwaju hutauweza jaribu kuchemsha bamia bila kuziunga pengine weka chunvi kidogo kwa ajili ya ladha kisha saga kwenye blenda unywe.

  6. Punguza kula mikate mikate na maandazi ya kwenye bekari ukiweza tengeneza mwenyewe vifungua kinywa kama viazi mchemsho mihogo n.k.

  7. Punguza mafuta mengi kwenye vyakula unavyokula hasa nyama na na mafuta unayotumia yawe yale ya mimea. Nafikiri ukifuata ushauri utaona mabadiliko ingawa sijamaliza yote ilahaya ni ya muhimu.

  Pia kuna thread humu ilikuwepo ya mtu mwenye tatizo kama lako jaribu kuitafuta utaona ushauri mwingi uliotolewa wenye faida.
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida.

  Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

  Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu.

  Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

  Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

  MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?

  Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa.

  Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

  NINI HUSABABISHA TATIZO?

  Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

  NINI KIFANYIKE?

  Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo:

  Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda Choo. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi.

  Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

  Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil' muda mfupi kabla ya kwenda kulala.

  Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.
   
 6. B

  Bongemzito Senior Member

  #6
  Dec 2, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru mno mkuu kwa ushauri wako nimekuelewa sana,juisi ya ukwaju nilikuwa siipendi ila sasa ntaanza kuinywa
   
 7. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #7
  Dec 2, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Hii ni ''constipation'',na constipation ndiyo chanzo cha magonjwa yote duniani.

  Daktari atakueleza ufanye nini. Tatizo ni maji tu. Kunywa maji ya kutosha kusaidia peristalisis. Ukikaa muda mrefu sana,hii pia inaongeza constipation. Kama kazi yako ni kazi katika desk,basi uwe mwangalifu,na ufahamu unahitaji kufanya marekebisho baadaye.

  Usinywe uji wa aina yoyote. Sijui kwa nini hyo mtu anakushari kunywa uji. Hiyo itakuongezea tu constipation. Kunywa ukwaju,hii ni bitter drink. Ukwaju,ndimu,limau,vitu kama hivi vitasaidia vipi? Labda kama short-term solution,unatumia hii acidic diet kusaidia digestion.

  Kula vyakula laini,kama ugali lazima upikwe kiaina,uwe laini. Kama ukienda South Africa,utaona katika magenge yao ya chakula wanapika ugali laini kuliko wanavyopika hapa Tanzania.

  You must be alert. Kama unaanza kuona dalili za constipation,nenda kafanye jogging. Kwa sababu ukichelewa sana,it may be too late.
   
 8. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #8
  Dec 2, 2010
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,738
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Hiyo ni Constipation ndugu yangu.
  Kikubwa ni kuwa unahitaji chakula chenye "dietary fibers" kama vila Dona, mboga za majani na matunda. Fanya utaratibu wa kupata matunda na mboga za majani kila siku pamoja na kunywa maji mengi. Punguza kula nyama na badala yake pendelea protein za kutoka kwenye mimea kama vile soya, mbaazi, maharage, choroko, njegere. Jaribu hivi kwa muda wa wiki mbili, utaanza kuona mabadiliko chanya. Kama hutapata mabadiliko, basi, constipation yako inahitaji utalaam zaidi.
   
 9. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #9
  Dec 2, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Pole sana ndg yangu hata mimi nimejifunza mengi sana humu kwani hata kama sijui sasa nimejifunza na nitajitahizi......

  Tatizo lako kweli ni hatari na linawakumba wengi sana. Mimi mwenyewe sipendi kabisa kunywa maji naweza kaa hata siku 3 bila kunywa maji na kuhusu mboga za majani ndio sipendi kabisa hivyo kabla sijaingia katika dozi hizo bora nianze kuepukana na hatari hiyo.
   
 10. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mpenzi wa Nyama Choma/Kukaanga?
  Punguza matumizi hayo hasa kama chakula kikuu. Ongeza kula maembe, mapapai na Avocado
  Ongeza kunywa maji hasa baada na kabla ya kula.
   
 11. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #11
  Dec 6, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  ahahahahahah ndiyo maana umekuwa bonge, kun.ia huwezi.
  kwenye bold hiyo ni ndyamgongo
   
 12. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  I feel like Zitto Kabwe: nimepewa sumu ya chakula.

  Nina kichefuchefu usiku mzima na nina incontinence lakini asubuhi nina mkutano muhimu, siwezi kuacha kuhudhuria na siwezi kwenda kuachia matapishi ghafla kwenye business roundtable.


  Ni kitu gani naweza kunywa/kula kikaondoa kichefuchefu na kutapika?

  Shukrani za dhati.
   
 13. N

  Nonda JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  wewe ni wa jinsia ipi? maana yake umetaja kichefu chefu!
  Itawasaidia watoa msaada katika kujikita na eneo la majibu yao.
   
 14. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  papai na parachichi kwa wingi. viazi na mboga zenye nyuzinyuzi (roughages) kama kabichi na spinarch ndio ushauri mwepesi. Kunywa maji kwa kwenda mbele. Hicho kichefuchefu kapime mimba. ukiona hali inazidi kamwone daktari.
   
 15. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwanza utuambie wewe ni nani Mwanamke au Mwanamme? kisha kichwa chako cha habari umesema unataka Dawa ya kutibu ( Constipation Kuvimbiwa) Sasa hayo Maradhi ya kuvimbiwa hayahusiani

  na kupewa sumu ya chakula. hayo maradhi ya Kuvimbiwa na tumbo yanweza kuhusiana na hayo Maradhi uliyoyataja mwisho yaani Maradhi ya kichefuchefu na kutapika? sasa tuambiwe kwanza ukweli wako tujuwe wewe ni Male/Female, kisha utuambie una ugonjwa gani ili tuweze kujuwa namna ya kukupa Dawa Asante
   
 16. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #16
  Jan 19, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Nakupa mimi huduma ya Kwanza Tumia Matumizi ya kinywaji laini ukwaju katika

  kesi ya shinikizo la damu, kutapika,

  kichefuchefu na maumivu ya kichwa.


  Faida za ukwaju
   
 17. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #17
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Majivu ya jiko la kuni kutwa mara tatu, robo kijiko cha chai.

  Hakikisha madaktari bingwa nchi hawapati dawa hii ya siri wasije wakaichakachua, sawa??
   
 18. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kuna majani yanaitwa Zaatari, chemsha unywe

  Kwa wale ambao tumbo hujaa upepo na kuuma mnaweza kunywa maji ya moto yaliyochanganywa na asali
   
 19. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #19
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Hiyo heading ni kama haiendani na contents zako. Navyojua constipation ni pamoja na kukosa choo, kuvimbiwa n.k. Sasa hayo ya kichefuchefu yanatoka wapi? ndio maana umeulizwa JINSI yako ili upewe dawa mrua.
  Kama ni constipation peke yake kunywa maji kwa wingi kuvimbiwa kutapungua na utapata choo.
   
 20. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #20
  Jan 19, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,220
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  Kwanza kabisa, tungependa kujua jinsia yako. Pili, kichwa cha habari ni constipation ambayo kitaalamu ni matatizo yanayotokana na choo,ima kuwa kigumu au kutopata kwa wakati mwafaka. Incontinence ni tatizo linalohusu njia ya mkojo, mfano mtu akiwa hapati mkojo kwa flow ya kawaida hiyo ndiyo maana yake. Kwa ufupi ukisema constipation unamaanisha matatizo ya choo, na unapotaja incontinence una maanisha matatizo ya mkojo(urine incontinence).
  Kama una constipation nakushauri upate vyakula vyenye fiber nyingi kama nyama, ule matunda kama mapapai, ndizi mbivu n.k. Kama utakula chungwa basi ule na ''nyama'' zake ili zisaidie kama source ya fibers. Usisahau kunywa maji mara kwa mara na epuka vitu kama mikate mikavu isiyo na siagi.
  Kichefu chefu ni dalili ya tatizo na si ugonjwa, kinaweza kuwa kimesababishwa na chakula na kwa akina mama hormonal changes. Vinginevyo maelezo yako hayajatupa nafasi ya kukusaidia zaidi kwasababu yanajichanganya.
  Nakutakia afya njema.
   
Loading...