Tatizo la kupata choo kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation). Fahamu chanzo na tiba yake

Nimetoka kununua huu ubuyu + ukwaju nataka nitengeneze juice yake, ntaleta mrejesho ahsantee
Kama utatumia ukwaju+ ubuyu.

Unachotakiwa kufanya Asubuh usile chochote kunywa jwisi peke yake tena yakutosha. Baada ya hapo subir mpaka kwenye saa 7 mchana ndio upige msosi tena ikibid usile wanga kabisa. Samaki changanya nanasi papai na chungwa. Ukimaliza jioni kunywa jwisi pekee ukalale.
Ukifanya hivyo tatizo lisipo isha wahi mapema kamuone daktari aliye karibu nawe.
 
Nenda kwenye Duka za dawa za asili maduka mengi yanapatikana msikitini.ukifika agiza abalt mulk tumia punje tatu tuu.na usiende kazini ck hiyo
 
Minyoo ya ulaya ,unamaanisha ya kwetu bongo ni sugu ?inabidi ipate dawa heavy, inawezekana nimesahau jina lake, after 3 months ntatumia hiyo "Ketrax" mkuu ,thank youu
Ila jitahidi sana, wala hii si utani. Na vidawa vyenyewe dozi wanauza buku au 1500 sasa mtu akiona ya ulaya 5000 anadharau hii. Mimi zamani ndo nilikuwa mhanga wa hii mpaka nilipookoka kutoka kwenye huo ushamba.
 
Apo tatizo ni mfumo mzima wa umeng'enyaji chakula na vyakula unavokula. Mcheki Dr Boaz Mkumbo MD mzee wa sayansi ya mapishi instagram, uko utapata ufumbuzi wa tatizo lako bila shaka.
 
Tumia juice ya ukwaju changanya na ubuyu weka sukari kidogo.

View attachment 1285328
Mrejesho wangu kwenye hili :

Jumatatu jioni nilitengeza hii juice ya ukwaju + ubuyu sikuweka kitu kingine chochote, nimekunywa glass kama 3 hivi,ni chachu hizo meno yananiuma hadi Leo yaani. Nikawa standby kwenda washroom kwa lolote litakalotokea (kudrive) , kimya nusu saa kimya lisaa mmh, nikalala nasubiri, usiku nikashtuka tumbo linauma na linaunguruma kama minyoo hivi, nikaamka kwanda toilet hamna kitu kabisa mpaka asubuhi hamna kitu,

Siku ya 2 nilivyotoka mihangaikoni tena nikanywa juice kama nusu lita hivi ,for real hii siku ndiyo hata sikusikia kuumwa tumbo yaani kama sijanywa chochote aisee, sijui nilikwama wapi jamani.
20191209_190314.jpg
20191209_172237.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu nashukuruni sana kwa maoni yenu mazuri kuhusu suala nililolileta kwenu,naendelea vizuri sasa, kilichonisaidia ni matunda+kunywa maji mengi zaidi, nakula zaidi papai,embe,chungwa, parachichi, na nimepunguza kula wali,Ugali,(chipsi sijaacha kabisa hizi,nimepunguza tu kwakweli)

Nashukuru sasa hata nikienda maliwatoni inakua fresh japo siyo sana ila tofauti na mwanzo, na natumai ntazidi kuona matokeo mazuri, mbarikiwe sana wote, I love you jf.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom