Tatizo la kupata choo kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation). Fahamu chanzo na tiba yake

Wadau,

Nna mdogo wangu wa kiume kwa mda sasa anasumbuliwa na taizo la kukosa choo, kupata choo kwa shida ama kupata choo aina ya mharo kidogo mara kwa mara. alishauriwa atumie papai pamoja na mbogamboga lakini bado tatizo lipo?Kuna mtu anasema eti ana chango.

  • Jee chango ni nini?
  • Kuna uhusiano gani kati ya chango na ngiri na tatizo la kutopata choo?
  • Jee atumie dawa wanazotangaza waganga wengi walioibuka hivi karibuni kwamba wanatibu matatizo hayo mf. ngiri, constipation (bahusi zina side effects)
  • Naamini nitapata majibu ya haya maswali hapa jamvini.
 
Tatizo la kukosa choo watoto wadogo au kuwa na choo kigumu na jinsi ya kulitatua
Watoto wadogo hasa wale ambao bado wananyonya na ndio kwanza wamenzishwa vyakula vinginevyo zaidi ya maziwa, mara nyingi hupatwa na choo kigumu au kukosa choo kabisa hali tunayoiita kimombo, constipation. Hali hiyo huanza pale mtoto anapoachishwa maziwa ya mama na kuanza kunyweshwa maziwa ya kopo au mengineyo au pia anapoanzishwa kula vyakula vingine zaidi ya maziwa. Mara nyingi watoto wanaonyonya maziwa ya mama huwa hawasumbuliwa na tatizo hilo, bali tatizo hilo huanza kujitokeza pale wanapoanza kulishwa vyakula vingine zaidi ya maziwa ya mama. Pia mama ambaye tayari mwenyewe anasumbuliwa na tatizo la kukosa choo, huenda mwanae pia akasumbuliwa na tatizo hilo.
Mtoto mwenye tatizo la kukosa choo huwa anapata choo wa shida huku akisumbuliwa na tumbo na kupata choo kigumu. Wakati mwingine hulia wakati akipata choo huku akijiminya na kukunja uso. Muone daktari iwapo mtoto ana umri wa chini ya mwezi mmoja na hajapata choo kwa siku 4.
Iwapo mtoto wako mchanga au mdogo ana tatizo la kukosa choo au kupata choo kigumu kwanza wasiliana na daktari au mpeleke hospitalini ili upate ushari wa daktari. Pia unashauriwa kujaribu njia zifuatazo:

1. Jaribu kumpa mtoto wako maji safi na salama kuanzia mililita 60 hadi 120 kwa siku. Punguza au ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao inavyokuwa. Ni bora maji ya mtoto yachemshwe na kufunikwa vyema.

2. Iwapo maji hayasaidii, jaribu pia kumpa juisi za matunda. Mpe mtoto wako juisi ya tufaha (apple), pea au prune iliyotengenezwa kwa kutumia maji salama na safi kila siku. Anza kwa mililita 60 hadi 120 kwa siku na punguza au ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao inavyokuwa.

3. Jitahidi kumpa mwanao chakula chenye ufumwele au fiber. Iwapo mwanao ameanza kula vyakula vigumu, basi mpe vyakula vyenye ufumwele kuliko vyakula vyenye wanga, kama vile tumia unga wa shayiri au tunda la apple na pea lililopondwa pondwa vyema na kuwa kama uji. Epuka kumpa mtoto cereal ya mchele au uji wa mchele kama anatatizo la kukosa choo au kufunga choo.

4. Jiepushe kumpa mtoto wako vyakula vyenye wanga na sukari na vyakula vinavyotengenezwa kwa unga uliokobolewa.

5. Mpake mwanao mafuta kidogo sehemu inayotoka choo kikubwa ili kurahisisha utokaji wa kinyesi. Usitumia mafuta ya madini (mineral oil) au dawa za kulainisha choo na za kuharishwa katika kutibu tatizo hilo la kukosa choo la mtoto.

6. Kukosa choo watoto wadogo mara chache huwa kunasababishwa na magonjwa kama vile Hirschsprung ugonjwa wa kumee neva katika utumbo, au Cystic Fibrosis. Muone daktari au mpeleke mtoto wako hospitalini kama tatizo hilo la kukosa choo linaendelea hata baada ya kubadilisha aina ya chakula cha mtoto au linaambatana na dalili nyingine kama vile kutapika au mtoto kukosa utulivu na kuhangaika.

7. Kuna baadhi ya watoto wanakosa choo au kuwa na choo kigumu kutokana na kutumia maziwa ya ng’ombe. Iwapo umetumia dawa na umefuata maelekezo ya kuondoa ukosefu wa choo na hukufanikiwa. Katisha kumpa mtoto maziwa ya ng’ombe kwa siku mbili au tatu, baada ya siku hizo iwapo bado hajaacha choo badi endelea kumpa maziwa hayo, na pengine tatizo hilo halisababishwi na maziwa ya ng’ombe.

8. Mwogeshe au mweke mwanao katika beseni la maji ya uvuguvugu na hakikisha maji yanafika hadi kifuani. Mkande mtoto tumbo lake wakati akiwa majini na njia hiyo husaidia kulegeza misuli ya mwili wa mtoto, na kumsaidia kupata chook wa urahisi.

NB: Ukosefu wa choo kwa watu wazima baadhi ya wakati huandamana na magonjwa kama vile Arthritis, Appendicitis, Cataract, saratani, shinikizo la damu, Rheumatism na kadhalika lakini kwa watoto huenda tatizo hilo likawa halisababishwi na maradhi hayo.
Utafiti unaonyesha kuwa hakuna uhusiano wowote kuhusu kukosa choo mtoto na kupewa nyongeza ya chuma au Iron Supplement. Hivyo usimkatishe kumpa mwanao chuma iwapo anakosa choo. Kwani chum ni muhimu sana katika kuzuia upungufu wa damu mwilini kwa mtoto wako mdogo.
 
Sehemu kubwa ya jibu ni kunywa maji. aShida watu wengi wanawapa watoto wao dead water. Tumia biowater ni siku hiyo hiyo tatizo litaisha. Bio water inapatikana kwenye kapuni ya QNET. WEBSITE: QNet | Direct Selling - Home Utapata kifaa kinaitwa BIO DISC. nITYAFUTE NJE YA HII FORUM KAMA KWELI UKO SERIOUS.
UNIQUE
 
Kama mboga mboga na matunda haijasaidia tafadhali mpeleka hospitali haraka sana. Hilo ni tatizo kubwa sana kuliko tunavyofikiria.
 
Mara nyingi hutibika kwa kula mboga za majani na matunda ila kuna umuhimu wa kumleta hospitali ili kutafuta kiini cha tatizo.watoto afya zao hubadlika ghafla,anaweza akawa mzima sa hizi alafu mgonjwa dakika inayofuata,usipuuzie kumpeleka hospitali
 
habari wana JF last week rafiki yangu aliniambia amekuwa na shida ya kupat choo kubwa kwa muda mrefu wakati mwingi inamchukua wiki nzima kupata na hata akipata huwa kigumu. nikamshauri atumie Castor oil kuona kama ataharisha akatumia jumapili iliyopita kweli ilimchukua muda kuarisha lakini at last aliarisha kama mara 7 na kutapika mara 3. lakini cha kushangaza tangu siku ile ya jumapili hadi leo ajapata choo tena.

Jamani hili ni tatizo au?
 
habari wana JF last week rafiki yangu aliniambia amekuwa na shida ya kupat choo kubwa kwa muda mrefu wakati mwingi inamchukua wiki nzima kupata na hata akipata huwa kigumu. nikamshauri atumie Castor oil kuona kama ataharisha akatumia jumapili iliyopita kweli ilimchukua muda kuarisha lakini at last aliarisha kama mara 7 na kutapika mara 3. lakini cha kushangaza tangu siku ile ya jumapili hadi leo ajapata choo tena.

Jamani hili ni tatizo au?

Hilo ni tatizo, maana formula inatakiwe iwe Input = Output. Yaani kama unakula mara tatu kwa siku unatakiwa pia utoe huo uchafu mara tatu kwa siku (upate choo mara tatu). Una tatizo la kukosa choo (Constipation). Ukiacha hali iendelee utakabiliwa na tatizo la satatani ya utumbo mkubwa (Colon cancer).

Cha kufanya:
1. Kunywa juice ya ukwaju (angalau 1X3)
2. Kula papai asubuhi au wakati wowote kabla ya mlo wowote
3. Unaweza pia kunywa juice ya carrot (Isiyochanganywa maji-fresh carrrot juice)
4. Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi
5. Kunywa maji mengi (minimum 2 litres/day, but more is better)

Epuka au acha kabisa:
1. Acha kula ugali wa kukoboa ugali wa sembe), badala yake kula ugali wa dona
2. Acha kula vyakula vilivyopikwa kwa kutumia unga uliokobolewa (mfano, chapati, maandazi, mikate myeupe), badala yake tumia unga usiokobolewa

Ushauri wa ziada:
Tatizo likizidi au kuendelea mwone daktari.
 
constipation hiyo. mwambie ajitahidi kula mapapai juice mboga za majani na anywe maji ya kutosha! otherwise operation inamsubiri na kisu kinapigwa palepale kwenye mtandao!
 
constipation hiyo. mwambie ajitahidi kula mapapai juice mboga za majani na anywe maji ya kutosha! otherwise operation inamsubiri na kisu kinapigwa palepale kwenye mtandao!

EEEE Bwana eee, hivi kweli no, ajitahidi kama vipi anipigie 0755 557094 nitampa fomula ya mkorogo ambao i am sure utamsaidia, hapa jamvini watanidisi sana.
 
dawa ni moja tu hata ule vyakula vyote bila diet wala matunda.JUICE YA UKWAJU, asbh kabla hujala kitu chochote,mimi huwa nnatengeneza wk end,naweka kwenye friji napiga asbh km 2 hivi,nikirudi hm jioni naweza piga nyingine wakati wa kula,ama asbh tu nikinywa 2 zatosha,mchana lazima niharibu.

USHAURI
km unashindwa kubeba kwenda nayo ofisini,piga 2 at once,ila kaa mbali na watu,utakavyoanza achia ile hwa yetu,hahahahah fanya zoezi la kila siku utaona matokeo,huna haja ya kujinyima ni dawa tosha,ukiweza tia asali ni nzuri zaidi ukishindwa hata sukari FOR ME IMEWORK OUT
 
kwakweli juic ya ukwaju ni noma kawa shida yako tengeneza nzito nakwambia nusu saa nyingi ucpokwenda chooni bac tena
 
<b>habari wana JF last week rafiki yangu aliniambia amekuwa na shida ya kupat choo kubwa kwa muda mrefu wakati mwingi inamchukua wiki nzima kupata na hata akipata huwa kigumu. nikamshauri atumie Castor oil kuona kama ataharisha akatumia jumapili iliyopita kweli ilimchukua muda kuarisha lakini at last aliarisha kama mara 7 na kutapika mara 3. lakini cha kushangaza tangu siku ile ya jumapili hadi leo ajapata choo tena. <br />
<br />
Jamani hili ni tatizo au?</b>
<br />
<br />
ATUMIE DULUCOLAX HII AIFICHI
INAKAA TUMBONI KUONDOA UCHAFU ...UMENIKUMBUSHA MBALI NIKIWA PUGU BOY AKA WAZEE WA POND AKA WATOTO WA MABAGALA NILIKUWA NA ALLERGE YA CHAKULA MWANZONI NIKAWA NAJIPIKIA SASA KILA NIKIPIKA NAKIRUDI NAKUTA UKOKO..NIKAJIULIZA KULIKONI JAMANI AKUAN ANAESEMA MAMA YANGU ALINISHAURI KILA BAADA YA MIEZI 2-3 NITUMIE KUSAFISHA TUMBO NIKACHUKUA VILE VIDONGE SIKU HIYO NILILETA NYAMA 99 KWA MNAOKUMBUKA LILE BWEN OPP NA MSOSI SIKUMBUKI JINA.....,NIKAWAWEKEA NYAMA SAFIIINIKAWATWANGIA KAMA DULUCOLAX 6 NA WALI SAFII NIKAFUNIKA NILIPORUDI KUSOMA USIKU NAKUTA MWENZANGU WA CHINI ANAAMKA KILA MARA NAMUULIZA NINI AISEE TUMBO LINAUMA NIKAJUA WA KWANZA ALIENDA KAMA SI CHINI YA MARA 8 MPAKA ASBH NA MWISHO AKAISHIA KUKESHA AKISOMA..USIKU ULE ULE MWINGINE IMAN IKAMSHINDA AKANIFWATA UNAJUA NILIWAKUTAWATU WANAKULA CHAKULA CHAKO NIKAONJA UMEWEKA NINI WOTE TUNASHINDA CHOONI USIKU MZIMA NIKAMWAMBIA M NIMEKULA MBONA SIENDI WENGINEE HATA DARASAN AWAKWENDA JARIBU DULUCOLAX
 
Pamoja na maelezo mazuri Sisi binadamu tunahitaji kubadikika katika vitu viwili 1) Kunapokuwa tunaku chakula chochote tujitahidi kuchakuwa chakula chetu mara 16 na kuendelea - hapa huwa mtihani mkubwa lakini tujitahidi kutafuna muda mrefu. 2) tuache tabia ya kunywa maji baada ya mlo, kitaalamu kula huku ukipata funda mbili tatu za maji kama tunavyowafanyia watoto tunapolalisha vyakula vyao hupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo.
 
Mimi huwa nakula papai zima peke yangu, baada ya nusu saa au lisaa naenda kushusha mzigo wa haja chooni
 
Kiboko ya hilo tatizo piga juice ya ukwaju ya ukweli ambayo haijachakachuliwa xana.Kunywa ya kutosha majibu utayapata baada ya nusu saa 2.Angalizo ucje ukanywa safarin au ukiwa mbali na choo maana ucje ukaumbuka.
 

Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom