Tatizo la kupata choo kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation). Fahamu chanzo na tiba yake

Wadau siku za nyuma nilikuja hapa na tatizo la kukosa choo, tumbo kujaa gesi. Tatizo mpaka leo bado lipo. Na mwezi ulioita nimefanyiwa kipimo cha OGD Endoscopy...
Madhara ya kukosa choo kwa muda mrefu

kutopata-choo-jpg.360705



MADHARA YA KUKOSA CHOO KWA MUDA MREFU

Habari za leo rafiki ni matumaini yangu unaendelea vyema na kufurahia uwepo wa blog hii, Nimepokea email nyingi kuhusu tatizo la kutopata choo hvyo nimeona ni heri kuzungumzia hapa ili wote mfahamu tatizo hili

tatizo Hili ni sugu sana miongoni mwa watu wengi na kwa watoto wadogo pia Bila kujua ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka hata hivyo wengi huwa wanapuuzia na kuona ni tatizo la kawaida,
LAHASHA!!! Napenda kukuambia rafiki tatizo la kutopata choo kwa Muda mrefu ndio chanzo cha magonjwa mengine tena ya hatari zaidi kwasababu mtu unapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa

uchafu unaotakiwa kutoka hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea unahamia kwenye damu na kuwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kukuathiri zaidi

~kwa kawaida mtu anapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku na mara Tatu kwa wiki hivyo iwapo unakosa choo kwa siku Tatu ilhali unakula elewa moja kwa moja una tatizo katika mfumo wa mmeng'enyo

CHANZO CHA TATIZO HILI LA KUTOPATA CHOO
~tatizo hili husababishwa zaidi na ulaji mbovu wa vyakula na kutokujizoesha kwenda haja mara kwa mara pia kula vyakula vilivyokobolewa na matumizi mabaya ya dawa na magonjwa mengine pia mabadiliko ya hormone

DALILI ZA KUTOPATA CHOO

Dalili za tatizo hili ni ÷

KUPATA HOMA KALI
KUTETEMEKA KWA BARIDI
KUTUMIA NGUVU NYINGI NA MUDA MWINGI KUJISAIDIA
ULIMI KUWA NA UTANDU MWEUPE NA KUTOA HARUFU MBAYA
KUKOSA HAMU YA KULA
TUMBO KUJAA GESI
KUPATA VIDONDA SEHEMU YA NJE YA HAJA KUBWA

NAMNA YA KUTIBU NA KUEPUKA TATIZO LA KUTOPATA CHOO
~matibabu ya tatizo la kutopata choo kwa ufup ni magumu na marahisi pia kutokana na ukubwa wa tatizo pia hata hivyo kila mtu
anaweza kujikinga na tatizo hili kwa kufuata kanuni za ulaji wa lishe bora kwasababu tatizo la kutopata choo husababishwa na namna
unavyokula au kuishi hivyo ukifuata kanuni za lishe bora tatizo hili

halitakupata hivyo njia sahihi ya kujikinga na tatizo la kutopata choo ni kula nafaka zsizokobolewa, matunda, mbogamboga na maji kwa wingi

~matibabu hufanyika kwa kuangalia ukubwa wa tatizo na Hali ya mhusika kwan matibabu ya mtoto sio sawa na ya mtu mzima mwenye miaka 70 Hali kadhalika tatizo hili likijulikana mapema huwa rahisi kulikabili tofauti na tatizo la mda mrefu ambapo tiba

Yake huweza kuwa kubwa haswa ambapo tiba Yake huhusisha vidonge na chakula na hata kufanyiwa upasuaji kuondoa kinyesi kilichoganda katika damu na kuendelea na matibabu ya chakula

MADHARA YA KUKOSA CHOO KWA MUDA MREFU

madhara ya kukosa choo kwa Muda mrefu ni÷
KUPATA SARATANI YA UTUMBO
FIGO KUSHINDWA KUFANYA KAZI VIZURI
KUPATA PRESHA NA KUPATA UGONJWA WA INI
KUPATA MAGONJWA YA MOYO NK

KUMBUKA :zingatia kula milo mitatu kila siku, kula vyakula vyenye nyuzinyuzi nyingi (high fibre diet), kunywa maji mengi na fanya mazoezi mara kwa mara pia usizoee kutumia dawa za kemikali ovyo ovyo chanzo. Tatizo la kupata choo kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation). Fahamu chanzo na tiba yake
 
Pole sana mkuu. Unabidi urudi tena kwa dokta akuongezee dozi(high dose ppi) halafu pia zingatia vyakula unavyokula. Usile vyakula km maharage viazi na vyakula vya acid kwa wingi. Badilisha msosi mkuu
 
Wakuu ukila karanga nyingi ukaenda chooni sikufichi utatoa wastes maridadi kabisa.uchafu wote unatoka kilaini kwa kweli karanga mbichi na asali Ni nzuri Sana kwa wenye matatizo ya kupata choo
 
Ipi tofauti ya bei ya choo kibaya na kizuri ??.....nataka niangalie kipi kitanilipa ili niangalie kipi kitoke kwanza
 
Kama ilivyo pengine wewe au ndugu,jamaa na marafiki wanatatizo hilo basi wajuze hiki.

Nazani wengi wetu tunafahamu vyakula vya nyuzinyuzi (Fibres).
Ndiyo vyakula hivyo husaidia kupunguza tatizo la kutopata choo au choo kigumu.

Kabla naomba tufahamu vyakula vya nyuzinyuzi.
Vyakula hivi hupatikana hasa katika matunda.
Mfano: Nanasi, Ndizi, embe (Hasa embe bivu), papai, Machungwa n.k
Basi kama unatatizo hilo tumia vyakula vya nyuzinyuzi pamoja na kunywa maji kwa wingi.
Basi tatizo litakuwa limekwisha

Tatizo likiendelea muone daktari
 
Habari wana JF mie nina tatizo la kutopata choo kwa muda wa wiki kama mbili na zaidi..hali unazidi japo nmetumia dawa za kusaidia choo zilisaidia kwa muda zilipo kwisha hali ikaendelea kama kawaida.

Tatizo hili limefanya tumbo linauma limejaa hadi kufikia hatua napata maumivu ya kifua muda mwingine nahisi kitu kinakaba kama kiungulia ...najitahidi kula matunda na vyakula vinavyoweza kusaidia kupatikana choo ila hali bado...nikipata ni kidogo sana sometimes kinakua kigumu.

Ahsanteni sana.
 
Zingatia unywaji wa maji ya kutosha, hakikisha ndani ya saa 24 umetumia angalau lita 2.5 hadi 3.

Jitahidi kutumia chakula kiasi vyema usizidi saizi ya ngumi zako mbili, itarahisisha mfumo wa chakula. Zingatia ratiba ya chakula na hakikisha unafanya mazoezi.

Kwa maelezo yako unaweza kuwa na tatizo la mmeng'enyo wa chakula, vyema kumuona daktari.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom