Tatizo la kuongozwa na wakomunisti

Ustaadh

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
413
16
Uamuzi wa CCM kuwaengua wagombea wa jinsia ya kiume katika kinyang'anyiro cha uspika kwa kisingizio cha kujali jinsia ya kike unaonyesha wazi jinsi utawala wa kikomunisti ulivyo mbaya. Kwa maamuzi haya ya kikundi cha watu wachache TZ inaungana na mataifa kama Korea ya kaskazini, Cuba, China na maengine ya dizaini hiyo ambapo 'wateule' wachache huamua na kushinikiza maamuzi yao kukubaliwa na wengi hata kama wanakwenda kinyume na katiba yao na hata katiba ya nchi. Dalili ziko wazi kuwa tusipokuwa makini kuna hatari ya kutengenezwa utawala wa kifalme ambapo ndugu, marafiki, jamaa, na washikaji ndio wanaoendesha nchi huku demokrasia ikisiginwa. Haaingii akilini kwa kigezo cha jinsia kupigiwa debe kwenye uspika tu wakati nyadhifa zingine zote wala hakuna anayewakumbuka kina mama. Ni dhahiri CCM inawapa peremende kina mama ili wajione wamepiga hatua na kuchekelea huku haki zao chungu mzima zikizimwa.

Nachelea kusema tunaweza kupata mshituko wakati JK atakapotangaza baraza jipya la mawaziri kwa kuhusisha hata wale wasiotarajiwa kwani anaamini hana cha kupoteza - hagombei tena! Lakini kila jambo lina mwisho hata kama itachukua miaka 10 au 20. Mungu ibariki Tanzania.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom