Tatizo la kunuka mdomo(kinywa) husababishwa na nini?

View attachment 1740414

Wadau, heri ya mwezi mpya huu, nina swali ambalo linahitaji msaada wenu.

Kwa nini kuna baadhi ya watu midomo inatoa harufu mbaya!?

Hata Kama akipiga mswaki baada ya muda harufu hiyo hurudi.

Unakuta mtu meno ni meupe na masafi ila mdomo unanuka, shida ni nini?

Na dawa yake ni nini?

Karibuni wadau, shukrani sana.
*******

Ushauri



Pia soma: Ongezeko la watu kunuka mdomo

Dk Shita Samwel, Mwananchi
Katika maisha ya kila siku inawezekana umewahi kukutana na mtu ambaye ukiwa karibu naye kimazungumzo, utagundua anatoa harufu mbaya mdomoni.

Kwa kawaida mdomo na pua hutoa pumzi nje ambayo huwa na harufu asilia ambayo haiwezi kumkera mtu mwingine, lakini mara nyingine hali hiyo inaweza kujitokeza kwa mtu kutoa pumzi yenye harufu mbaya.

Pengine watu wa karibu au wanaokutana na mwathirika wa hali hii, wanaweza wakadhani mtu huyo ni mchafu mwenye na tabia ya kutopiga mswaki au kutosafisha kinywa chake vizuri.

Wengi hawajui kuwa mtu huyo anaweza kuwa na tatizo linalojulikana kitabibu kwa jina la halitosis, ambalo maana yake ni kutoa pumzi ama mdomoni au puani.

Mtu mwenye tatizo hili anaweza kukumbana na kunyanyapaliwa na wanajamii wanaomzunguka kiasi cha kuweza kumsababishia matatizo ya kisaikolojia.

Mwathirika anaweza kupata na tatizo la hofu iliyopitiliza anapokuwa katika jamii; anaweza akajinyofoa kutoka katika jamii na kujitenga na baadaye anaweza kupata sonona.

Ugonjwa wa halitosis

Karibu asilimia 20 ya watu duniani wanakumbwa na ugonjwa huu na hivyo kukimbilia kwa wataalamu wa afya ya kinywa.

Hufika kwa wataalamu hawa wakidhani wana magonjwa ya kinywa ikiwamo mashimo katika meno, kulika kwa meno, kuoza kwa meno na magonjwa ya fizi.

Ukweli ni kuwa si wagonjwa wote wenye kutoa pumzi yenye harufu mbaya wana tatizo halisi la halitosis, kati ya asilimia tano hadi 72 wanaofika katika huduma za afya hugundulika kuwa hawana tatizo hili moja kwa moja.

Tatizo la kutoa pumzi yenye harufu mbaya ambalo ndiyo ugonjwa halisi, linasababishwa na uwapo wa mrundikano wa bakteria katika uvungu wa fizi na nyuma ya ulimi karibu na koo.

Kinywa kwa ujumla, kikijumuisha meno, fizi, ulimi na vifuko vya mate kinaweza kuwa ni maficho mazuri kwa mamia ya bakteria. Ndiyo maana inaaminika tatizo la harufu mbaya mdomoni ni kinywa chenyewe.

Kinywani pekee kuna karibu jamii 600 za bakteria ambao huambatana na mabaki ya vyakula tunayokula kila siku. Kuwapo kwa protini ya kwenye mate na protini ya vyakula tunavyokula na uvunjwaji wa mabaki yake na bakteria waliopo mdomoni, ni chanzo cha kuwapo kwa harufu mbaya.

Mabaki ya protini mdomoni ambayo huvunjwavunjwa na bakteria na kuwa tindikali ya amino na hapo baadaye inapovunjwa, hutoa gesi yenye harufu mbaya.

Mfano mzuri ni pale protini ijulikanayo kama methionine na cysteine inapovunjwavunjwa kinywani na hivyo kutoa gesi yenye harufu mbaya ijulikanayo kama Hydrogen sulphide.

Mara nyingi harufu ya kinywa inaweza kuwa nzito zaidi baada ya mtu kuamka. Hii ni kwa sababu wakati wa kulala mdomoni kunakuwa na kiasi kidogo cha hewa ya oksijeni.

Bakteria waliopo mdomoni ni wale wasiohitaji uwepo wa hewa ya oksijeni hivyo kipindi cha usiku tukiwa tumelalala, ndipo huvunjavunja mabaki ya chakula ambayo huambatana na kutolewa gesi zenye harufu mbaya.

Vilevile harufu ya kinywa inaweza kubadilikabadilika kutokana na vyakula tunavyokula ikiwamo vitunguu maji, vitunguu swaumu, hiliki, tangawizi na pia uvutaji sigara na unywaji wa pombe.

Hivyo siyo mara zote kupumua harufu isiyo ya kawaida ni ugonjwa; mara nyingine inakuwa ni tatizo la muda tu lililochangiwa na vyakula na matumizi mengine ya vitu.

Asilimia 10 zilizobaki, mara nyingi husababishwa na matatizo mengine ikiwamo magonjwa ya kooni, puani, shambulizi za nyufa za mifupa iliyopo usoni, magonjwa ya mfumo wa chakula, magonjwa katika mapafu, magonjwa ya masikioni na madhara ya ugonjwa sugu wa mafindofindo.

Vilevile kuwapo kwa majipu ya fizi au meno, vidonda mdomoni au michubuko, vidonda vya kooni na maambukizi ya virusi vya herpes simplex na HPV. Mara chache pia tatizo hili linaweza kuchangiwa na magonjwa ya ini ikiwamo kuharibika kwa ini na majipu katika ini.

Mara nyingine wanaoshtakia tatizo hili hubainika kuwa na tatizo la usafi wa kinywa. Na wanaposhauriwa kuboresha usafi wa kinywa kwa kutumia dawa za meno, au kusukutua na dawa maalumu za kusafisha kinywa nyuma ya ulimi, tatizo huisha haraka.Tiba ya Tatizo hili ipo kwa mwenye kuhitaji anitafute kwa wakati wake.
 
Back
Top Bottom