Tatizo la Kumtetea Kiongozi Aliyeshindwa ni Pale Kiongozi husika anapotafuta Kinga

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
8,391
4,055
Ukiona kiongozi au nchi inaingia katika kuongelea suala liwe la udini au ukabila, basi ujue kiongozi/serikali iliyopo imeshindwa kazi, sasa katika kutapatapa ndio hutafuta jani,tawi, au mti wa kuushikilia angalau kuongeza siku kadhaa madarakani.
Na tatizo linakuzwa zaidi unapo pata waandamizi wa serikali au kiongozi huyo wanapoacha kumsaidia au kuisaidia serikali kwa kusema kweli bali kwa kufunika kombe ili mwana haramu apite.
Hivi karibuni kuna waandamizi wa serikali yetu Matheus, na Nguleja, wao badala ya kumwambia fisadi kwamba hapana hapa tumekosea/umekosea, wao wana mwambia umepatia, madhara yake ni kwamba wananchi ambao ndio wenye serikali hawakubaliani na maneno nk ya hawa waandamizi, matokeo yake serikali ina zidi kuyumba, matokeo yake viongozi waliopo madarakani wataanza kuteleza kutoka kwenye hili tawi waliloshikilia/nyasi na iliwajiokoe watakimbilia kitu kilicho karibu nao nalo ni ukabila/udini, sasa madhara ya hili tawi/majani haya yakujiokoa/kushikilia ni kwamba yatakuwa na madhara hata kwa hao wanaomtemtea aliye shindwa, kwani baadae watajiona kumbe wote si wamoja, mwingine ni mchukuma, mwingine wa newala, ,wingine wa tobola, mwingine wa bwagamoyo nk nk almsiki si matusi watajikuta hata maswahiba wao wamedhurika kwani yule atakaye tumika kumpiga wa tabola hatu chukulia kwamba huyu ni mwenzetu, au yule atakaye mpiga, wa bwagamoyo hatachukulia kwamba huyu ni mwenzetu. hivyo chonde chonde mwenye akili haambiwi tazama..
 
ndo kichaka cha kikwete hicho, jamaa anatupeleka pabaya
Sasa kitu kikubwa je huyo Matheus au Nguleja watapona kwenye hiyo vita? maana wao si wamoja? ndipo watakapo gundua mi mpagani, yule sunni, huyu mlutheri nk nk
 
Back
Top Bottom