Tatizo la kukosekana kwa umeme ni la kujitakia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la kukosekana kwa umeme ni la kujitakia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SolarPower, Jun 29, 2011.

 1. S

  SolarPower JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 226
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna sababu zozote ambazo Serikali inaweza kuzitoa na kukubalika kuwa sababu kuu kwanini tunakabiliwa na tatizo la ukosefu wa umeme kwa sasa. Sababu kuu na ya pekee iliyotufikisha hapa ni uzembe na ukosefu wa uzalendo toka kwa viongozi wetu. Haiingii akilini kuona kuwa Serikali inashindwa kutenga angalau shilingi bilioni 300 kila mwaka kwa ajili ya kuzalisha umeme lakini wakati huo huo inakuwa tayari kutenga zaidi ya shilingi bilioni 80 kila mwaka kwa ajili ya BUNGE. Kwa miaka mitano hii ni zaidi ya MEGAWATI 500 ZA UMEME.

  Na kufuatana za ripoti za CAG zaidi ya shilingi trilioni 2.5 katika bajeti ya Serikali ya mwaka hutumiwa vibaya. Fedha hizi pekee ni zaidi ya MEGAWATI 3100 ZA UMEME KWA MWAKA.

  Pia tukumbuke kuwa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na TAMISEMI kwa mwaka ujao wa fedha (2011/2012) ni zaidi ya shilingi trilioni 3.4
   
Loading...