Tatizo la Kukosa Usingizi (Insomnia) na tiba yake

Hiyo inaitwa ''Insomnia'' inasababishwa na kuwa na mawazo sana, stress, kunywa maji mengi kabla ya kulala au utumiaji wa kahawa kwa baadhi ya watu

Jitahidi kuuchosha mwili kiasi kwa mazoezi ya viungo kabla ya kulala, na kuavoid hivyo visababishi hapo juu

Kuhusu synthetic drugs watu huwa wanatumia piriton ambayo ni dawa ya flue pia, Pia nasikia ukila ndizi mbivu usiku ni rahisi kupata usingizi (sijui kama ni researched)

Watakuja wataalam zaidi kukusaidia

Inshallah,
 
Diazepam Vidongeee...!! Utalala mpaka ufurahi sema tatizo inaleta addiction yani haiponeshi sema inakufanya ulale tu na mwili ukizoea hiyo hali ndo utakuwa hulali kabisa bila kunywa dawa so cha muhimu nenda hospital upate matibabu ya Kisaikolojia yanayokufanya usipate usingizi eithee upewe dawa za Depression ambazo hutibu hali ya msongo wa mawazo lakini pia hufanya ulale zinaitwa AMITRYPTILINE. Pole sanaa...
 
Hiyo inaitwa ''Insomnia'' inasababishwa na kuwa na mawazo sana, stress, kunywa maji mengi kabla ya kulala au utumiaji wa kahawa kwa baadhi ya watu

Jitahidi kuuchosha mwili kiasi kwa mazoezi ya viungo kabla ya kulala, na kuavoid hivyo visababishi hapo juu...
Thanks man!
 
Diazepam Vidongeee...!! Utalala mpaka ufurahi sema tatizo inaleta addiction yani haiponeshi sema inakufanya ulale tu na mwili ukizoea hiyo hali ndo utakuwa hulali kabisa bila kunywa dawa so cha muhimu nenda hospital upate matibabu ya Kisaikolojia yanayokufanya usipate usingizi eithee upewe dawa za Depression ambazo hutibu hali ya msongo wa mawazo lakini pia hufanya ulale zinaitwa AMITRYPTILINE. Pole sanaa...
Diazepam ndio dawa?
 
Je ambao tuna matatizo ya kusinzia mfano wakati wa darasa au kipindi cha mahubiri kanisani.

yaan sehemu yoyote ile inayokuwa na mda mrefu wa mazungumzo.

Je hapo shida nini?
 
tatizo la kukosa usingizi isomnea husababishwa na mambo yafuatayo

mawazo :msongo wa mawazo hufanya mtu kukosa usingizi hivyo hutumia muda mwingia kuchanganua baadhi ya mizunguko na changamoto za maisha. mawazo ni adui mkubwa sana kwenye afya ya akili mpka ya mwili na tabia kwa ujumla.

matumizi ya computer ama simu: matumizi ya simu ya muda mrefu ni tatizo kwa kuipa kazi kubwa macho pupil na cornea ya jicho kucontrol mwanga ivo basi kukaa kwa muda mrefu kwny screaan ama tv huleta changamoto kubwa kumaintain muda wa kulala.

Madawa/chemical : zipo dawa amabazo husabisha mtu kutokupata usingizi nazo n mirungi , caffein ,kahawa energy drink hizo humfanya mtu kutopata usingizi na kufanya misuli kuwa active wakati ili mtu alale anahitaji misuli irelax na mwili kuwa at rest ndo hupata usingizi.

Maumivu makali /pain:Yapo magonjwa yanayoleta maumivu makali muda wote mfano cancer ,dental diseases ... maumivu makali hufanya mtu kutopata usingizi.

Upweke |sonona huu n ugonjwa mkubwa kwa wali waliozoea kulala pembeni mwa wenzi wao wanapokua mbali hupata shida kupata usingizi.

Makelele : kelele ni sauti ambazo hazipo kwenye mpangilio maalumu hivyo bac huleta sauti mchanganyiko ambazo huumiza ngoma ya sikio na kuleta kuchanganyiwa distabance.

mwisho usingizi n bora kwa afya ya ubongo.
 
Hello guys,

Kuna wakati hutokea unatakiwa uamke hasubuhi mapema ili uwahi kazini lakini cha kusikitisha ni kwamba usiku haukupata usingizi! utasema ngoja nijitahidi niwahi kazini nikirudi nitalala kisha usiku unaofuata inakuwa ni hivyo hivyo. Unakosa usingizi. Inachosha sivyo?. Basi kama wewe ni miongoni mwa wenye hili tatizo pole sana. Lakini husijari tatizo hili linatibika.

Twende pamoja...

Tatizo hili kisayansi hufahamika kama INSOMNIA au hari ya kukosa usingizi.
INSOMNIA ni tatizo la kiafya ambapo mtu anakosa uwezo wa kulala au anashindwa kupata mda wa kutosha wa kulala tofauti na alivyotarajia malanyingi huambatana na tatizo la kusinzia wakati wa mchana, kukosa nguvu na pia kuwa ni mtu mwenye msongo wa mawazo.

Pia tafiti zinaonyesha kuwa watu wengi wenyetatizo hili ndio huongoza kwa kusababisha ajari nyingi za barabarani na hata kudhoofisha uwezo wao wa kufikiri

Pia zipo takwimu zinazoonyesha kwamba 10 hadi 30 ya watu wazima(adult) walishawahi kuwa na tatizo la kukosa usingizi katika maisha yao, lakini pia nusu ya watu wote duniani walishawahi kupata tatizo la insomnia angalau malamoja kwa mwaka na pia isitoshe watu wenye umri zaidi ya miaka 65 husumbuliwa zaidi na tatizo hili kwa upande wa jinsia wanawake ndo ukumbwa zaidi na tatizo hili kuliko wanaume

DALILI ZAKE NI ZIPI?
Zifuatazo ni dalili mbalimbali ambazo utazigundua kwa mtu anayesumbuliwa na tatizo hili la kukosa usingizi

>1: Kwanza kabisa utamuona mtu huyu akiangaika akiwa kitandani alafu ubadilisha mitindo ya kulala mala kwa mala ili kutafuta usingizi.
> 2: Malanyingi mtu huyu ikitokea ameamka usiku na kukatisha usingizi basi hishindwa kupata tena usingizi basi ikitokea hivyo hujikuta anaamka asubuhi sana.
> 3: Pia watu wenye tatizo hili huwa wanashindwa kuwekea umakini katika shuhuri mbalimbali wanazofanya kama vile kazini au wanapojisomea pia wakati mwingine hata wanapokuwa wanaendesha usafiri hivyo huchangi pakubwa katika kusababisha ajari za barabarani, watu hawa pia mala kwa mala hupatwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu
>4: Dalili nyingine ni kwamba wata hawa huwa na tabia ya kusinzia wakati wa mchana pia huwa ni wenye hasila, msongo wa mawazo na hata kuwa ni watu wenye hofu.
>5: Watu wenye tatizo hili pia hukosa nguvu malanyingi huwa ni watu wenye kuhisi kichoka hasa wakati wa mchana pia huwa ni wenye kushindwa kufikilia mambo kwa kina.

JE NI ZIPI SABABU ZA HILI TATIZO LA KUKOSA USINGIZI??

Dalili mbalimbali tulizoziona hapo juu husababishwa na mambo kadha wa kadha yakiwemo haya yafuatayo;

>1: Matatizo ya upumuaji ambayo hasa hutoke usiku wakati wa kulala ambayo malanyingi husababishwa na mambo mbalimbali kama vile maladhi yanayofahamika kama (UPPER AIRWAYS RESISTANCE SYNDROME) ambamo humo ndani yake yapo maradhi yanayopelekea tundu za upumuaji kupungua na kuwa nyembamba zaidi hivyo kupelekea mtu kushindwa kupumua vizuri na kupelekea kukosa usingizi .
>2: Matumizi ya dawa mbalimbali zikiwemo mirungi, caffeine, nikotini, cocaine na hata urevi wa pombe husababisha mtu kuwa macho kwa mda mrefu hivyo humfanya ashindwe kulala.
>3.Pia zipo dawa ambazo hutumika kutuliza maumivu ya mwili mfano dawa dawa zilizopo katika kundi la opioid ambapo mtu akiwa anazitumia kwa mda mrefu au labda alikua anatumia kisha akasitisha kutumia dawa hizo humletea pia tatizo la kukosa husingizi.
>4:Wakati mwingine mtu anakuwa amesitisha matumizi yake ya dawa za kutuliza msongo wa mawazo au dawa za kupata usingizi mfano Benzodiazepine humfanya mtu huyu kurudia tena katika hari yake ya kukosa usingizi.
>4: Kwa watu wenye maradhi ya moyo yakiwemo shinikizo la juu la damu na angina nao wapo katika shida hii
>5: Kunda ugonjwa unaitwa "miguu kuwaka moto" kitaalamu hufahamika kama Restless Legs Syndrome, malanyingi watu wenye tatizo hili huisi kama wanachomwa na vitu vyenye ncha kali katika sehemu za miguu hasa wakati wa usiku hivyo huwapelekea kukosa usingizi kabisa
>6: Hata maumivu ya aina yeyote ile labda ni maumivu ya kichwa, tumbo, mgongo au majeraha hasa wakati wa usiku huwa yanasumbua kwakweli humfanya mtu awe macho usiku kucha.
>7: Sababu nyinginezo ni kama mtindo wa maisha kama vile matizo ya uzazi kutokuwa na tabia ya kufanya mazoezi na mahusiano.

AINA ZA INSOMNIA
1. Ya muda mfupi;

Malanyingi hii hutokea na kumalizika chini ya wiki moja na visababishi vyake ni vile vidogo vidogo vikiwemo kubadili mtindo wa maisha au mazingira mitindo ya kulala au msongongo wa mawazo

2. Ya muda mrefu:
Hapa mtu huwa anafuruliza kupatwa na tatizo hili kwa mda wa chini ya mwezi mmoja, watu wenye aina hii ya insomnia huwa wanashindwa kupata usingizi hatakama wanao mda mwingi wa kulala hivyo huwapelekea kushindwa kufanya vizuri kazi zao wakati wa mchana.

3. Insomnia sugu:
Sasa hii ile ambayo inadumu zaidi ya mwezi mmoja watu hawa huwa wanakuwa na msongo wa mawazo wa uliopitiliza hadi kupelekea kuzuka kwa maradhi mengine yakiwemo maradhi ya moyo

MADHARA YAKE NI YAPI??
Ikitokea mtu mwenye tatizo hili akakosa matibabu kwa wakati yapo madhara mengi atayapata ambapo hutofautiana kulingana na aina ya sababu iliyopelekea tatizo hili. Kwamfano mtu anaweza kukonda kupita kiasi, kupatwa matatizo ya akiri na hata kupelekea kuwa kichaa.

NJIA ZA KUEPUKANA NA INSOMNIA!!

Bila shaka tatizo hili linazuilika kama tu mtu atafuata mitindo mizuri ya maisha
Kwamfano kama mtu ataweza kulala na kuamka katika mda ulelule kilasiku basi ita mjengea mazoea hayo na kumsaidia kuepuka tatizo hili.

Pia si jambo zuri kufanya mazoezi wakati wa usiku hasa pale unapokaribia mda wa kulala

MADHARA YAKE NI YAPI??
Ikitokea mtu mwenye tatizo hili akakosa matibabu kwa wakati yapo madhara mengi atayapata ambapo hutofautiana kulingana na aina ya sababu iliyopelekea tatizo hili. Kwamfano mtu anaweza kukonda kupita kiasi, kupatwa matatizo ya akiri na hata kupelekea kuwa kichaa.

NJIA ZA KUEPUKANA NA INSOMNIA!!
Bila shaka tatizo hili linazuilika kama tu mtu atafuata mitindo mizuri ya maisha
Kwamfano kama mtu ataweza kulala na kuamka katika mda ulelule kilasiku basi ita mjengea mazoea hayo na kumsaidia kuepuka tatizo hili.

Pia si jambo zuri kufanya mazoezi wakati wa usiku hasa pale unapokaribia mda wa kulala
 
Wengi wanakua wana njaa, njaa ikiwa inauma uwezi kulala. Kula vizuri ushibe, faster unakoroma kama kondoo
 
Wengine tuna hadi mapakiti ya VALIUM sio kwa ajili ya ulevi bali usingizi, incase ukikata mapema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom