Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Kuna watoto wamekuja likizo hapa home huyo mdogo ana miaka 4 na ni kikojozi mzoefu. Tumemnunulia mpira wa kumtandikia ili asiozeshe godoro na kumkataza asinywe chai au maji Mengi kabla hajalala. Pamoja na hilo tunahakikisha kabla hajalala anakuwa amekojoleshwa,pia usiku tunamuamsha na pia ile alfajiri.

Kwa sasa ana siku 10 hajakojoa tena kitandani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa experience wengi hukojoa ile alfajiri so jitahidini kumlisha chakula laini usiku ambacho hakitamlazimu kunywa maji mengi kulainisha then set alarm saa 10 alfajiri muamshe akakojoe
 
Mwanangu alikuwa na tatizo hilo lakini lilikujaisha lenyewe. Humu JF kuna witch doctors nakushauri usumwingize mwanao kwenye witchcraft, just wait tatizo litajiishia.
 
Hii inaitwa enuresis. Daktari wa mfumo wa akili hasa wa watoto atakusaidia.Tatizo liko kwenye mfumo wa fahamu. Ubongo wa binadamu unafanya kazi masaa 24. Kibofu kikijaa ujumbe unafika kwenye ubongo na usingizi unapata.

Mtoto wa miaka miwili bado mishipa ya fahamu pamoja na sphincter zinajijenga lakini miaka mitatu watoto wengi huwa wanaamka. Wengine hufika miaka 5 lakini 12 ni tatizo.

Weka alarm ya kukuamsha umpeleke choo ni kila baada ya masaa manne.
Je kwa mtu mzima inakuaje? Nina ndugu yangu tulivokua wadogo tulikua na tabia hiyo lakini mimi iliacha. Anaelekea 27 years na bado anaachia usiku..ni ngumu kumwambia si wajua aibu na mtu mzima..

Je, anasaidiwaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wakuu,

Nina mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 12 sasa anaingia class 7. Anakojoa kitandani kila siku. Kwa mwezi anaweza asikojoe mara moja au mbili tu. Lakini siku zote hizo anakojoa sana.

Katumia dawa za kienyeji, za kimasai pia lakini imeshindikana. Nikampeleka hospital kuna vidonge alipewa. Walisema akinywa ndani ya siku 30 tatizo litaisha. Hakuna unafuu. Nikampeleka Muhimbili kuna Dr niliambiwa anasaidia lakini ilishindikana. Dr alisema hali itaisha yenyewe.

Yeye binti pia haipendi hii hali. Maana huwa anakuja na njia nyingi za kupona tatizo lake kama kunywa maji ya mchele, kunywa maji ya nazi, kuchemsha yale manyoya ya mahindi mabichi nk.

Sasa anakaribia kukua na soon ataenda form one boarding.

Naomba msaada wenu kwa yeyote anayejua dawa au Dr anaweza msaidia please. Tupo Dar

Mkuu, fuate hii link ujifunze jambo.

Delivered from spirit of bed wetting
 
Habari wakuu,

Nina mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 12 sasa anaingia class 7. Anakojoa kitandani kila siku. Kwa mwezi anaweza asikojoe mara moja au mbili tu. Lakini siku zote hizo anakojoa sana.

Katumia dawa za kienyeji, za kimasai pia lakini imeshindikana. Nikampeleka hospital kuna vidonge alipewa. Walisema akinywa ndani ya siku 30 tatizo litaisha. Hakuna unafuu. Nikampeleka Muhimbili kuna Dr niliambiwa anasaidia lakini ilishindikana. Dr alisema hali itaisha yenyewe.

Yeye binti pia haipendi hii hali. Maana huwa anakuja na njia nyingi za kupona tatizo lake kama kunywa maji ya mchele, kunywa maji ya nazi, kuchemsha yale manyoya ya mahindi mabichi nk.

Sasa anakaribia kukua na soon ataenda form one boarding.

Naomba msaada wenu kwa yeyote anayejua dawa au Dr anaweza msaidia please. Tupo Dar
Mkuu kuna rafiki yangu alikuwa anajikojolea,mpaka tukiwa m4 4 enzi hizo alitumia kila aina ya dawa.

Alijaribu kuchelewa kulala ila wapi

Kutokunywa maji ila wapiii

Kuamshwaaa ila wapii

Mwisho wa siku ilikuja kuishs yenyewe automatic,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanangu wa miaka sita kuna wakati pia anakojoa, tunachofanya lazima akojoe kabla ya kulala na pia kati ya saa sita na saa saba tunamkojolesha hapo hatakojoa kitandani, ila tukijisahau mida hiyo lazima aumwage!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dawa ya tatizo hilo ni:

1. Control unywaji wa maj na vimiminika sanasana usiku, asinywe kabisa ikiwezekana
2. Saikolojia yake inabid ibadilike, achukie kabisa hyo kitu
3. Afanye kegel exercise kila siku, hii ni kumwezesha a build muscles znazohusika na uruhusaj wa mkojo kwenye mfumo wake
4. Aamke usiku mara mbili kwenda kukojoa



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dawa ya tatzo hlo ni:

1. Control unywaji wa maj na vimiminika sanasana usiku,sinywe kabisa ikiwezekana
2. Saikolojia yake inabid ibadilike,achukie kabisa hyo kitu
3. Afanye kegel exercise kila siku,.hii ni kumwezesha a build muscles znazohusika na uruhusaj wa mkojo kwenye mfumo wake
4. Aamke usiku mara mbili kwenda kukojoa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kidogo number 3 na ku support ila hizo nyingine ni ngumu sana mkuu.

Yaniii wengii waooo pamoja na huyo best yangu tulikuwa hadi tuna chap ila wapii. Yanii anakula kibokoo kimoja kitakatifuuu ndani ya mwezi mmoja ila wapii.

Kuna siku tuli mchapa kimoja kama kawaida alikuwa ajavaa kitu siku hiyoo kikapenyaa alivyo amkaa alitutukana sana akasema kuanzia leo hataki msaada wetu tumuacheee. Jamaa hadi alilia.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zamani vikojozi tulikuwa tunawatembeza na kawimbo kao kale ka kindumbwe ndumbwe chalila



Hii iliwafanya watoto wawe makini na kuondoa kabisa ishu ya ukikojozi!!

Maana anajua akikojoa tu natembezwa mtaamzima na godoro lake la mkojo na ngoma na hako kawimbo

Skuiz ndo naona hapa mnawapeleka hospitali

Dah! Kweli zama zinatofautiana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah! Usinikumbushe huu ugonjwa. Niliteseka sana kisaikolojia wakati nakua, hadi nikakosa kujiamini. Vuta picha ni mtoto alaf una huu ugonjwa na unalelewa na wazazi ambao sio wako. Kwanza wanaona unajiendekeza so kila siku ilikua ni kichapo. Sitaki hta kukumbuka!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom