Tatizo la kukaukiwa koo/mate kinywani

mayenga

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
4,118
1,966
Nina tatizo la kukaukiwa na koo kiasi kwamba napata shida hata katika kupumua na kuongea.nisaidie wana JF
 
Pole Mayenga kwa tatizo ulilonalo la koo. Ushauri wangu utafute Dr. bingwa wa magonjwa ya MASIKIO,PUA NA KOO(ENT) nina imani utapata msaada na tiba ya uhakika.
 
pole mayenga kwa tatizo ulilonalo la koo. Ushauri wangu utafute dr. Bingwa wa magonjwa ya masikio,pua na koo(ent) nina imani utapata msaada na tiba ya uhakika.

nakushukuru sana.
 
Nakushauri nenda tu ukamuone daktari akuchunguze afya yako maana tatizo lako linaweza kuwa linasababishwa na vitu vingi? kama vile aleji ambayo inaweza kukufanya uwe unakohoa kikohozi kikavu, au magonjwa mengine pia yanaweza kusababisha hali hiyo.

ila kwa msaada pendelea kunywa maji mengi sana kila siku ambayo yana joto la kawaida, penda pia kula matunda yatakayokuongezea vitamini C na kuepukana na mavumbivumbi, ikibidi chumba unacholala hakikisha kina usafi wa kutosha kama ni mpenzi wa makapeti ya ndani basi hakikisha yanakuwa safi ili kupunguza vumbi.

by the way pole sana na tatizo linalokusumbua.
 
Nina tatizo la kukaukiwa mate kinywani kiasi kwamba nalazimika kula matunda na kunywa maji mara kwa mara.

Naombeni msaada wa nn nifanye na nijuzeni aina ya ugonjwa maana sijapata msaada kwa matabibu wetu,wananirusha.
 
You may be Dehydrated. Inawezekana haunywi maji ya kutosha. Unatakiwa Kunywa angalao lita tatu kwa siku. Au unapumua kwa mdomo. Hapo itabidi ujifinze kupumua kwa pua
 
Unakunywa maji kiasi gani? acha kwanza vinywaji vyenye kaffeina wakati nikisubiri kusikia kiasi cha maji unachokunywa kila siku
 
Habarini ndugu
Naomba kama mtu anafaham sababu ya kukaukiwa koo anisaidie. Koo linakuwa linakakuka hata nikinya maji haisaidii.
 
Dalili ya ugonjwa wa kisukari.
1.Kiu kubwa
2.kukojoa kupita kiasi
3.Matatizo ya macho.
4.kuchoka haraka.
5.Vidonda kuchelewa kupona.
Hiyo 1,2,3,4 sio lazima kuwa ni kisukari,yapo magonjwa mengine yenye dalili hizo.
 
Hili tatizo limeibuka DSM hapa home tuko watu 3 na rafiki yangu pia amekutwa na hii kitu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom