Tatizo la kukatika Umeme ni Dar es Salaam yote au?

Wadau hivi hii katikakatika ya umeme inayoendelea ni huku kwetu tu au ni jiji zima la Dar? Huku maeneo ya kawe, mbezi beach, tegeta tunateseka sana. Naamini na maeneo mengine hali ni hiyo hiyo. Kwa muda wa karibu mwezi mmoja kumekua na hii shida kwa kiasi kikubwa sana.

Nakumbuka kipindi cha Waziri Kalemani tatizo la kukatika umeme lilipungua kwa kiasi kikubwa sana. Isije ikawa baadhi ya watumishi TANESCO wanataka kumkwamisha Waziri mpya wa Nishati Mh Makamba.
Hata hivyo umeme ni anasa tusiendekeze anasa. Mababu zetu Karne na Karne walitumia mbalamwezi na kuni kwani walipungukiwa nini? Waliishi kwa furaha na Manisha ya kuridhika.
 
Back
Top Bottom