Tatizo la kukatika umeme nchini kumalizika Septemba

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
sospeter-muhongo_210_120.jpg

SERIKALI inatarajia kuzindua mradi mkubwa wa kuboresha miundombinu ya kusafirisha umeme Septemba mwaka huu, utakaomaliza tatizo la umeme kukatika.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema kwa sasa miundombinu ya kusafirishia umeme ni midogo na katika kuboresha hilo, kuna mradi mkubwa utazinduliwa Septemba mwaka huu wa kusafirisha umeme.

Alisema mradi huo ni wa kusafirisha umeme kutoka kilovoti 220 hadi 400 kutoka Dar es Salaam-Tanga hadi Arusha na Iringa-Dodoma-Shinyanga, hivyo tatizo la kukatika umeme litatatuliwa.

Waziri huyo alitoa maelezo hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Korogwe Mjini, Mary Chatanda (CCM) aliyetaka kufahamu lini umeme utakoma kukatika wilayani Korogwe.

Akielezea hilo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani alisema Serikali inafanya marekebisho ya transfoma na chanzo cha umeme cha Hale mkoani Tanga ili kumaliza tatizo la kukatika umeme mara kwa mara wilayani Korogwe na mkoani Tanga kiujumla.

Akijibu swali la msingi la Chatanda aliyetaka kufahamu kama serikali haioni sasa wakati mwafaka Mji wa Korogwe na viunga vyake kuunganishwa na Gridi ya Taifa, Dk Kalemani alisema Mji wa Korogwe hupata umeme kutoka Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Hale kilichounganishwa katika Gridi ya Taifa pamoja na viunga vya mji huo pia vilivyounganishwa kwenye gridi hiyo ya taifa.

Hata hivyo, alisema mji wa Korogwe bado una maeneo ambayo hayana umeme ambayo ni vitongoji vya Bagamoyo, Habitat, Kilole Sabibo, Kitopeni, Kwadungwe, Makwei, Ruengera Relini, Ruengera Darajani na baadhi ya vitongoji vya Mtonga, Kwamkole na Kwasemangube.

Naibu Waziri alisema maeneo hayo yataingizwa katika mpango wa utekelezaji wa bajeti ya Shirika la Umeme(Tanesco) kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Source: Habari Leo
 
hapa Mbeya wamekata umeme sasa hivi..Huyu Muhongo ajiuzulu tu haiwezekani wanakata umeme bila taarifa yoyote Tanesco ni jipu
 
Heading inasema tatizo la kukatika umeme litamalizika mwezi Septemba. Wakati kwa mujibu wa habari yenyewe hiyo Septemba ndipo mradi wa kuboresha miundombinu ya kusafirisha umeme utakuwa unazinduliwa. Au baada ya uzinduzi wake huo mradi utakamilika ndani ya huo mwezi mmoja wa Septemba?
 
Kwa hiyo hamuiamini serikali yenu pendwa??
Hizi kauli kungekuwa kuna system ya kuzi filter kujua zimewahi kutolewa na nani na lini? Ungeshangaa manake ni nyingi na zimewahi kutolewa na karibu kila kiongozi wa hiyo sekta tena zaidi ya mara moja, lakin hazijawahi ku work, sasa kama si porojo ni nin?
 
Heading inasema tatizo la kukatika umeme litamalizika mwezi Septemba. Wakati kwa mujibu wa habari yenyewe hiyo Septemba ndipo mradi wa kuboresha miundombinu ya kusafirisha umeme utakuwa unazinduliwa. Au baada ya uzinduzi wake huo mradi utakamilika ndani ya huo mwezi mmoja wa Septemba?
Habari inasema uzinuzi wa mradi utaanza september haisemi uzinduzi wa ujenzi wa mradi utaanza september.

Means now ujenzi unaendelea, september utakuwa umeshakamilika na utaanza rasmi kutumika
 
Hizi kauli kungekuwa kuna system ya kuzi filter kujua zimewahi kutolewa na nani na lini? Ungeshangaa manake ni nyingi na zimewahi kutolewa na karibu kila kiongozi wa hiyo sekta tena zaidi ya mara moja, lakin hazijawahi ku work, sasa kama si porojo ni nin?
Nyingi zilitolewa nyakati za mkwere.

May be sasa ni zama mpya
 
Tatizo la wachangiaji wengi hawatembei ..miradi ya kV 400 IPO katika hauta za mwisho naenda kaone singida shinyanga Dodoma na mwingine kwingi kwenye barabara Kuu miradi iko wazi mwanaume awpo kazini
 
Habari inasema uzinuzi wa mradi utaanza september haisemi uzinduzi wa ujenzi wa mradi utaanza september.

Means now ujenzi unaendelea, september utakuwa umeshakamilika na utaanza rasmi kutumika
Ahsante mkuu. Kulingana na para ya kwanza isemayo serikali inatarajia kuzindua mradi mkubwa wa kuboresha miundombinu ya kusafirisha umeme Septemba mwaka huu, ni wazi kwamba uboreshaji wenyewe bado kuanza hadi Septemba. Kwa hiyo kwa vile ni mradi mkubwa unaweza kuchukua muda mrefu kiasi.

Hata hivyo kwa ujumla wake hii ni habari njema sana kwetu watanzania.
 
Hizi ngonjera za kawaida tu hakuna jipya....hadi leo mradi wa dart ambao walisema utaanza kazi mwezi wa nne huu ni mwezi wa tano! Hilo tu limewashinda...
 
Ahsante mkuu. Kulingana na para ya kwanza isemayo serikali inatarajia kuzindua mradi mkubwa wa kuboresha miundombinu ya kusafirisha umeme Septemba mwaka huu, ni wazi kwamba uboreshaji wenyewe bado kuanza hadi Septemba. Kwa hiyo kwa vile ni mradi mkubwa unaweza kuchukua muda mrefu kiasi.

Hata hivyo kwa ujumla wake hii ni habari njema sana kwetu watanzania.
Ni kweli kabisa, naona mambo yanaanza kuwa mazuri kwenye hii nchi
 
matatizo ya umeme ni project ya watu au chama fulani. tusidanganyane hayatakaa yaishe. muhongo anatupooza kisiasa
 
aliwahi kusema wkt flan ukfka mgao utakua historia Tanzania,simbachawene nae akaja na kauli yake wakati wa issue ya gas nayo cjui imshaisha humo kwenye mabomba? saiv tena ndo September!! HV tumevurugwa jmn? hapa kazi tu
 
Back
Top Bottom