Tatizo la kukatika umeme hivi sasa siyo kwajili ya Maandalizi ya Elnino bali Uzalishaji umepungua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la kukatika umeme hivi sasa siyo kwajili ya Maandalizi ya Elnino bali Uzalishaji umepungua

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by majege, Sep 20, 2012.

 1. m

  majege Senior Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  ​Nimefuatilia uhusiano wa Tangazo lilitolewa na idara ya Hali ya hewa kuhusu uwezekano wa Kutokea Elnino Mwaka huu na yale matangazo na utekelezaji wa TANESCO wa kukata umeme uliyofuata punde baada ya tangazo hilo.

  Ukitazama kwa kina kuna uwezekano mkubwa kuwa Elnino hiy haitakuwepo, ila lile tangazo lilikuwa limepikwa ili kuhalalisha ukataji umeme. kwani wote tunajua msimu huu kwa kawada kina cha maji kwenye mabwawa yetu huwa kipo chini sana kukidhi uzalishaji unaotakiwa.

  Ukizingatia Serikali kupitia waziri mwenye dhamana alishasema mgawo wa umeme sasa ni historia baada ya kufunga mitambo ya kutumia Gesi ya ubungo imekuwa ni vigumu kurudi kwa wanachi na kauli Tofauti. NAOMBA KUWASILISHA mtazamo wangu.
   
 2. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Siwezi kushangaa kwani serikali hii ya JK ni ya kisanii...
   
 3. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  huu ni usanii ndani ya nchi hii....serikali imekua ikipika mambo kutekeleza agenda zake za siri..........
   
 4. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,371
  Trophy Points: 280
  Bado hamjanishawishi. Mbagala umeme ulikatwa saa 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni, na kweli niliona wanabadili nguzo mpaka usiku na sasa hivi wameshamaliza. Na sio huko tu nimewaona bali katika maeneo mengi hapa Dar.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ni kweli wanafanya hayo matengenezo lakini nadhani wametumia hilo tishio la el nino kama excuse ti. Tunatambua kuwa kazi ya kukarabati miundombinu haipaswi kusubiri hadi kuwe na tishio la mafuriko. Na tunafahamu pia kuwa kina cha maji katika mabwawa kimepungua sana. Tunafahamu kuwa juzi juzi hapa izara iliilazimisha songas kupeleka gesi yote inayozalisha kwa ajili ya kuzalisha umeme. Tunafahamu kuwa IPTL inafanya kazi at full capacity. Kuna kila dalili kuwa hali ya uzalishaji umeme ni mbaya. Waache kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwa sababu tunaona ngozi yetu bado imepauka, haina mng'aro wa mafuta na pia hata harufu ya hayo mafuta hatuisikii
   
 6. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mkuuu,

  Kwli ulilolisema ni la kweli kabisaaaa, Imefika wakati sasa hata vyombo vyetu vya habari vijaribu kutupa matukio yote ya nyuma ambayo tanesco wamekuwa wakitusimulia kila kukicha kwa kuweka visingizio vingi.

  Mradi wa Gesi unarudia tena mara ya pili mara ya kwanza waliweka Budget kubwa kwa ajili ya bomba kubwa la Gesi wao wakaweka bomba ndogo sasa wanakuja na mradi wa pili wa bomba kubwa tena kwa ajili ya gesi huu si wizi wa mchana yani serikali yetu yenyewe yaaaani utendaji wake ni mbovu kabisaaaaaa.

  Huku kuingia kwa soko huria a.k.a Ubinafsishaji wengine walikuwa wameisha uelewa ni wapi watanenepa, na Mwl,JK Nyerere alikuwa anaupinga sana huu mfumo alijua fika kabisa sisi bado ni tungeupokea kwa hali nyingine kabisa na si kwa style hiiii, Viongozi wengi walio pewa dhamana ndio wezi wakuu na wahujumu uchumi kwa sasa na ndio maana wengi walimpinga sana Nyerere na Azimio la Arusha sasa matokeo yake ndio haya kila ukisikiliza hotuba ya Mwl Nyerere utazani alihutubia Jana


   
Loading...