Tatizo la kujilinganisha katika akili za vijana wa sasa

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
5,849
2,000
Kujicompare ni nini labda?! Kujicompare ni ni neno la kiswanglish ambalo linabeba maana ya kujifananisha au kujilinganisha. Yawezekana ni miongoni mwa tabia za kale za mwanadamu ila sina shaka miaka hii ndio imekuwa miongoni mwa tabia ya kuonekana sana katika mienendo ya vijana.
Katika tabia utakuta kijana anakuwa yupo nyuma kimaendeleo katika nyanja zote yaani kiufahamu, kiuchumi na hata kimaumbile muda mwingine lakini hakubaliani na huo ukweli ila anajaribu kujiaminisha vitu ambavyo ni vya kusadikika na mbaya zaidi hushindana au HUJICOMPARE na wale ambao wamemzidi kiuhalisia na anapogundua kuwa hawawezi basi huanza chuki binafsi na huanza kuhamasisha vijana wengine wenye akili kama zake kumchukia au kumfanyia ubaya huyo anayejicompare naye.

Nitawapa mfano ambao wengi mtauelewa, kwa mfano msanii kama Naseeb abdul ama maarufu kama diamond au baba latifa ambaye kwa mbinu zake binafsi aliweza kukwea level za juu za biashara ya muziki wa bongo falvour na kuweza kujipatia mafanikio ambayo si ya kawaida pengine hata kwa wafanyakazi wa taasisi zinazolipwa mishaara mizuri kama mabenki au zinginezo.
Leo hii kuna vijana, baadhi ni wanamuziki ambao walikuwa pengine sawa au hata juu ya diamond lakini kutokana na wao kushindwa kutumia vizuri maono yao wamejikuta wako pale pale kiuchumi na hata jina halikui zaidi ya hapa nchini kuvuka mipaka, na leo wanahesabu mwaka wa 10 au 20 bila bila wakati mwenzao akichanja mbunga kila mwaka kwa mfululizo ndani ya miaka yake aliyoshika maiki ambayo si zaidi ya mitano au sita katika tasinia ya bongoflava. Vijana hawa aidha kwa kusema wazi wazi au kwa majungu wanaishia kujicompare na msanii huyu na kujigundua kuwa hawapo sawa naye basi hubakia kumchukia bila sababu yeyote. Hii ni matokeo ya tabia niisemayo ya kujicompare au kujilinganisha na mtu mwingine.

Huo hapo juu ni mfano tu wa hali hii ilivyo ila najua kwa wewe ambaye hii mada kwa namna moja au nyingine imekugusa utakuwa umeshanielewa ninazungumzia nini hapa.

Utakuta labda mpo kazini, unajitahidi sana kufanya kazi kwa bidii na kwa kujitolea hadi boss wako anakuukubali na kukurecommend katika jambo lolote uwe team leader. Utashangaa miongoni mwa wale unaofanya nao kazi atatokea m'moja au wawili au zaidi ambao watakuchukia ntu bila kosa lolote ati ni kwasababu wao wanajiona ni kama wewe ila hawajaamua tu kuonyesha makali yao sasa iweje wewe ujifanye unajua kuwazidi (unaona hapo sasa kujicompare kunaanza).

Pengine ni mwanafunzi aidha ni sekondari au chuo kikuu......na wakati wa vipindi au presentation wewe upo mstari wa mbele katika kuhoji maswali kwa mwalimu lakini pia kwa kila swali analouliza mwalimu wewe hauachi kunyoosha mkono ujibu hilo swali tena kwa kujiamini bila kuogopa kukosea au kupatia, ila kutatokea wanafunzi wenzako tena back benchers hawa wanakuwa mara nyingi ambao wataanza kunong'ona maneno ya chuki, kejeli, dharau, kufedhehesha dhidi yako eti kwa sababu wao nao wanaakili kama wewe ila hawakuamua kujibu tu maana wao ni wagumu na hawapendi kujishow darasani(unaona ujinga wa kujicompare huo)

Utakuta upo mtaani busy na maisha yako huna story na mtu unatoa salamu ila huna muda na maisha ya wengine kwa maana ya kufuatilia nani kala nini leo nani kafanya nini ambacho hakitakupunguzia wala kukuongezea chochote hata. Kuna watu watatokea na watashindwa kukubali kuwa wewe si kama wao watataka kujicompare kuwa wao na wewe ni sawa wakati ukitazama uhalisia wao muda wao wanatumia kufuatilia watu wengine, hawana maendeleo, simu zinavifurushi vya kukopa, meseji zao ni tafadhali nipigie, wao na wewe wapi na wapi?

Hii tabia imekuwa sugu sana kwa vijana wa sasa kiasi kwamba watu wanaweza kukuchukia bila sababu sababu tu huwa wanatumia muda wao kukuchunguza na kukufuatilia kwa chini chini huku wakikusambazia maneno ya kukuharibia au kukuchukiza bila sababu yoyote ya msingi. Tabia hii si nzuri na huwakuta vijana ambao wanaishi kwa akili za kuazimana ama 'mob psychology'. Vijana wenye hulka ya namna hii si wazima na wanaonyesha kuwa hawajapevuka na kukomaa kiakili kama inavyotakiwa.

Vijana wenye mfumo wa maisha wa kujicompare na wengineo ni ngumu sana kufanikiwa kimaisha maana huwa na udhaifu mkubwa katika kujitambua wao ni nani na wanamajukumu na wajibu gani katika jamii inayowazunguka.

Hii tabia ni kama Uchawi wa miaka hii. Maana watu wa namna hii hufikia hata hatua ya kukutolea upepo katika tairi ya gari yako kisa hasira tu za kuwa ulipo nao walitaka kuwapo sasa iweje uwepo wakati wao wameshindwa kufikia hapo......hivyo kwakuwa wanalazimisha uhalisia ufanane na akili zao za kitoto ndio mwishowe wanajikuta wamefanya vitu vya ajabu ili wakuharibie ili ushuke muwe sawa wafurahie na roho zao za kufeli maisha.

Hii hali ilishanikuta juzi kati nilipokwenda brela kusajiri jina la kampuni. Yaani jamaa anakubania wazi wazi kwamba anachukia kijana mdogo unakuwaje na kampuni wakati yeye alitaka kumiliki kampuni siku moja ila ameshindwa kwasababu hakuwa serious na mipango ya maisha yake. Basi atakutajia msululu wa vitu ambavyo utahitajika kupeleka ili usajiriwe na bado ukimletea atataka kukufanyia figisu ili usifanikishe hayo malengo ndio maana vijana wengi huona ni inshu kusajiri kampuni hapa tz maana hulalamikia urasimu unaosababishwa na wafanyakazi wenye chuki binafsi na watu wasiowajua hata kidogo.

VIJANA ACHENI TABIA HII YA KUJICOMPARE NA WALE MNAOWAHISI KUWA WAMEWAPITA. Kama umeona umeshindwa muombe msaada akuonyeshe njia na kama hiyo nayo ni shida basi jitathimini wewe binafsi madhaifu yako ni kwanini unashindwa na anakushinda usipoteze muda kufuatilia maisha ya mwenzako.............ukimfuatilia na kumchukia wewe utapata nini na ni muda gani unafanya maisha yako binafsi na maendeleo. Acheni ujinga ujinga vijana wenye hii tabia.:mad::mad::mad::mad::mad:
 

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
5,849
2,000
Halafu wewe jamaa ukishalewa ni lazima uje hapa jukwaani watu wajue unajua kusoma na kuandika? Nyie ndio mnaochangia Magufuli aone kuna hela kama mnalewa mapema hivi.
ha ha ha ha ngoja naendelea bob
 

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
5,849
2,000
Karibuni wadau tujadili mada na pia mfanye kuwaarifu wale wenye hii tabia waache maana haina faida kwao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom