Tatizo la kujikojelea .... kwa mtoto wa miaka 8-10

KUNA WATU WENGINE KWA KUONGOPA USUMBUFU WA KUAMKA USIKU KUWAPELEKA CHOONI WATOTO WALIWAZOESHA MAMPASI, HAYA NDO MAZARA YAKE.
 
Wakuu ...Naomba msaada wa Tiba ya mtoto anayejikojelea kitandani kila siku.

mtoto wa miaka 10
asanteni.
Mkuu MPUNGUZIE vinywaji vya VIMIMINIKA mfano maji,,soda ,,juice,NK...na mtoe KUKOJOWA USIKU MARA KWA MARA,,,,,EPUKA USHAURI wa waganga wa KIENYEJI,,,,yupo NDUGU YNGU tena MTU mzima kabisa alikuwa na tatizo kama hilo,,YALIMKUTA MAKUBWA,,,zaidi ya KUKOJOWA,,,KITANDANI....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaribu kumpeleka hospitali nahisi anaweza tibika, kuna mtu mmoja aliwahi kuwa na mtoto mwenye tatizo hilo akampeleka hospitali akapona, walisema alikuwa na tatizo homoni zinzohusiana na mambo hayo, nitajaribu kufatilia na kama nikipata majibu sahihi nitautafuta uzi huu nikupatie mrejesho..
 
Kuona daktari hili tatizo kilo kwenye ubongo zaidi. Kama mdau aliposema hapo juu apunguze kunywa maji msaa mawili kabla ya kulala pia muwe na alarm ya kumuamsha aende haja ndogo
 
Wakuu ...Naomba msaada wa Tiba ya mtoto anayejikojelea kitandani kila siku.

mtoto wa miaka 10
asanteni.
Tafuta kwenye famasi dawa inaitwa imipramine au Amitriptylinne umpe usiku kabla ya kulala...
Kienyeji wanasema "eti"....ukimpa maji yaliyopatikana kwa kuchemsha ndevu za mahindi atapona
 
Tafuta kwenye famasi dawa inaitwa imipramine au Amitriptylinne umpe usiku kabla ya kulala...
Kienyeji wanasema "eti"....ukimpa maji yaliyopatikana kwa kuchemsha ndevu za mahindi atapona
Hiyo dawa ya kienyeji ndio dawa nilipo kua primary kunawanafunzi walikua wanaongelea na kutoa ushahidi wamepona.Chukua maindi makavu na siyo ndevu za maindi chemsha Lita moja ya maji kwa maindi kikombe cha chai,yakitokota epua yaache ya kwa siku moja.Uanze kumpa kikombe kimoja kila siku asubui kwa muda wa Siku tatu adi nne.

Hiyo hali ya kukojoa kitandani itapote ata kama alikua anakojoa kila siku.Wazee wa zamani wanasema mtt akinywa maji ya maindi yaliyo lala akitaka kujikojolea atasikia harufu itakayo mfanya azuie mkojo na kuamka kwakuwa itamkera ila sina uhakika na hii theory ya wahenga ninacho amino nikwamba dawa ya maji ya maindi inafanya kazi.
 
Back
Top Bottom