Tatizo la kuhamisha pesa kutoka M-pesa kwenda CRDB

Easymutant

R I P
Jun 3, 2010
2,564
1,129
Sijajua ni mimi tu ninayepata hili tatizo ambalo limekuwa la kudumu kwa muda mrefu sana, Kuhamisha pesa kutoka mobile money hususani M-pesa kwenda CRDB inachukua muda mrefu sana na hata ukiwapigia simu is either watakwambia wapigie Vodacom M-pesa kwa madai kuwa wao hawajaona hiyo transaction ili hali umeshapokea message ya M-pesa kwamba wao washatuma (Customer care wa CRDB ni ka jipu kengine)... Ukiwaeleza M-pesa customer care wanakwambia wapigie CRDB huku muamala umeshakwenda CRDB)

Jana usiku nimefanya kuhamisha pesa kutoka M-Pesa to CRDB hadi sasa muamala haujaonekana kwenye account ya CRDB nawapigia customer care (customer kero) wanasema itawekwa Jioni ya leo au Kesho asubuhi..

Sijui kama lengo la hii system ilikuwa kurahisisha au kukwamisha maana kama una kitu cha kibiashara cha haraka unajikuta CRDB wamekukwamisha.
 
Hilo tatizo lipo sana ila nilikuja kugundua wenye tatizo ni vodacom maana ukifanya muamala kwenda mitandao mingine unafanyika ndani ya sekunde 30. Nimejaribu mara nyingi unakuta wanakuambia kuna tatizo kati ya m-pesa other ila muda ule ule ukijaribu tigo pesa au airtel money inakubali
 
Back
Top Bottom