Tatizo la kichomi ni moja ya dalili za ugonjwa Moyo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
VIJANA wengi leo nyumbani Bongo wanapatwa na maradhi ambayo zamani yalikuwa ya wazee au watu wa makamo. Maradhi haya ni kama kisukari na mstuko wa moyo.

Kichomi ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya. Ukipatwa muda mrefu au kila wakati ; basi chunguza zaidi.

Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa.
  1. Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi (acid) kuzidi
  2. Dalili za ugonjwa wa moyo uitwao Ischemic
Jambo la kuangalia ni je?
  1. Unashikwa kichomi ukiwa unatembea?
  2. Umeinama au umelala
  3. Ukishakula chakula
Kama unapatwa kichomi wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali ina maana kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo.

Kama unapatwa kichomi baada ya kula ina maana kuna tatizo katika chakula unachokula. Je mlo wako una acid(uchachu) sana? Je, unakula vyakula vyenye pilipili na binzari(spices) kwa wingi sana? Kama una kula sana vyakula

vyenye asidi ina maana tumbo lako halimengenyui sawasawa linachoka.
Kawaida binadamu unabidi kubadili badili ulaji. Usirudie vitu fulani fulani kila siku. Mathalan usiweke pilipili katika kila mlo.
Tatizo jingine ni ulaji wa chakula chenye chumvi nyingi sana. Chumvi inakorofisha pia mzunguko wa damu mwilini.
Hasa kama hunywi maji.

Kama unapatwa kichomi ukiwa umelala au umeinama ina maana kuna tatizo pia la mzunguko wa damu ndani ya moyo au kwenda moyoni. Labda una tatizo la unene (je unafanya mazoezi ya kutosha?) kama unafanya mazoezi, je unafanya mazoezi ya aina gani?
Kuna mazoezi ya aina mbili.
Mazoezi ya nguvu na haraka (cardio vascular); kama kukimbia, mpira, ngumi, kuinua vyuma nk.

Au mazoezi laini yanayofanywa kwa kukihimili (isometric) mathalan ukiweka mkono upande mmoja wa kichwa huku ukisukuma kichwa kisukumane na mkono, unafanya tizi la kuongeza nguvu ya shingo. Zoezi aina hii linaitwa Isometric.
Aina ya mazoezi ya aina hii ni kama Yoga, Pilates na baadhi ya mitindo mbalimbali ya mapigano yaani masho ati mathalan Tai Chi ya Kichina.
Tizi la Yoga zuri sana maana limetulizana:






Pilates si tofauti sana na Yoga ni kama ndugu wa karibu. Ila Pilates inafafanua zaidi mambo mengine kama tumbo nene:

NI muhimu kuchanganya mazoezi haya mawili. Yaani ukishafanya mazoezi ya nguvu, ya kuhema unatulizana.
Kama una kichomi cha mara kwa mara yaweza kuwa ni dalili za ugonjwa wa moyo, kisukari au mambo mengine. Kuondokana na mambo haya:

  1. Kamwone mganga wa moyo
  2. Kama huna ugonjwa wa moyo angalia unavyokula. Je, unakula sana vyakula vya mafuta
  3. Punguza ulaji wa mafuta au vyakula vizito jaribu kula zaidi samaki ambao huwa na mafuta yasiyoumiza mwili.
  4. VITUNGU SAUMU VIBICHI vinasaidia sana kukinga moyo, matatizo ya mafuta, lakini tatizo ni harumu mbaya ya mdomo. Hivyo unaweza kuwa unachanganya na mboga nyingine za saladi unapokula mlo kila siku. Kama nyanya, matango, nk.
Mbali na ulaji suala la mapumziko ya kutafakari au kwa kimombo Meditation limefanyiwa utafiti na kuonekana kwamba linasaidia sana maradhi ya moyo, akili na stress ya mwili kwa ujumla. Jaribu hizi hapa chini, ukiweza dakika kumi hadi 20; mara mbili kwa siku, kufuatana na muda ulio nao.




2. KUVUTA PUMZI




3. KULALA CHALI HUKU UNAVUTA NA KUPUMUAhii ni aina ya masho ati ya Kirusi ambayo inasisitiza Uvutaji pumzi sahihi.
Inaitwa Systema.



TATIZO LA KICHOMI NI MOJA YA DALILI ZA UGONJWA MOYO… « kitoto
 
Last edited by a moderator:
Wakuu.

Naomba kujua dalili za ugonjwa wa Moyo.

Sijawahi kushuhudia moyo ukinienda mbio au kupiga kwa kasi kama wakati huu, je dalili ni zipi hasa nimeenda hosptali kupima Bp wakasema sina Bp
je inawezekana na wasiwasi au mfadhaiko tu wa maisha au ni nini.
 
Wakuu.

Naomba kujua dalili za ugonjwa wa Moyo.

Sijawahi kushuhudia moyo ukinienda mbio au kupiga kwa kasi kama wakati huu, je dalili ni zipi hasa nimeenda hosptali kupima Bp wakasema sina Bp
je inawezekana na wasiwasi au mfadhaiko tu wa maisha au ni nini.
Kama bado upo nitafute ni kusaidie
 
Wakuu.

Naomba kujua dalili za ugonjwa wa Moyo.

Sijawahi kushuhudia moyo ukinienda mbio au kupiga kwa kasi kama wakati huu, je dalili ni zipi hasa nimeenda hosptali kupima Bp wakasema sina Bp
je inawezekana na wasiwasi au mfadhaiko tu wa maisha au ni nini.
Moyo kwenda mbio Ni hatari nenda kwa cardiologist ukapime
 
Back
Top Bottom