Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 220,708
- 728,539
Kama bado una kumbukumbu na hotuba ya JK aliyoitoa mara baada ya kuapishwa kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; hivi majuzi tu, aliahidi kuwasiliana na NEC ili kuona uwezekano wa marekebisho yanayoweza kufanyika kwenye Tume hiyo na hivyo kujenga mazingira ya kuboresha chaguzi zijazo..........................................
Tatizo kwa JK ni kutokuona NEC haina sababu ya kufanya marekebisho yoyote ya maana ila Bunge ndicho chombo cha kikatiba ambacho kina ridhaa ya kuifanyia marekebisho hiyo Tume ili kuhakikisha chaguzi zijazo zinafanyika kwa uhuru na haki na kuondokana na misuguano ambayo yaweza kuhatarisha usalama wa taifa hili.............................
Nchini Kenya mara baada ya umwagaji damu wa mwaka 2007/08 Bunge lao lilipitisha sheria ya kuvunjwa kwa Tume na kuanzishwa kwa Tume nyingine ambayo ina wajibika moja kwa moja bungeni.............................Hata mahojiano ya wasailiwa wa nafasi nyeti za makamishina za Tume hiyo mpya iitwayo IIEC yaani Interim Independent Election Commission of Kenya ambayo ilichukua nafasi ya ECK au Election Commission of Kenya...................................
Baada ya kamati ya Bunge kupitisha majina ya wateule wa kuiongoza Tume hiyo mpya waliwakilisha majina kwa Raisi Kibaki kwa uteuzi na bunge kuyabariki................utaratibu huu unaondoa kabisa dhana ya Raisi kama taasisi kujiona ina miliki namna na jinsi chaguzi kufanyika huku nayo ikiwa na masilahi mazito kama mgombea wa nafasi ya Uraisi na kwa mavuno ya chama chake cha kisiasa........................
Hivyo katika marekebisho ya NEC kikwazo kikubwa ni JK ambaye ni mhubiri mzuri wa kuwatuhumu wengine kuchochea umwagaji wa damu huku kimya kimya yeye mwenyewe anaandaa mazingira ya nchi kumwaga damu kwa kuzuia kabisa mageuzi ya kisiasa katika uendeshaji wa taifa hili.......................
Adui yetu mkuu hivi sasa ni JK katika mageuzi ya kisiasa kwa sababu ndiye anayekwamisha jitihada zote za kulitoa taifa hili katika mifumo mgando ambayo isiyoshirikishi kwenda kwenye mifumo endelevu ambayo ni shirikishi kwa jamii nzima......................