Tatizo la 'Jinsi Ya Kufunga' Ni Janga La Taifa

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Dakika ya pili tu ya pambano tumepoteza nafasi! ..na zikafuata chance nyingi za wazi tukashindwa kuzitumia...

Kwangu mimi nawapongeza stars kwa mchezo mzuri waliojaribu kutuonyesha lakini wamekua na shida hiyo moja kubwa ya jinsi gani ya kutumbukiza mpira wavuni...

Hizi kosa kosa hazikuanza mechi ya leo..hata game ambazo tulishinda..unakuta kumbe tungeweza shinda goli nyingi zaidi...

Mfano mzuri mwingine kuwa tuna shida hiyo niliuona juzi kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Mlandege ya Zanzibar....Mchezaji Makambo alipata nafasi nzuri akaitumia vema kirahisi akafunga.....muda baadae mchezaji Kaseke akapata nafasi kama ile ya makambo akiwa analitazama goli.jirani kabisa..tena ndhani hata kipa alishapotea hakuwepo golini...kaseke akapaisha le mpira kwa kimo cha mnazi.....pale pale nikzidi kujifunza kitukuwa tuna shida kama nchi.

Yaliyotokea leo niliyahisi lakini nikashangaa wa tz wengi wakawa na imani kuwa tunashinda

Ifikie wakati sasa kutengeneza timu yetu hasa kuimarisha idara ya ushambuliaji/jinsi ya kufunga/mafunzo mengi ya saikolojia vitendo na nadharia.na mwsho tuendelee kutengeneza vipaji/vizazi vipya vya baadae.
 
Goli alilofunga mayele jana dhidi ya Kmkm mtanzania hawezi kabisa kufunga style ile.....
Pia jana imezidi dhihirika kuwa wageni ndio hasa wenye kujua kufunga kuliko wazawa..ushahidi ni jinsi gani kmkm walivyokua wakipaisha mipira wanapolifikia goli la yanga
 
Wanapaisha makusudi ukute nao ni mashabiki wa yanga pia
 
Wachezaji Akina Kibu Dennis hawafanyi mazoezi ya kufunga goli.
Mipira mingi wanapaisha hawajifunzi kupiga na kunyoosha mpira golini.
Nimemkumbuka Mwaikimba.
Soka na upeo mzuri wa elimu vinakwenda sambamba.

Unakuta mchezaji kaishia la 7 wazazi wake wameangaika kumpatia elimu bora lakini uwezo wake umeishia hapo unategema afanye vizuri kwenye soka lenye maamuzi ya haraka anapokuwa na mpira?

Wale ambao hawana elimu lakini wanafan6a vema wengi wao ni mazingira magumu ya maisha waliyokutana nayo la sivyo kielimu wangekuwa mbali sana
 
Inashangaza Sana.
Mchezaji amepata ajira ya kusajiriwa yenye mshahara mnono tu, lakini anarudia makosa yale yale kila mechi.
Na wala hafanyi juhudi ya kuyarekebisha kwenye mazoezi binafsi au akiwa na timu yake ili awe bora zaidi.
Hoja yako ya Elimu duni ni moja ya sababu, na kuto kujitambua.
Utastaajabu mchezaji mshambuliaji hawezi hata kupiga faulo. Ni kupaisha tu miaka nenda rudi.
Wachezaji wetu wakitoka uwanjani wanachofikiria ni kukaa viti virefu tu na kupenda kusifiwa.
Ndio maana Nchi yetu haina washambuliaji makini.
Hao Akina Messi pamoja na vipaji walivyonavyo wanajifua kila kukicha ktk mazoezi binafsi ndio maana wanakuwa bora zaidi na zaidi.
Ni jambo la kushangaza sana nchi yenye watu karibia milioni hamsini, vijana wa kiume wapatao milioni kumi na tano, tunashindwa kupata mshambuliaji
makini.
Tunabaki kuwalilia vikongwe wa kigeni Akina Okwi, Makambo, Chama, na wengineo wanaotoka nchi za jirani.
Ni aibu kwa Taifa.
 
Soka na upeo mzuri wa elimu vinakwenda sambamba.

Unakuta mchezaji kaishia la 7 wazazi wake wameangaika kumpatia elimu bora lakini uwezo wake umeishia hapo unategema afanye vizuri kwenye soka lenye maamuzi ya haraka anapokuwa na mpira?

Wale ambao hawana elimu lakini wanafan6a vema wengi wao ni mazingira magumu ya maisha waliyokutana nayo la sivyo kielimu wangekuwa mbali sana
Hii ni kweli ujiangalua hata wachezaji wa zamani waliowika sana elimu yao ilikuwa kubwa na upeo wao ulikuwa mkubwa na hata wengine walitoka timu za taasisi kama watumishi wa serikali.......mtu kaishia la 7 au form 4 failure brain capacity na utayari wa kujifunza na kuelewa falsafa za kocha na mifumo ni ngumu ...elimu ya soka hasa delivery ya kocha na.system ya elimu ya kawaida ni.almost the same...

Kuna kocha mmoja alishasema wachezaji wa kitanzania hawafundishiki
 
Back
Top Bottom