wakuu,
hapa JF Dr kunana uzi huu:
https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/210330-tonses.html
Dr Nguruvi3 alikuwa amemjinu mtoa mada kama nilivyoquote hapo chini:
sasa mheshimiwa Dr. Nguruvi 3 na wengine
naomba kujua zaidi hapo kwenyered.
Nina mtoto wa miaka mitatu sasa na amekuwa akipata joto la mara kwa mara miguuni na kichwani kwa kama mwezi mmoja sasa. daktari kasema ana infection kwenye damu na kifua. amempa sindano za powersif na antibiotics.
1. ni namna gani nyingine ambazo huenda hiyo infection kwenye damu ilimuingia mwanangu (kumbuka hajawahi kuwa na tatizo la tonsils maishani mwake). na je,
2. nini kifanyike kuzuia maambuklizi kama hayo kwa siku za usoni? na mwisho, je,
3. hayo matibabu aliyopewa ni sahihi kwa tatizo lake au niendelee kutafuta utaalam zaidi??
asanteni sana wakuu
heri ya mwaka mpya 2012!
hapa JF Dr kunana uzi huu:
https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/210330-tonses.html
Dr Nguruvi3 alikuwa amemjinu mtoa mada kama nilivyoquote hapo chini:
Ni uvimbe katika Tonsils za kwenye koo na husababishwa na virus au bacteria. Unatibika kwa dawa kutegemeana na aina ya mdudu hasa wale bacteria. Moja ya bacteria maarufu wanaitwa streptococcal. Inapotokea ugonjwa kujirudia basi mgonjwa hufanyiwa operesheni ndogo inaitwa tonsillectomy, yaani wanaondoa tonsil. Hii inazuia kujirudia rudia ambako kunaweza kuleta complications. Wadudu kama strept wanaweza kusababaisha kitu kinaitwa peritosillar absess(Quinsy) na kuweza kusababisha mambo kama
infection katika damu(septicaemia), au sehemu nyingine kama figo na moyo.Ingawa complication hutokea nadra lakini huwezi jua hiyo nadra itatokea wapi. Ikimtokea mtu wako sio nadra ni madhara kamili.
Ningekushauri uwaone wataalam(ENT) ukiwaeleza kujirudia rudia kwa hali hiyo na kama zipo kumbu kumbu wapelekea ili wabaini ukubwa wa tatizo.
Dhana hii ya vitu baridi imeenea sana, hakuna mahali kwenye medical iterature imeelezwa. Haina ukweli. Ni Bacteria au virus. Kama ni virus huwa 'self limiting' kwasababu hakuna dawa ya kutibu virus.
Mara nyingi huwa ni bacteria ambao wanatibika kwa dawa za kawaida kabisa. Tatizo ni pale kunapokuwa na usugu na kujirudia rudia. Kinachotokea hapo ni kuwa hao bacteria wanaweza kupata access kwa kwenda sehemu nyingine na huko wakasababisha madhara makubwa zaidi. Hiyo ndiyo inaitwa complication. Kwa medical terminology, complication ni matokeo ya tatizo fulani. Kwa mfano bacteria wakitoka kwenye tonsils nakuingia katika damuhalafu kutua katika figo na kusababisha 'Glomerulonephritis', basi maradhi ya figo ni complication ya untreated tonsilitis.