Tatizo la Gesi

Kabathe

Member
Jan 18, 2011
23
5
Sote tunapenda kihifadhi mazingira
Tunapenda hewa safi na mazingira yenye kijani kibichi ya kuvitia
Kwakuwa umeme wa Tz si wa uhakika, kwa wapenda mazingira gesi ndo ilikuwa mkombozi
Katika kipindi cha mwaka mmoja bei ya Gesi imepanda si chini ya mara nne
na kwa sasa pamoja na bei kupanda Hakuna Gesi ktk vituo vingi.
Katika hali hii ya mgao wa umeme, inatulazimu si kwa kupenda, si kwa kuto kujua madhara ila hatuna namna bali kutumia mkaa.
 
Hiyo government ya jk.........

Chakushangaza hukana hata kiongozi anayelizungumzia hili........

Then wanasema tusikate mti..........
 
Mi naona kama tukipigana kidogo ndio tutaheshimiana........

Ila siombei vita.........kuna nchi bei za mikate zikipanda wanaandamana mpaka kesho...
 
Inasemekana meli kubwa ya ORYX iliyokuwa inaleta gas imeshindwa kufika baada ya tishio la maharamia wa kisomali kutishia kuiteka,,hata hivyo mimi nilidhani tunatumia ya songosongo!!
 
Kwa hali hio si ya kusubiri mtawala atoa tamko, ni sisi wananchi kutoka barabarani kupinga ongezeko hilo lisiloenda sambamba na maisha ya watanzania walio wengi !!!!

Hivi na tukiamua kuandamana kupinga ongezeko la bei katika bidhaa muhimu inabidi tuombe kibali toka kwa Mwema au ????
 
Maharamia wa Kisomali wachelewesha gesi kuingia nchini

Na Richard Makore ,
18th January 2011
Serikali imesema uhaba wa nishati ya gesi katika vituo vya mauzo nchini, ulitokana na maharamia wa Kisomali kuzuia meli kubwa ya kampuni ya Oryx katika Bahari ya Hindi, ambayo ilikuwa njiani kuja nchini kuleta nishati hiyo.
Kauli hiyo ya serikali ilitolewa jana na msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Alyoce Tesha alipozungumza na NIPASHE kuhusu madai ya kuwapo uhaba wa gesi katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Tesha alisema baada ya meli hiyo kubaini kuwapo kwa tishio la maharamia kutaka kuiteka, ilirudi ilikotoka kuomba ulinzi zaidi kabla ya kuanza tena safari yake ya kuja nchini.
Alisema meli hiyo muda wowote inatarajia kutia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam na kupakua nishati hiyo na kuanza kuisambaza maeneo mbalimbali.
Tesha alisema meli nyingine ya Oryx, ipo njiani ikiwa na shehena kubwa ya gesi na kwamba, baada ya nishati hiyo kuingia kwa wingi, bei itashuka.
Wananchi wengi hivi sasa wanatumia gesi kwa matumizi ya nyumbani baada ya bei ya umeme kuwa juu.
Kutokana na uhaba wa gesi, hivi sasa nishati hiyo katika vituo hivyo imepanda mara mbili, ambapo kilo 15 ya mtungi wa gesi, zinauzwa kwa Sh. 70,000, badala ya Sh. 35,000.
Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE katika vituo hivyo na kuzungumza na wauzaji umebaini kuwa kuna uhaba mkubwa wa nishati hiyo, hali ambayo imewafanya wapandishe bei.
Baadhi ya vituo vinavyouza gesi, vilisema vinatarajia kuingiza gesi hiyo nchini, kuanzia keshokutwa.



CHANZO: NIPASHE
 
hivi gesi ya songosongo haiwezi kutumika kupikia? kama inaweza tatizo ni nini haiwekwi kwentye mitungi?

macinkus
 
Back
Top Bottom