Wadau wa JF,
Kuzoea tatizo sio kutatua tatizo naona sasa tumeshazoea hii ya kutumia masaa mawili kutoka Ubungo mpaka Posta inafika wakati tunaona ni sawa. Tunajua kuna ahadi za kujenga barabara za juu (flyovers) lakini pia kulikuwa na mawazo ya kujenga barabara za kuzunguka jiji letu la Dar (ring road) hivyo hii imefikia wapi.
Kulikuwa na tetesi sana ya kupunguza magari kuingia mjini haswa maeneo ya Ubungo kwa kuhamisha kile kituo pale kilipo kutawanya kwenye barabara ya Morogoro nje ya mji, Kilwa Road na barabara ya Bagamoyo haya yanafanyiwa kazi au ndio tushazoea shida?
Du juzi nimetumia masaa 2 na nusu kutoka Kimara mpaka Posta nikachoka sana. Wakuu wa nchi hebu hili nalo tuliangalie kwa kuchukua hatua hata kama ni kidogo kidogo. Kwa mfano hiki kituo cha Ubungo mbona bado hakijahama tatizo nini?