Tatizo la engine ya gari lako kuzimazima (Engine Stalling)

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
3,327
9,321
Asilimia kubwa ya matatizo ya engine kuzimazima yanasababishwa na components za umeme kama Sensors, Valves, solenoids n.k.

Engine inaweza kuzima muda wowote mfano wakati ipo idle, wakati unaaccelerate, wakati unafunga brake n.k.

Sababu zote zinazoweza kupelekea tatizo hili zinaingia katika makundi haya matano.

1. Loss of spark(kukosekana cheche kwenye engine)
Distributor

Hii hupeleka high voltage kwenye spark plug kulingana na firing order na katika muda sahihi. Pia baadhi ya distributor huwa na hall effect au magnetic mechanism kwa ajili ya timing kwenye ignition. Kama ikiwa na tatizo inaweza kupelekea umeme usifike kwenye spark plugs au kufika katika muda ambao si sahihi na hivyo kukosekana kwa cheche kwa wakati sahihi.

Coil on plug/Spark plug/spark plug wires/Ignition coil

Kama chochote kati ya hivi nilivyotaja hapa kikiwa kina shida inaweza kupelekea kukosekana kwa cheche au kuwa na cheche zisizo na nguvu kabisa. Hii inaweza kupelekea engine yako kuzima.

Crackshaft position sensor

Hii huwa na kazi kubwa tatu ambazo ni kufanya timing kwenye ignition, kupeleka RPM signal kwenye ECU na mwisho ni kujua speed ambayo engine inazunguka. Nayo pia kama ikileta shida basi engine yako itakuwa inazimazima.

Camshaft position sensor

Hii ndio sensor ambayo hujua ni cylinder gani firing inafanyika na kuweza kuestablish injector synchronization na coil firing sequence kwenye gari ambazo zinatumia Direct Ignition System (DIS). Hivyo kama nayo ikiwa na fault gari inaweza kuwa inazimazima.

2. Loss of fuel(Kukosekana kwa mafuta kwenye engine)
IAT sensor

Sensor hii ambayo husoma joto la hewa linaloingia kwenye engine ikiwa na shida basi huleta matatizo. Kama sensor hii inapeleka signal ya HOT tu basi engine itakuwa inapokea mafuta machache na hivyo hupelekea gari kuzimazima ikiwa umeliwasha bado la baridi(Hard cold start) au misi wakati wa asubuhi au engine ikiwa ya baridi. Kuna magari mengi hii sensor huwa inawekwa kwenye housing moja na MAF sensor, Hivyo mtu anaweza kuona alibadilisha MAF kusolve tatizo kumbe shida ilikuwa IAT sensor.

ECT sensor

Kama ilivo IAT sensor hii nayo huwa na tabia ya kupeleka signal ya HOT tu sometimes. ECU hudhani engine ni ya moto na hivyo kupeleka mafuta kidogo. Kama ni wakati wa asubuhi basi lazima gari itamisi na kuzimazima.

Oxygen sensor au A/F ratio sensor

Hii sensor hueleza hali ya engine kama ni Lean(mafuta kidogo) au Rich(mafuta mengi) kulingana na chemical reactions zilizofanyika kati ya exhaust gases na heating element. Kama signal ya too rich pekee ndio itakuwa inaenda kwenye ECU basi ECU itapunguza kiasi cha mafuta kinachokuja kwenye engine. Na hivo engine yako inaweza kumisi au kuzima.

Fuel pump

Kama fuel pimp ikiwa na fault inaweza kuleta mafuta kidogo au katika pressure ndogo. Hii inaweza kupelekea engine yako kumisi au kuzima muda wowote.

Injector Nozzle

Hizi sanasana kama zimeziba ndio huwa zinaleta shida. Ikiziba inaweza ikapitisha mafuta kidogo au isipitishe kabisa. Yote mawili yanaweza kupelekea engine yako kuzimazima.

3. Load(Mzigo mkubwa kuliko uwezo wa engine)
Mzigo siyo lazima uwe ule ulioubeba kwenye gari yako. Hata components za gari lenyewe zinaweza kusababisha load kwenye gari yako. Mifano ni

Torque converter.

Kwenye transmission kuna muda torque converter linapoanza kuharibika huwa lina kawaida ya kuengage clutch yake muda wowote, hivyo kama gari ikiwa idle basi lazima tu itazima kwa sababu mzigo utakuwa umeongezeka ghafla kwenye engine.

Torque converter clutch solenoid.

Kama ilivo kwa Torque converter pia TCC solenoid ikianza kufa huwa kuna muda inaamuru clutch ya torque converter iengage au ifanye delay kwenye kudisengage. Kama ikiengage wakati gari ipo idle basi engine itazima. Ikichelewa kudisengage wakati unaendesha gari yako itazima wakati wa kufunga brake.

MAP sensor

Hii ndio sensor inayodetect kiasi cha mzigo ambacho kinaendeshwa na engine. Mara nyingi ikifa diaphram yake huwa inatoboka hivyo taarifa kwenye ECU kwamba hakuna load yoyote, Hivyo mafuta yataletwa kidogo kwenye engine hata kama hewa inaingia nyingi. Hivyo engine inaweza kukosa nguvu na kuzima.

4. Kiasi kidogo/kikubwa cha hewa kwenye engine.(Mara chache)
Hii husababishwa na.

Air filter

Yes Air filter ikiziba lazima utakosa hewa ya kutosha kwenye engine hivyo hata mafuta yataletwa kulingana na hewa iliyopo. Hivyo haitazalishwa nguvu ya kutosha na hivyo engine inaweza kuzima.

Idle Air Control Valve(IACV)

Hii ndio valve inayohusika na kucontrol kiasi cha hewa kinachoingia kwenye engine wakati gari ipo idle (sailensa). Kama hii valve imekufa au imejaa carbon basi sailensa itakuwa inajipandisha au kujishusha yenyewe na kila siku utakuwa unaadjust. Ikiwa inajipandisha engine itakuwa inatumia mafuta mengi na kama inajishusha basi engine itakuwa inazimazima.

Throttle Position sensor

Hii kuwa inakuwa na resistive element ambayo kama itachubuka sehemu basi gari inaweza kuzima wakati unakanyaga accelerator.

Exhaust Gases Recirculation(EGR).

Kama EGR valve ni mbovu au imejaa carbon au solenoid yake imekufa basi inaweza kuleta shida hasa wakati engine ni ya baridi. Kama engine ni ya baridi basi unapowasha gari EGR valve inatakiwa kuwa imefunga. Kama itakuwa wazi lazima gari itamisi au kuzima kabisa.

MAF sensor

Hii huwa inapima flow rate ya hewa ambayo inaingia kwenye engine. Kama ikiwa na fault na ikawa inapeleka taarifa kwamba flow rate ni ndogo basi lazima mafuta nayo yataletwa kidogo. Hivyo kuna muda engine inaweza kuwa inazimazima.

5. Matatizo kwenye mifumo ya umeme.
Pia kama Battery au Alternator ya gari lako ni mbovu basi unaweza kukumbana na hii changamoto. Pia kwa sehemu kubwa ni relays zinaweza kusababisha hili tatizo. Niliwahi kuelezea kwenye uzi wangu mmoja kwamba relays zinapoanza kuchoka huwa zina tabia ya kuzima unapokuwa na electrical load kubwa.

Nimejitahidi kucover vitu vingi kadri nilivyoweza. Ingawa pia vinaweza vikawepo vitu vingine ambavyo vinaweza kupelekea engine yako kuzimazima. Kwa mfano leaks kwenye baadhi ya pipes n.k.
 
Engine inaweza kuzima muda wowote mfano wakati ipo idle, wakati unaaccelerate, wakati unafunga brake n.k...
Huu uzi madini tupu. Umenikumbusha kuna Noah ya Bro wangu ilikuwa inamisi asubuhi walibadili MAF sensor.
 
Ina pin 5 mkuu.

Okay kama ni 5 Pin basi kuna pin mbili za ground (moja ya IAT sensor na moja ya MAF sensor). Hizo tatu zilizobaki, Moja ni 12V supply ya IAT sensor, nyingine ni 5V supply ya MAF sensor na ya mwisho ni Signal line ya MAF sensor.

Hivyo kama alikuwa anapata shida kwenye cold start basi hiyo IAT sensor ilizingua, ila kwa sababu iko ndani ya jumba moja na MAF sensor ndio maana unaona kama kanunua MAF sensor mpya.
 
Asilimia kubwa ya matatizo ya engine kuzimazima yanasababishwa na components za umeme kama Sensors, Valves, solenoids n.k.

Engine inaweza kuzima muda wowote mfano wakati ipo idle, wakati unaaccelerate, wakati unafunga brake n.k.

Sababu zote zinazoweza kupelekea tatizo hili zinaingia katika makundi haya matano.

1. Loss of spark(kukosekana cheche kwenye engine)
Distributor

Hii hupeleka high voltage kwenye spark plug kulingana na firing order na katika muda sahihi. Pia baadhi ya distributor huwa na hall effect au magnetic mechanism kwa ajili ya timing kwenye ignition. Kama ikiwa na tatizo inaweza kupelekea umeme usifike kwenye spark plugs au kufika katika muda ambao si sahihi na hivyo kukosekana kwa cheche kwa wakati sahihi.

Coil on plug/Spark plug/spark plug wires/Ignition coil

Kama chochote kati ya hivi nilivyotaja hapa kikiwa kina shida inaweza kupelekea kukosekana kwa cheche au kuwa na cheche zisizo na nguvu kabisa. Hii inaweza kupelekea engine yako kuzima.

Crackshaft position sensor

Hii huwa na kazi kubwa tatu ambazo ni kufanya timing kwenye ignition, kupeleka RPM signal kwenye ECU na mwisho ni kujua speed ambayo engine inazunguka. Nayo pia kama ikileta shida basi engine yako itakuwa inazimazima.

Camshaft position sensor

Hii ndio sensor ambayo hujua ni cylinder gani firing inafanyika na kuweza kuestablish injector synchronization na coil firing sequence kwenye gari ambazo zinatumia Direct Ignition System (DIS). Hivyo kama nayo ikiwa na fault gari inaweza kuwa inazimazima.

2. Loss of fuel(Kukosekana kwa mafuta kwenye engine)
IAT sensor

Sensor hii ambayo husoma joto la hewa linaloingia kwenye engine ikiwa na shida basi huleta matatizo. Kama sensor hii inapeleka signal ya HOT tu basi engine itakuwa inapokea mafuta machache na hivyo hupelekea gari kuzimazima ikiwa umeliwasha bado la baridi(Hard cold start) au misi wakati wa asubuhi au engine ikiwa ya baridi. Kuna magari mengi hii sensor huwa inawekwa kwenye housing moja na MAF sensor, Hivyo mtu anaweza kuona alibadilisha MAF kusolve tatizo kumbe shida ilikuwa IAT sensor.

ECT sensor

Kama ilivo IAT sensor hii nayo huwa na tabia ya kupeleka signal ya HOT tu sometimes. ECU hudhani engine ni ya moto na hivyo kupeleka mafuta kidogo. Kama ni wakati wa asubuhi basi lazima gari itamisi na kuzimazima.

Oxygen sensor au A/F ratio sensor

Hii sensor hueleza hali ya engine kama ni Lean(mafuta kidogo) au Rich(mafuta mengi) kulingana na chemical reactions zilizofanyika kati ya exhaust gases na heating element. Kama signal ya too rich pekee ndio itakuwa inaenda kwenye ECU basi ECU itapunguza kiasi cha mafuta kinachokuja kwenye engine. Na hivo engine yako inaweza kumisi au kuzima.

Fuel pump

Kama fuel pimp ikiwa na fault inaweza kuleta mafuta kidogo au katika pressure ndogo. Hii inaweza kupelekea engine yako kumisi au kuzima muda wowote.

Injector Nozzle

Hizi sanasana kama zimeziba ndio huwa zinaleta shida. Ikiziba inaweza ikapitisha mafuta kidogo au isipitishe kabisa. Yote mawili yanaweza kupelekea engine yako kuzimazima.

3. Load(Mzigo mkubwa kuliko uwezo wa engine)
Mzigo siyo lazima uwe ule ulioubeba kwenye gari yako. Hata components za gari lenyewe zinaweza kusababisha load kwenye gari yako. Mifano ni

Torque converter.

Kwenye transmission kuna muda torque converter linapoanza kuharibika huwa lina kawaida ya kuengage clutch yake muda wowote, hivyo kama gari ikiwa idle basi lazima tu itazima kwa sababu mzigo utakuwa umeongezeka ghafla kwenye engine.

Torque converter clutch solenoid.

Kama ilivo kwa Torque converter pia TCC solenoid ikianza kufa huwa kuna muda inaamuru clutch ya torque converter iengage au ifanye delay kwenye kudisengage. Kama ikiengage wakati gari ipo idle basi engine itazima. Ikichelewa kudisengage wakati unaendesha gari yako itazima wakati wa kufunga brake.

MAP sensor

Hii ndio sensor inayodetect kiasi cha mzigo ambacho kinaendeshwa na engine. Mara nyingi ikifa diaphram yake huwa inatoboka hivyo taarifa kwenye ECU kwamba hakuna load yoyote, Hivyo mafuta yataletwa kidogo kwenye engine hata kama hewa inaingia nyingi. Hivyo engine inaweza kukosa nguvu na kuzima.

4. Kiasi kidogo/kikubwa cha hewa kwenye engine.(Mara chache)
Hii husababishwa na.

Air filter

Yes Air filter ikiziba lazima utakosa hewa ya kutosha kwenye engine hivyo hata mafuta yataletwa kulingana na hewa iliyopo. Hivyo haitazalishwa nguvu ya kutosha na hivyo engine inaweza kuzima.

Idle Air Control Valve(IACV)

Hii ndio valve inayohusika na kucontrol kiasi cha hewa kinachoingia kwenye engine wakati gari ipo idle (sailensa). Kama hii valve imekufa au imejaa carbon basi sailensa itakuwa inajipandisha au kujishusha yenyewe na kila siku utakuwa unaadjust. Ikiwa inajipandisha engine itakuwa inatumia mafuta mengi na kama inajishusha basi engine itakuwa inazimazima.

Throttle Position sensor

Hii kuwa inakuwa na resistive element ambayo kama itachubuka sehemu basi gari inaweza kuzima wakati unakanyaga accelerator.

Exhaust Gases Recirculation(EGR).

Kama EGR valve ni mbovu au imejaa carbon au solenoid yake imekufa basi inaweza kuleta shida hasa wakati engine ni ya baridi. Kama engine ni ya baridi basi unapowasha gari EGR valve inatakiwa kuwa imefunga. Kama itakuwa wazi lazima gari itamisi au kuzima kabisa.

MAF sensor

Hii huwa inapima flow rate ya hewa ambayo inaingia kwenye engine. Kama ikiwa na fault na ikawa inapeleka taarifa kwamba flow rate ni ndogo basi lazima mafuta nayo yataletwa kidogo. Hivyo kuna muda engine inaweza kuwa inazimazima.

5. Matatizo kwenye mifumo ya umeme.
Pia kama Battery au Alternator ya gari lako ni mbovu basi unaweza kukumbana na hii changamoto. Pia kwa sehemu kubwa ni relays zinaweza kusababisha hili tatizo. Niliwahi kuelezea kwenye uzi wangu mmoja kwamba relays zinapoanza kuchoka huwa zina tabia ya kuzima unapokuwa na electrical load kubwa.

Nimejitahidi kucover vitu vingi kadri nilivyoweza. Ingawa pia vinaweza vikawepo vitu vingine ambavyo vinaweza kupelekea engine yako kuzimazima. Kwa mfano leaks kwenye baadhi ya pipes n.k.
Gari haipokei silence mara tu baada ya kutoa plug na kurudisha....hadi nimenunua mpya lakini wapi japo kabla ya kuzitoa ilikuwa inawaka fresh. je tatizo ni nini?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom