Tatizo la engine ya gari kumisi (Engine Misfire), Sababu zake na baadhi ya solutions zake

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
3,327
9,321
Tatizo la engine kumisi(engine misfire) linaweza kusababishwa na mambo mengi sana kama vile, damaged, worn au bad spark plugs, weak ignition coil, broken, clogged au no current katika injector nozzle, fuel pressure regulator, fuel pump, vacuum leaks, sensors kama MAF, MAP, O2, IAT, ECT n.k. In fact sababu za engine kumisi zipo nyingi sana. Pia ni sababu hizihizi ambazo huwa zinapelekea muda mwingine gari kukosa nguvu.

Pia misfire zimetofautiana kuna mwingine akiwasha tu gari anakutana nayo, mwingine akiwa amebeba mzigo au mlimani, mwingine anakutana na misi akiwa anapunguza mwendo n.k.

Sasa ili kurahisisha kulipata tatizo ngoja tuigawanye engine kama hivi, Engine ni system(mfumo), na system kama engine tunategemea itakuwa na inputs (mifano ni hewa, mafuta na cheche), outputs (mifano ni nguvu(power) na moshi) na pia itakuwa na feedback loop (mfano ni Oxygen sensor). Sasa tuachane kwanza na output na feedback loop, asilimia zaidi ya 90% ya matatizo ya engine kumisi huwa yanasababishwa na inputs yaani mafuta(fuel), hewa(air) na cheche(spark). Pia katika kusolve matatizo kwenye magari ni vizuri kuanza na kitu ambacho hakichukui muda mwingi kukikagua.

Hivyo ngoja tuziangalie case 3 za inputs na nyingine 2 nitaziongeza mwisho. Haya nitakayoyaeleza hapa baadhi unaweza kuyafanya mwenyewe mwenye gari lakini mengine kidogo yanahitaji utaalamu. Pia kama kuna kitu nimekisahahu yoyote anaweza kuongezea. Haya sasa tuendelee...

MAFUTA
Kitu cha kwanza kuangalia ni kama mafuta ya kutosha yanafika kwenye engine. Kwenye engine huwa kunakuwa na fuel lines. Katika hizo fuel lines huwa kunakuwa na sehemu ya kuchomeka pressure gauge. Chomeka pressure gauge na weka switch on. Pressure gauge inauzwa siyo zaidi ya Tsh. 50k au unaweza kutafuta fundi mwenye pressure gauge akakupimia.

(a) Kama fuel pump na pressure gauge ni nzima pressure inatakiwa kusoma 35 psi mpaka 45 psi. Ndani ya muda wa dakika 2 pressure haitatakiwa kushuka chini ya 30 psi au kwenda juu ya 60 psi. Washa gari na kanyaga accelerator mara ya kwanza taratibu na mara ya pili kwa nguvu. Na mara zote pressure haitakiwi kwenda nje ya range niliyoitaja.

(b) kama utapata pressure nje ya hiyo niliyotaja hapo juu basi kuna shida kwenye pump yako au fuel pressure regulator.
Ukichomoa vacuum line kwenye regulator inatakiwa ukinusa pale kwenye regulator ulipochomoa ile pipe usisikie harufu ya petrol, kama unasikia harufu ya petrol maana yake diapram imetoboka na regulator ni mbovu pia wakati engine imewashwa ile vacuum pipe uliyochomoa inatakiwa iwe inasuck hewa kuingia kwenye engine. Kama regulator ni nzima basi fuel pump ni mbovu au fuel filter imejaa uchafu.

Fuel-Pressure-Regulator-508x381.jpg
1978_Honda_Civic.jpg
FPR-584x381.jpg

Kama kila kitu kipo sawa hapo juu basi mwisho utamalizia kupima injector nozzle. Njia ambayo wengi huitumia hapa ni kwa kutumia screw driver ndefu. Ule upande unaofungulia unauweka karibu na nozzle halafu mshikio unakuwa sikioni wakati engine inarun unatakiwa usikie kicking sound ambayo ipo consistent. Kama mlio haupo consistence basi nozzle ina shida pia kama husikii sauti yoyote basi injector nozzle inaweza kuwa imeziba au haipati umeme. Unaweza kucheck kama inapata umeme kwa kutumia torch light. Wengine hufanya cylinder power balance test kwa kuchomoa waya kwenye connector ya nozzle moja baada ya nyingine wakati umewasha gari. Kila unapochomoa waya mlio unatakiwa kubadilika, Kama mlio haubadiliki basi injector inashida au haipokei umeme.

CHECHE (SPARK)
Hiki ni kipengele kifupi kukagua kwa sababu unakagua vitu viwili tu yaani Spark plugs na coil on plug au spark plug na spark plug wires.

kwa upande wa spark plugs wengi huwa wanafanya spark jump test(yaani unachomoa spark plug wires moja baada ya nyingine wakati umewasha gari). Kama kuna kuna muda utachomoa na mlio hautabadilika basi hiyo waya uliyochomoa spark plug yake ina shida. Lakini pia kama mtu ana multimeter anaweza kupima resistance kwenye electrode ya spark plug(Hapa lazima ujue material yaliyotumika kutengeneza spark plug yako pia ujue kama spark plug yako ina resistor ndani au haina) na pia kuangalia kama kuna continuity kati ya electrode na ground(haitakiwi iwepo).

Kwa upande wa spark plug wires, Utakagua kama kuna sehemu zimechubuka. Pia unaweza kutumia spray bottle, utaijaza maji halafu utapulizia kwenye waya wako, kama kuna sehemu kuna leak basi utaona blue flashes zikitoka.(Kinachoescape kwenye hizi nyaya siyo umeme ila ni cheche hivyo kumwagia maji kwa sprayer haitakuletea shida yoyote). Hakikisha umekaa katika sehemu ambayo mwanga ni kidogo. Pia kama unajua material za huo waya unaweza kupima resistance kwa multimeter.

Kwa upande wa coil on plug, test pekee iliyopo ni kupima resistance ya primary coil na secondary coil then unarefer na zile zinazotolewa na manufacturer.

HEWA (AIR)
Hii huenda ikawa ndio sehemu ngumu kuigundua hasa kwa baadhi ya cases. Pia misfiring nyingi zinazosababishwa na njia ya hewa hutokea ama ukiwa unaaccelerate au wakati wa kudecelerate. Ni mara chache sana kukutana na misfire ambayo inasababishwa na njia ya hewa wakati engine ipo idle.

Kitu cha kwanza kabisa kagua air filter kama chafu safisha. Pia kagua kama kuna leak yoyote katika njia ya hewa kuanzia kwenye air filter mpaka kwenye intake manfold kama hutaona tatizo basi shida inaweza ikawepo kwenye mojawapo ya sensors zilizopo kwenye njia ya hewa na intake manfold ( MAF sensor, MAP sensor, TPS sensor(mara chache) na IAT sensor). Pia ECT sensor na IAT sensor zinaweza kupelekea misfire wakati wa cold start. Hapa ni vizuri ukaanzie kwenye OBD II scanner kama gari yako ina port ya OBD 2 otherwise ni suala la kuanza kutest sensor mojamoja.

NDANI YA ENGINE
Ndani ya engine poor compression inaweza kusababisha misfire. Poor compression inaweza kusababishwa na Piston rings kuisha, cylinder bore kutanuka, cylinder head gasket kuharibika, Intake na exhaust valves kutofunga vizuri(carbon kuganda kwenye valves), n.k. Hapa ukienda kufanya cylinder compression test utapata majibu.

NYONGEZA
Leak yoyote kwenye EGR valve au hoses za EGR au Kwenye exhaust manfold kabla ya Oxygen sensor au Oxygen sensor mbovu zinaweza kupelekea misfire. Na siyo kila muda hiyo EGR na O2 sensor utakuletea code kwenye scanner yako. Hivyo kama mtu akifanya OBD II diagnosis ni vizuri akasoma live data za Fuel trim.

Kwa kawaida Fuel trim inatakiwa kuwa -3 mpaka +3 kwa Short term(ST) fuel trim au -10 mpaka +10 kwa Long term(LT) fuel trim. Kama una chini ya -3 fuel trim kwenye ST na chini ya -10 fuel trim kwenye LT au moja wapo kati ya hizo maana yake kuna vacuum leak mahali na hivyo ECU imeamuru kwamba mafuta yaje machache kwenye engine kwa kupunguza muda wa Injector nozzle kuwa wazi. Hivyo lazima engine yako itamisfire.

MWISHO

Pia soma Mada hizi
- Mambo haya yanaweza kuharibu battery ya gari yako. Ni vema kuyaepuka

- Baadhi ya solutions za matatizo ya automatic gearboxes

- Baadhi ya watu mnaofanya Computer diagnosis kwenye magari mnawamislead wateja wenu na kuwaingiza gharama zisizo za lazima

- Kuna umuhimu mkubwa sana kufanya check up ya mifumo ya umeme na electronics kwenye gari yako

- Muhimu: Zijue athari za kuondoa thermostat kwenye gari yako
 
uko vizuri sana kwa kusomea. Ingawa mafundi wengi ni ujanja ujanja hata haya majina umeyataja hawayajui.sasa ukute umesoma hivyo halafu uliwahi kuwa fundi wa modification itakuwa ni balaaa

Shukrani mkuu...
 
Tatizo la engine kumisi(engine misfire) linaweza kusababishwa na mambo mengi sana kama vile, damaged, worn au bad spark plugs, weak ignition coil, broken, clogged au no current katika injector nozzle, fuel pressure regulator, fuel pump, vacuum leaks, sensors kama MAF, MAP, O2, IAT, ECT n.k. In fact sababu za engine kumisi zipo nyingi sana. Pia ni sababu hizihizi ambazo huwa zinapelekea muda mwingine gari kukosa nguvu...

Jitu shukrani sana kwa Elimu murua unayotoa.

Nikipata shida nitakutafuta jamaa.
 
Tatizo la engine kumisi(engine misfire) linaweza kusababishwa na mambo mengi sana kama vile, damaged, worn au bad spark plugs, weak ignition coil, broken, clogged au no current katika injector nozzle, fuel pressure regulator, fuel pump, vacuum leaks, sensors kama MAF, MAP, O2, IAT, ECT n.k. In fact sababu za engine kumisi zipo nyingi sana. Pia ni sababu hizihizi ambazo huwa zinapelekea muda mwingine gari kukosa nguvu.

Pia misfire zimetofautiana kuna mwingine akiwasha tu gari anakutana nayo, mwingine akiwa amebeba mzigo au mlimani, mwingine anakutana na misi akiwa anapunguza mwendo n.k.

Sasa ili kurahisisha kulipata tatizo ngoja tuigawanye engine kama hivi, Engine ni system(mfumo), na system kama engine tunategemea itakuwa na inputs (mifano ni hewa, mafuta na cheche), outputs (mifano ni nguvu(power) na moshi) na pia itakuwa na feedback loop (mfano ni Oxygen sensor). Sasa tuachane kwanza na output na feedback loop, asilimia zaidi ya 90% ya matatizo ya engine kumisi huwa yanasababishwa na inputs yaani mafuta(fuel), hewa(air) na cheche(spark). Pia katika kusolve matatizo kwenye magari ni vizuri kuanza na kitu ambacho hakichukui muda mwingi kukikagua.

Hivyo ngoja tuziangalie case 3 za inputs na nyingine 2 nitaziongeza mwisho. Haya nitakayoyaeleza hapa baadhi unaweza kuyafanya mwenyewe mwenye gari lakini mengine kidogo yanahitaji utaalamu. Pia kama kuna kitu nimekisahahu yoyote anaweza kuongezea. Haya sasa tuendelee...

MAFUTA
Kitu cha kwanza kuangalia ni kama mafuta ya kutosha yanafika kwenye engine. Kwenye engine huwa kunakuwa na fuel lines. Katika hizo fuel lines huwa kunakuwa na sehemu ya kuchomeka pressure gauge. Chomeka pressure gauge na weka switch on. Pressure gauge inauzwa siyo zaidi ya Tsh. 50k au unaweza kutafuta fundi mwenye pressure gauge akakupimia.

(a) Kama fuel pump na pressure gauge ni nzima pressure inatakiwa kusoma 35 psi mpaka 45 psi. Ndani ya muda wa dakika 2 pressure haitatakiwa kushuka chini ya 30 psi au kwenda juu ya 60 psi. Washa gari na kanyaga accelerator mara ya kwanza taratibu na mara ya pili kwa nguvu. Na mara zote pressure haitakiwi kwenda nje ya range niliyoitaja.

(b) kama utapata pressure nje ya hiyo niliyotaja hapo juu basi kuna shida kwenye pump yako au fuel pressure regulator.
Ukichomoa vacuum line kwenye regulator inatakiwa ukinusa pale kwenye regulator ulipochomoa ile pipe usisikie harufu ya petrol, kama unasikia harufu ya petrol maana yake diapram imetoboka na regulator ni mbovu pia wakati engine imewashwa ile vacuum pipe uliyochomoa inatakiwa iwe inasuck hewa kuingia kwenye engine. Kama regulator ni nzima basi fuel pump ni mbovu au fuel filter imejaa uchafu.

View attachment 1496526View attachment 1496527View attachment 1496528

Kama kila kitu kipo sawa hapo juu basi mwisho utamalizia kupima injector nozzle. Njia ambayo wengi huitumia hapa ni kwa kutumia screw driver ndefu. Ule upande unaofungulia unauweka karibu na nozzle halafu mshikio unakuwa sikioni wakati engine inarun unatakiwa usikie kicking sound ambayo ipo consistent. Kama mlio haupo consistence basi nozzle ina shida pia kama husikii sauti yoyote basi injector nozzle inaweza kuwa imeziba au haipati umeme. Unaweza kucheck kama inapata umeme kwa kutumia torch light. Wengine hufanya cylinder power balance test kwa kuchomoa waya kwenye connector ya nozzle moja baada ya nyingine wakati umewasha gari. Kila unapochomoa waya mlio unatakiwa kubadilika, Kama mlio haubadiliki basi injector inashida au haipokei umeme.

CHECHE (SPARK)
Hiki ni kipengele kifupi kukagua kwa sababu unakagua vitu viwili tu yaani Spark plugs na coil on plug au spark plug na spark plug wires.

kwa upande wa spark plugs wengi huwa wanafanya spark jump test(yaani unachomoa spark plug wires moja baada ya nyingine wakati umewasha gari). Kama kuna kuna muda utachomoa na mlio hautabadilika basi hiyo waya uliyochomoa spark plug yake ina shida. Lakini pia kama mtu ana multimeter anaweza kupima resistance kwenye electrode ya spark plug(Hapa lazima ujue material yaliyotumika kutengeneza spark plug yako pia ujue kama spark plug yako ina resistor ndani au haina) na pia kuangalia kama kuna continuity kati ya electrode na ground(haitakiwi iwepo).

Kwa upande wa spark plug wires, Utakagua kama kuna sehemu zimechubuka. Pia unaweza kutumia spray bottle, utaijaza maji halafu utapulizia kwenye waya wako, kama kuna sehemu kuna leak basi utaona blue flashes zikitoka.(Kinachoescape kwenye hizi nyaya siyo umeme ila ni cheche hivyo kumwagia maji kwa sprayer haitakuletea shida yoyote). Hakikisha umekaa katika sehemu ambayo mwanga ni kidogo. Pia kama unajua material za huo waya unaweza kupima resistance kwa multimeter.

Kwa upande wa coil on plug, test pekee iliyopo ni kupima resistance ya primary coil na secondary coil then unarefer na zile zinazotolewa na manufacturer.

HEWA (AIR)
Hii huenda ikawa ndio sehemu ngumu kuigundua hasa kwa baadhi ya cases. Pia misfiring nyingi zinazosababishwa na njia ya hewa hutokea ama ukiwa unaaccelerate au wakati wa kudecelerate. Ni mara chache sana kukutana na misfire ambayo inasababishwa na njia ya hewa wakati engine ipo idle.

Kitu cha kwanza kabisa kagua air filter kama chafu safisha. Pia kagua kama kuna leak yoyote katika njia ya hewa kuanzia kwenye air filter mpaka kwenye intake manfold kama hutaona tatizo basi shida inaweza ikawepo kwenye mojawapo ya sensors zilizopo kwenye njia ya hewa na intake manfold ( MAF sensor, MAP sensor, TPS sensor(mara chache) na IAT sensor). Pia ECT sensor na IAT sensor zinaweza kupelekea misfire wakati wa cold start. Hapa ni vizuri ukaanzie kwenye OBD II scanner kama gari yako ina port ya OBD 2 otherwise ni suala la kuanza kutest sensor mojamoja.

NDANI YA ENGINE
Ndani ya engine poor compression inaweza kusababisha misfire. Poor compression inaweza kusababishwa na Piston rings kuisha, cylinder bore kutanuka, cylinder head gasket kuharibika, Intake na exhaust valves kutofunga vizuri(carbon kuganda kwenye valves), n.k. Hapa ukienda kufanya cylinder compression test utapata majibu.

NYONGEZA
Leak yoyote kwenye EGR valve au hoses za EGR au Kwenye exhaust manfold kabla ya Oxygen sensor au Oxygen sensor mbovu zinaweza kupelekea misfire. Na siyo kila muda hiyo EGR na O2 sensor utakuletea code kwenye scanner yako. Hivyo kama mtu akifanya OBD II diagnosis ni vizuri akasoma live data za Fuel trim.

Kwa kawaida Fuel trim inatakiwa kuwa -3 mpaka +3 kwa Short term(ST) fuel trim au -10 mpaka +10 kwa Long term(LT) fuel trim. Kama una chini ya -3 fuel trim kwenye ST na chini ya -10 fuel trim kwenye LT au moja wapo kati ya hizo maana yake kuna vacuum leak mahali na hivyo ECU imeamuru kwamba mafuta yaje machache kwenye engine kwa kupunguza muda wa Injector nozzle kuwa wazi. Hivyo lazima engine yako itamisfire.

MWISHO
Kama una tatizo kwenye engine au automatic gearbox unaweza kunipigia kwa namba 0621221606 au unaweza kubonyeza 👉👉👉 HAPA ili kunitumia message whatsapp moja kwa moja.

Pia soma Mada hizi
- Mambo haya yanaweza kuharibu battery ya gari yako. Ni vema kuyaepuka

- Baadhi ya solutions za matatizo ya automatic gearboxes

- Baadhi ya watu mnaofanya Computer diagnosis kwenye magari mnawamislead wateja wenu na kuwaingiza gharama zisizo za lazima

- Kuna umuhimu mkubwa sana kufanya check up ya mifumo ya umeme na electronics kwenye gari yako

- Muhimu: Zijue athari za kuondoa thermostat kwenye gari yako
nishachukua namba yako si kwamba hadi nipate tatizo nitakutafuta kwa ushauri maana bora kinga kuliko tiba
 
Mkuu nina suzuki swift 1.3 M13A engine iliwasha taa ya check engine alafu inazima kupeleka kwa fundi nikaambiwa fuel pump imekufa nikanunua nyingine lakini bado likaendelea kwa mabadiliko kidogo kwamba check engine inawaka lakini gari haizimi kupeleka tena kwa fundi wakasafisha O2 sensor baadae gari ikaanza kukosa nguvu lakini taa haiwaki tukafungua coil tukaona kuna moja imelegea na pia plug haichomi nikanunua mpya baadae gari ikaenda vizuri sema ukipunguza mwendo mlimani rpm inashuka ukikanyaga mafuta inarudi Sawa nikarudi kwa fundi akasafisha fuel injector tatizo limepungua kwa asilimia 90 lakini huku kushtuka nakumalizaje?
Nipo Kgm
 
Pole sana mkuu. Hii gari umeanza nayo au umeinunua mkononi mwa mtu?!
 
Jamani plug no 2 haichomi inaungua, kuna fundi anasema valve zimekonda tubadilishe .
Jamani ma engineer tatizo itakuwa mini hapo
 
Back
Top Bottom