Natty Bongoman
JF-Expert Member
- Oct 10, 2008
- 403
- 191
Habari wanaJF,
Kuhusiana na suala la elimu bora Tanzania, mimi nadhani tulio wengi tumefikia mahali tunafikiri kufundishwa kwa kiswahili kutaboresha elimu yetu.
Sijue nyie wenzangu, ila mimi nilishangilia nilipopata D kiswahili form four national exam. Pointi hapa ni kwamba kiswahili chetu cha kila siku mitaani na majumbani sio kama nilichokiona ndani ya mtihani wa form four. Yaani kwa kweli hicho kiswahili kingetumika ndani ya mtihani wa Physics (Fizikia?) ningepata changamoto ya kuchanganua lugha afu kuchanganua somo, nahisi ningetumia mda mrefu zaidi.
Maoni yangu,
1. Kiswahili fasaha unachokutana nacho ndani ya elimu za juu, wengi hatukijui vizuri - hata tuliokulia Dar na kanda zote za pwani ... sasa sembuse wa mikoani? Tukitaka kiswahili kiwe lugha ya kufundishia, itabidi tutie mkazo katika kufundisha kiswahili fasaha na kipana kuanzia shule za awali, na espesheli kukazia yale maneno ya kisayansi, kifundi, kimahesabu, nk kwa sababu ni maneno ambayo hatutumii sana katika maongezi ya kila leo. La sivyo kama hatujui kiswahili fasaha, tutarudi kukariri mashuleni hata kama lugha ya kufundishia ni kiswahili.
2. Hizi nchi nyingi tunazozisifia kuwa na elimu bora zina tabia ya kurutubisha elimu. Mtoto anasomewa vitabu, wengine kabla hata hawajaongea vizuri. Mtoto akiwa shuleni, wazazi wanasaidia na maswala ya shule - homework nk. Leo hii siwezi amini kuna wazazi (kati ya wazazi wawili) ambao hawana elimu ya kumfundisha ama kumsaidia na maswala ya shule mtoto wa awali ama darasa la kwanza. Basi tulio wengi hatuwazii ama tuna uvivu wa kumtayarisha mtoto kimasomo kuanzia nyumbani kabla hawajaanza shule.
3. Tuzingatie fani ya ualimu kuwa ni ya muhimu sana kiasi kwamba hata uchaguzi wa watakaosomea ualimu uwe wa msingi. Tunategemea nini serikali inapopeleka waliofeli sekondari kwenda kusomea ualimu na uaskari? Hatuwezi pata walimu wenye uwezo mzuri kwa mfumo huu. Naamini wako wengi tu wenye ubongo na uwezo wakitaka kuwa waalimu lakini mshahara hauwavutii kabisa. Ni mda serikali na uongozi wa elimu nchini kuzingatia nani anachaguliwa kuwa mwalimu na nini wampe mwalimu awe na motisha mzuri wa kufundisha.
4. Mwanafunzi bora ni yule anaejiamini. Kujiamini kunakuja na malisho ya ubongo wa mtoto. Kwa mfano tabia potofu za kumuaminisha mtoto wazungu wana akili kuliko sisi - zinamfanya mtoto asijiamini na asishindane na wazungu kwa mfano huu.
5. Tutambue na kuzingatia kwamba kutojua kitu sio ujinga ila ni kutokuwa na elimu kuhusiana na kitu hicho. Ina maana ukijielimisha utakijua hicho kitu vizuri hata kuliko yule aliekucheka mwanzoni. Epuka sana sana kutumia hivi vipimo vya kizungu wanaviita IQ TEST kupima watoto wetu. Natambua mzungu alitumia hizi test kujipandisha...
Hebu fikiri staili zao za hizi test... ni kama kumuuliza mtoto wa kijijini alama ya 'pundamilia' barabarani ina maana gani, afu asipojua unamwandika ni mjinga.