Tatizo la Elimu Tanzania sio Pesa pekee bali mbinu ya kufundisha na ubunifu

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,598
8,738
Nimesikia watu wengi kwenye mtandao wakipigia debe elimu ya bure!! tatizo la pesa kweli lipo lakini vilevile hatuna madarasa ya kisasa, walimu wa kutosha na mbinu mpya za ufundishaji.

Tanzania haitaweza kufanya yote haya niliyoyataja kwa Tanzania nzima kwani wananchi wa Tanzania wametapakaa sana nchini na si rahisi kujenga shule kila mahali zenye kila kitu. Sasa badala ya kupiga debe ya elimu bure ni lazima tujiulize je ungekuwa na budget hiyo ungefanya nini tofauti kufundisha watoto wote.

Kwa wenye uwezo wa kulipia shule hawana budi kulipa hakuna sababu ya msingi ya nchi masikini kama Tanzania watoto waliotokea kwenye familia zenye uwezo wasome bure lakini kwa wale wasio na uwezo nakubaliana na wengi kwenye hilo. Mimi nilishatoa mawazo hapa yafuatayo

1. Wanafunzi wa vyuo vikuu wanao chukua mikopo na dhamana ya serikali ni lazima wafundishe miezi sita kabla ya kupewa vyeti vyao kama ilivyokuwa JKT. Hii itasaidia kupunguza gharama sana.
2. Kwenye ujenzi wa shule za Primary na Sekondari wakijenga wahusishe wenyeji. Hii itasadia wenyeji kuona ni part ya maendeleo yao na hii tabia wanafanya sana wachagga badala ya kusubiri serikali ifanye kila kitu.
3. Boarding School- Serikali ianzishe Boarding school kwa wilaya ambazo zina watu wachache hii itasaidia badala ya kuwa na shule nyingi kila mahali ni bora uwe na shule moja kubwa sehemu moja na watoto wa Primary na sekondari waweze kwenda.
4. Serikali isiruhusu shule zinazofelisha zifungwe au wabadilishe uongozi. Kama tatizo ni utamaduni wa jamii kama shule nyingi za Zanzibar wapeleke watoto shule za boarding.
5. Shele binafsi-Serikali ipige mahesabu ya gharama kwa mwanafunzi mmoja na iruhusu watu binafsi kujenga shule za kisasa na kuwapa hizo pesa shule zikifunguliwa kwa mwanafunzi. Kama zinafelisha zinafungwa
 
Mbona huwa mnakwepa mishahara ya walimu inayotosha kwa mwezi? Hata mlete malaika kutawala nchi hii bila kuwajali walimu mnajilisha upepo bure, hata mjenge madarasa, vitabu na mlipane posho nyingi sana, bila kumlipa mwalimu vizuri mtatoka povu sana Elimu haitapanda kamwe. Huo ndio msimamo wa walimu.

Poleni kwa kukwepa kutibu tatizo la msingi. Aluta continua kati ya Serikali Vs Walimu hadi kitaeleweka tu.
 
MotoYaMbongo

Hapo kaka umeongea point kubwa sana ambayo japo wanaifumbia macho lakini ndio ukweli wenyewe,wengi wanakimbilia kusema walimu viwango vyao vya Elimu ni vidogo hivyo haiwezekani kuwalipa mishahara mikubwa,lakini ikumbukwe kuwa walimu hawahawa ukiwalipa mishahara ya kuridhisha kulingana na viwango vya Elimu zao wapo watakaojiendeleza na tutaweza kuvutia watu wengine kujiunga na Fani ya ualimu.

Walimu hawana kipato kingine chochote pembeni ya mishahara yao,hivyo ni bora wangerudishiwa posho kama za ufundishaji,au za mazingira magumu ili wawe na moyo wa kwenda kufundisha hata sehemu zisizofikika kwa urahisi,Ni aibu kufikiria kuwa tunaweza kuendeleza Elimu wakati huyo mtoaji Elimu(mwalimu)anadharauliwa hata na kabeba mafaili ka masijala ya halmashauri..
 
Last edited by a moderator:
1. Wanafunzi wa vyuo vikuu wanao chukua mikopo na dhamana ya serikali ni lazima wafundishe miezi sita kabla ya kupewa vyeti vyao kama ilivyokuwa JKT. Hii itasaidia kupunguza gharama sana.[/B]

Nasapoti wazo lako kaka,na kama inawezekana hawa wanaopatiwa mikopo kama ulivyoainisha hapo kwenye namba 1 waende mashuleni si kwa miezi sita bali mwaka mmoja.

Na hii itasaidia sana kuwa na uhakika wa walimu wa kutosha muda wote wa mwaka wa masomo katika maeneo yote ta nchi..
 
Elimu bure na yenye viwango inawezekana bila shaka, inahitajika dhamira tu.

Serikali ya sasa inshindwa kupata ujasiri wa kufanya hii kitu sababu ya ufisadi, wanajua kutoa elimu bure ni kitu cha gharama kubwa sana hivyo wanaogopa kukosa chakuiba.
 
Tanzania ni kubwa sana hatuwezi kuwa na shule nzuri kila kijiji! hivyo kwa vijiji ambavyo vina watu wachache wafungue Boarding Schools na hizo pesa na walimu wawekwe sehemu moja. Kwenye Budget ni lazima tuamue pesa itumike wapi sasa hivi mfano serikali ina sera za kujenga shule lakini kama wangefikiria vizuri wangeweza kutumia hiyo pesa kwa mishahara. Watanzania tuna Tatizo hilo pesa ni tatizo na nchi ni masikini hivyo inabidi tufanye vitu kwa umakini huwezi kuweka sera ya kujenga shule bila ya kuangalia idadi ya watu, walimu n.k na pesa hizo hizo ndiyo za mishahara kwani hii ni wizara moja!. Kuna shule za sekondari zenye nafasi nzuri je ni kwanini serikali isikuze hizo shule kwa kujenga mabweni zaidi na madarasa.
 
sasa hoja yangu inaonekana baada ya matokeo ya kidato cha nne.
 
Mbona huwa mnakwepa mishahara ya walimu inayotosha kwa mwezi? Hata mlete malaika kutawala nchi hii bila kuwajali walimu mnajilisha upepo bure, hata mjenge madarasa, vitabu na mlipane posho nyingi sana, bila kumlipa mwalimu vizuri mtatoka povu sana Elimu haitapanda kamwe. Huo ndio msimamo wa walimu.

Poleni kwa kukwepa kutibu tatizo la msingi. Aluta continua kati ya Serikali Vs Walimu hadi kitaeleweka tu.

Mkuu!
Ni kweli kabisa mishahara ya walimu nayo ni tatizo kubwa kwa sasa.

Ebu sote tuiombe serikali kuongeza mishahara ya walimu na ikiwezekana kufufua ule mfumo wa ukaguzi wa shule kuanzia

maudhulio ya walimu ya kila siku,mada wanazofundisha kwa siku na ikiwezekana pawepo na utaratibu wa kuwamotisha

walimu wanamaliza mada zao mapema.

Na kama mishahara itaongezwa alafu pasiwepo mabadiliko yoyote,hapa ni bora kuifanya elimu iwe kwa wote (isitolewe kimatabaka).Nasema hivi nikiwa na maana ya kutokuwepo kwa shule za binafsi ili kuondoa dhana ya tabaka fulani kuendelea kuodhi kila kitu hata kama tabaka lingine lina uwezo huo lakini unamezwa kielimu na tabaka la juu lenye elimu,pesa na nafasi.

Kama kweli tunapenda elimu yetu iwe juu ni bora isifanywe biashara,kama itaendelea kufanya biashara tujue kuwa hata matokeo yatakuwa ya kibiashara zaidi.
 
Back
Top Bottom